Habari wana jamii form
kwa muda mrefu kumekuwa na battle kati ya A-city Vs Rock City. Nimefuatilia kwa makini nimeona pande zote hakuna anayekubali kushindwa.
Lakini kwa mtazamo wangu wa kawaida ukweli ndio huu
01. Population arusha city iko half of Mwanza rock city
02. Kujengwa kwa city Chuga iko 90% wakati rock city iko 50% wakati dar city 100% na a-city 75%
03. Kwa ujanja a-city 80%, dar city 99% na rock-city 40%.
03. Kwa mzunguko wa hela Dar-city 90%, A-city 70% na rock city 60%
04. kwa hali ya hewa A-city 100%, Dar-city 40% Na Rock City 50%
NOTE; i was born in a city but, i am living in monrovia
Unajua ni jiji gani la pili kwa kuchangia pato la Taifa ?
Ukijibu hilo swali nd'o utapata majibu wapi kuna fursa nyingi za kiuchumi na kijamii . Itakusaidia kutokuandika kwa mihemko . Kwa kukusaidia ni kwamba mji wa Arusha ni mji wa shughuli za kitalii zaidi kuliko mji mwingine wowote Tanzania labda wanachuana na visiwa vya Zanzibar . Hivyo uchumi wa Arusha chanzo chake kikubwa cha mapato ni utalii . Pia wana Tanzanite , mifugo na Kilimo kiasi . Arusha haina uwanja mpana sana wa shughuli nyingi za kiuchumi ukilinganisha na Mwanza .
Mwanza Uchumi wake unatokana na vyanzo vifuatavyo :
1 . Ziwa Victoria - Ajira ni nyingi mno zilizo rasmi na zisizo rasmi ukilinganisha na Utalii wa Arusha
2 . Madini ( hasa dhahabu ) - Ajira rasmi na zisizo rasmi ni nyingi ukilinganisha na zile zinazotokana na Tanzanite
3 . Kilimo asilia : Pamba , Mahindi na Mpunga . Arusha ina mashamba makubwa ya kisasa ya Kahawa na Maua ingawa hayaajili watu wengi ukilinganisha na Mwanza
4 . Ufugaji - kwa sehemu kubwa Arusha inaweza kuwa na mifugo mingi ingawa hiizidi sana Mwanza .
Kwa kifupi Mwanza ni sehemu ya uhakika kuwekeza kutokana na population kuwa kubwa kuliko Arusha na hivyo Mza ni soko kubwa.
Arusha wamepakana tu na Kenya upande wa Kajiado na Nairobi lakini Mwanza imepakana na Kenya kwa sehemu kubwa zaidi . Pia Mwanza imepakana na nchi za Rwanda , Burundi , Uganda na hata Congo .
Mza ni jiji lililo katikati ya nchi za Great Lakes na hivyo kuwa na mwingiliano mkuu unaowafanya watu wengi wa kawaida kuwa na kipato kizuri ukilinganisha na Arusha yenye pengo kubwa mno kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho.
Nawasilisha kwa leo.