punguzo umekuja na wazo zuri. Mimi najiuliza swali moja. Je nisababu zipi za msingi zinaziwafanya wafanya biashara wagome kutumia hizo mchine. Je ni kwasababu ya bei zake (initial cost) au kwavile wanajua kuwa utaratibu huu utawafanya wajulikane kipato chao basi hawataki kuzitumia. Je ni kwavile hawaoni faida ya wao kulipa kodi na hivyo kutafuta mwanya wa kuendelea kukwepa kulipa kodi?
Kuna vitu viko wazi ambavyo mimi naviona. Ukusanyaji wa kodi kwa TRA bado upo kwa kiwango cha chini, cha kusikitisha hata hicho kidogo kinachokusanya ni kiwango kidogo kinachofanya kazi za maana/kinachotumiwa kwa maendeleo. Kiasi kikubwa kinaishia mikononi mwa wachache kwa njia za deal deal. Na hiyo inawafanya watu wasione umuhimu wa kulipa kodi.
Pili hata wale wenye EFD tayari bado hawazitumii inavyotakiwa. Utakuta bado wanatumia risti zao za zamani au hatoi risti kabisa. Na mara nyingi sana na hii imenitokea mara kibao wafanya biashara anakwambia bei ya kifaa hiki ni mfano laki 7 ukitaka risti au laki 5.5 bila risti. Mteja yoyote atakimbilia kuchukua bidhaa bila risti na mwisho wa siku mfanya biashara ananufaika kwa kukwepa kodi. Lakini ki u-halisia huwa wanaongeza bei kumtisha mteja na hivyo kusababisha mteja akubali kutochukua risti. TRA needs to workout that, vinginevyo mtakuwa na hizo EFD lakini bado efficiency yenu ya kukusanya kodi itakuwa ndogo. Usahauri wangu kama zipo machine zinazoweza kupatikana kwa bei ndogo kama ulivyo pendekeza itakuwa ni jambo zuri. Lakini pia wanaweza kuwakopesha wafanya biashara na wakawa wanawakata hela yao kidogo kidogo hadi itakapo isha. Tusilazimishe kununua machine hizo kwa hela ndefu hivyo. Si kila mfanya biashara anahela ya kutoa kwa haraka na hasa anapogundua kuwa hicho kifaa hakimsaidi kama wanavyoelezwa eti kutunza kumbukumbu. Ingekuwa kweli wao wanaona kitawasaidia basi wangekimbilia, kumbukumbu zao wanazo ila huwa wanajaribu kuzificha na kwasababu TRA hawanauwezo wa kuzipata hujikuta wakiwakadilia malipo kidogo ya kodi licha ya kwamba utaona wengi wanalalamika kama vile wamekadiliwa kwa kiwango cha juu.
Wito wangu: Serikali ijitahidi kutumia vizuri kodi za wananchi, hii itawafanya wananchi ambao ndo walipa kodi waone kwamba kodi yao inatumika vizuri. Binafsi huwa nasikitika naposikia watu wamepiga hela za miradi flani, au wanafanya ubadhilifu, au wanatumia vibaya magari ya serikali. Wanafanya uchakachuzi katika sekta mbalimbali huwa nasikitika sana. Najua mwisho wa siku sisi ndo tunaumia maana hizo ni kodi zetu. Ukweli ni kwamba kama wafanyakazi wa nchi hii nao wangekuwa na option ya kukwepa kulipa kodi ya mapato (pay as you earn) watu wasingelipa. Hakuna mtu anayegoma kulipia huduma na hasa anapoona huduma zinzotolewa ananufaika nazo.
Watu hawana hospitali, viongozi wanakimbizwa nje wanapougua, shule zetu zinakwisha watoto wa viongozi wanasomeshwa nje au shule private nzuri. Barabara mbovu, tembelea maeneo wanapokaa wao. Huduma za maji na umeme mbovu kwao wanapata masaa yote. Sasa mtu anajiuliza kwanini nilipe kodi. Kwanini nami nisifanye saving itakayo nisaidia baadaye nitakapo ihitaji.