Ukweli kuhusu baadhi ya mabinti wa kilokole

Ukweli kuhusu baadhi ya mabinti wa kilokole

Mkuu usihusishe tabia/udhaifu wa mtu na Imani msingi wa hoja yako ni ulokole,yawezekana ulikutana na binti mwenye matatizo yake na tabia isiyofaa lkn sbb anasali kwa walokoke basi unahisi mabinti wote wako hivyo sio kila anayesali kwa walokole ameokoka....unaweza ukasali lkn hujaokoka maana ya KUOKOKA NI KUACHA DHAMBI kama anatenda dhambi huyo hajaokoka.
Soma uzi vizuri. Uchunguzi sijafanya kwa mmoja
 
Aisee hapa ninapokaa kuna kibinti kinafanya kazi za ndani kwa ndugu yake alafu ni msabato (wote wasabato) yani kafika wiki moja kaenda kanisani mara tano jmosi kusali kutoka kawaida ni sa tano lakin yeye atarudi sa tisa au kumi anajiamini sana hana swaga za kutongozwa yani ukimuangalia anaonekana haitaji masuala ya uasherati sasa huu uzi umenifumbua macho kumbe kiu akatia juu kwa juu bora niwe nasali nimejifungia ndani maana isije ikaonesha wote wazinzi
Utafeli sana mkuu kuwafananisha wasabato na walokole kama haujui walokole ni madhehebu ya aina ya TAG, EAGT, Ministry (huduma za maombezi za watu binafsi) bila kusahau dhambi inayowatesa walokole wengi ni uzinzi na uasherati....
 
Utafeli sana mkuu kuwafananisha wasabato na walokole kama haujui walokole ni madhehebu ya aina ya TAG, EAGT, Ministry (huduma za maombezi za watu binafsi) bila kusahau dhambi inayowatesa walokole wengi ni uzinzi na uasherati....
Ivi hawafanani kwenye masuala ya ibada kwa mfano nauliza2 maana sijui vizuri
 
Yaani wewe mwenyewe ni muasherati na mzinzi halafu unawasema wenzio. Mnafiki wewe.Usihukumu usije ukahukumiwa
 
Alafu wanatabia ya kuwadharau watu ambao hawaja okoka yani wanawaona kama watu ambao tayari wamefika motoni na ni ndugu na shetani...

Alafu ni wajuaji sanaa kwenye Mambo yote wanajikuta ni walimu wa mahusiano... Kutokana na sumu waliyo mezeshwa kanisani
 
Nadhani huyo demu wko ndo yupo kwenye kanisa la kishetani mama mchungaji gani wa kuwapa mafundisho ya kifedhuli ...narudia tena demu wko ndo yupo kwenye la kisengeli ndo yale ya kitapeli
 
Utafiti wako ni kweli mkuu lakini ukweli huu sio kwa mabinti wa kilokole tu karibia kila dhehebu linaguswa.

1. Kila mkusanyiko wa vijana wa kike na kiume asilimia kubwa uasherati na mahusiano ya kingono huwa hayakosi.

2. Asilimia kubwa ya mabinti wa kitanzania wanatokea kwenye familia masikini na wengi wanakabiliwa na changamoto ya kutokuolewa... (kuna idadi kubwa za mimba za kwanza kuliko ndoa)


3. Kila kwenye mikusanyiko ya dini wakiwepo vijana wa kike na wakiume huwa pia kuna vita ya kiroho dhidi ya uovu na wema. Wanaofanya maovu hawakosi tu na ndio maana unasikia mpaka viongozi wa madhehebu wanalawiti watoto.
Hivyo basi mikesha makanisai huwa ni vita hiyo.

4. Kila mtu huwa ni mbishi kwenye imani yake hata kama atapewa kila vidhibitisho juu ya anachokiamini. Mabinti wa kirokole wana misimamo juu ya yale wanayofundishwa.(Haijarishi kwa imani zingine ni mabaya)

5. Wachungaji wa kilokole wana maamuzi ambayo kikatiba wanaweza kuamua na yakawa ya mwisho kulingana na uongozi wao. Ila suala la kuita mke wa mtu usiku ni uhuni tu kwa baadhi ya wachungaji hawa na si wote. Halafu kumbuka kuna baadhi ya madhehebu viongozi ndio watoa maamuzi ya mwisho hata kama biblia itapingana nao.

6.Ni vizuri kila mtu akaoa mtu wa imani yake na dhehebu lake muendane lasivyo mtazidi kulaumu kila siku.

7. Asilimia kubwa kila mtu anapenda kuoa mcha Mungu. Kila mtu anaamua kwenda kanisani kwa sababu yaje binafsi...JE NI KIPI BORA UENDE KANISANI ILI UPATE MKE AU UENDE BAA UPATE MME.

MWISHO: Si wote waniitao BWANA BWANA watarithi UZIMA wa milele.

NAWAPENDA SANA MABINTI WA KILOKOLE.
Na sisi ni binadamu kama nyie msitusakame jaman
 
Nashangaa mleta mada kuongozwa na hisia kwani mtu kuwa mlokole ndo unakuwa huna hisia au hafanyi mambo mengine ya kibinadamu!
Kwani nini maana ya kuwa mlokole? [emoji56]
 
Hivi inashukua mda gani binti WA kilokole kutoa jibu pale unapokuwa umemtaka muwe wachumba...
 
Awali ya yote naomba kuweka katika kumbukumbu za jukwaa hili kuwa, mosi, uchambuzi huu haujalenga kubeza, kukejeli ama kudhalilisha imani za watu. Pili uchambuzi huu hauwahusu mabinti wote wa kilokole bali na baadhi ya wengi wao na si wote wapo hivi.

Pia nikiri kuwa, madhehebu ya dini zote yakiwemo ya walokole yana misingi na mafundisho mazuri hoja nitakazotoa zimetokana na mimi kuwa na mahusiano na binti wa dhehebu mojawapo kati ya haya madhehebu ya wanaojiita walokole na kupitia kuwa na huyu binti nilipata interaction ya kufahamiana nao wengi kwani ilibidi niingie kwenye makundi yao ya WhatsApp, nihudhurie events zao, nipate mialiko ya binafsi kuwa nawatembelea mmoja mmoja na pia nilipata wasaa wa kujenga nao urafiki wa karibu ambapo kuna vitu ambavyo wanavipenda na wanavifanya kwa siri watu wa nje hamtavijua kwa kuogopa kuchafua makanisa yao ila wao kwa wao wanafnya na wanajuana.

Findings;

1. Asilimia kubwa ya mabinti walioingia kwa utashi wao huku familia zao zipo madhehebu mengine ni wahanga wa matatizo kama kutokuolewa, ugumu wa maisha na u-single mother

2. Kwaya na mikesha ni kichaka cha maovu kwani mle kwenye kwaya kuna couple kila mtu na wake ila kama wewe mpenzi wako yupo huko na wewe husali huko hutajua.

3. Wana umoja katika kutunziana siri sana.

4. Wengi wao wanawinda kuolewa kwani katika jamii imezoeleka kuwa mabinti wacha Mungu wanafaa kwa kuoa. Wengi hujivisha ulokole ili wapate kuolewa. Ndio maana kule kuna ndoa nyingi sana; haupiti mwezi bila ndoa.

5. Wana uasili wa ubishi na kulazimisha anachotaka yeye ndo kiwe ukimpinga mtaishia kugombana au kuachana.

6. Kauli ya mchungaji ni sheria hata akipigiwa simu usiku na mchungaji ataenda na ukimzuia mmeachana.

7. Kutokana na mfumo wao wa kuabudu sauti zao ni kavu na wanaongea kama cherehani mkiwa mnajadili kitu anaongea kama anakukemea.

8. Wengi wao hawadumu katika mahusiano hasa pale anapokuwa na mtu ambaye sio mlokole.

9. Si wasikivu na wenye heshima na mara zote hujiona wako sahihi katika kila wanachokiwaza.

10. Waalimu wa kwaya hutafuna sana wanakwaya kipindi wakiwa wageni.

11. Wana mafundisho yao ambayo wanakaa na mama mchungaji. Huko kuna sumu nilizisikia kutoka kwa binti mmoja alipoamua kuniibia hizo siri. Kwakweli yana ukakasi kuyataja hapa.

Mwisho kabisa napenda tu kuweka sawa hili suala. Dini zote zina misingi na mafundisho mazuri inapotokea waamini wake wanaitumia misingi hiyo vibaya wanatengeneza vitabia ambavyo lazima jamii itavi-associate na dini/dhehebu husika.
Nao ni binadamu tu kama binadamu wengine, ambao biblia inasema katika kitabu cha warumi 3:23
kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
Pia Biblia inasema tusihukumu
Tuwaombee na tujiombee
 
Kuna pisi moja ya kilokole imeachika nikaamua kupita nayo jinsi inavyonicganyia rangi ,,,, nimegundua kwa nini mwamba alisalenda.......
 
Back
Top Bottom