Wabongo tumezoea sana wizi na kukwepa, wafanya biashara wamezoea super profit, kwa vile sasa mashine zitaonyesha kila kitu, nanataka kuzigomea!. Mbona wahindi wanazitumia na hawagomi?!.
Anayelipa kodi ni end user, hivyo anayepaswa kugoma ni mteja baada ya kupandishiwa bei kufuatia wafanya biashara kulipa kodi!, na sio wafanya biashara wagome kuuza, kisa kodi iko juu!. Huu sasa ni mwanzo mzuri wa hivi vibiashara mchoro mchoro vifungwe zibaki biashara halali tuu!.
Kwa upande wa EFD, nako ni wizi mtupu!, mashine inauzwa dola 100, hapa unauziwa dola 1000!.
Ukiamua kununua mwenywe, wale maajent wa TRA hawakubali ku install!.
Mijimashine yenyewe approved kwa Tanzania yote inatumia windows only kwa sisi tunaotumia mac, tunalazomika kununua computer ya window kwa ajili ya EFD tuu!.
Huu pia ni nyanyasaji!.
Pasco.
Pasco.
Nimekusoma Mkuu Pasco! Labda nichangie kidogo
Mosi wazo la TRA kuanzisha matumizi ya hizi machine ni vizuri na linapaswa kuungwa mkono japo jambo linapotambulishwa na kutumika kwa mara ya kwanza linakuwa na changamoto nyingi. katika hili nikubaliane na wewe kuwa kuna changamoto ambayo TRA wanatakiwa kuzifanyia kazi........
Ila kuna upotoshaji ambao unafanyika katika zoezi hili kwa mfano Kariakoo siyo kweli kuwa wafanyabiashara wa KKoo wote wanatakiwa kutumia hizi machine soko la kariakoo na viunga vyake vinawafanya biashara zaidi ya 60,000 lakini ambao wamelengwa kwenye zoezi hili ni 38,000 tu ambao Wamachinga,mama ntile hawahusiki na kwa maelezo ya TRA yeyote ambaye anaona kuwa pato lake halifiki 14mil kwa mwaka aseme ataondolewa kwenye zoezi na List ya hao wafanyabiashara ipo ila watu wameamua kugeneralize kuwa ni watu wote:
TRA wamelitanganza international tender kwa manufacturer wa mashine hizi na Jumla ya Kampuni 8 zilipita kwenye hii zabuni. na hizi machine zipo tailor kwa mazingira ya kitanzania kwa maana kwamba lugha Swahili/english na specification walizotumia ni kutoka TRA ambazo zitawesha zoezi hili kwenda smoothly. Kitu ambacho kinapelekea kuwa ukinunua machine kutoka kwa wazalishaji wengine mbali ya hao 8 machine yako itakuwa tofauti na haisomani na system ya TRA.
BEI YA MASHINE:
Gharama halisi ya Machine hizi kulingana na uwezo na aina ya biashara unayofanya zina range $245- 280 CIF + Distribution cost+Margin+ Other cost inaleta around $520 ukiconvert kwenye Tsh...unapata 800,000 ila wasambaji wamekuwa wakiuza mpaka laki 6 kwa kila machine.
Tatizo la Kkoo!
Mkuu Pasco tuwe wakweli na tuweke itikadi zetu pembeni hata kama CCM siwapendi! Issue ya EFDS ni Mtolea Ngoma tu ila kunasababu nyingine nyingi ambazo zimeambatana na hii. ila kwa muda mrefu wafanyabiashara wa kkoo wamekuwa cyo walipa kodi wazuri. na wengi wametajirika cyo kwasababu biashara inalipa bali ni kwamba hawalipi kodi.
Kutokana na mabadiliko ya kiuchumi biashara kariakoo zimedorora sana wale wateja waliokuwa wanatoka Malawi,Zambia,Congo,Zimbabwe na Kwingineko kuja kujumua Kkko hawaji tena.
Mosi wengine wanakwenda wenye China,wengine wananulia Uganda ambako wako wanaruhusu nguo kuingia bure au kwa kodi nafuuu kushinda sisi na kubwa zaidi kuna wakinga wamefungua magodauni Mbeya wanaenda kuchukua mizigo china na maeneo mengine wanauzia mbeya so wazambia, congo na malawi wanaona ni bora wanunulie Mbeya.
Kitendo cha TRA kutambulisha huu mfumo wa machine ambayo kila bidhaa unayouza kodi inakatwa automaticaly inaonekana ni Mwiba mkali kwa wafanyabiashara ambao cyo wakweli.
Na kwa mujibu wa wafanyabiashara issue cyo Bei ya Machine ni kwamba hawataki machine ziwepo kabisa!
Tuendelee kuelimisha kwa vile vidogo tunavyovijua kuliko kupotosha!
Naomba kuwasilisha mkuu!