Ukweli kuhusu alama ya mnyama

Kwanini usianze kwa kujibu maswali kuhusu hiyo sura inayomuhusu MNYAMA ,kuliko kutaka kuokoteza vimistari? Ndio maana najua huwez kujibu hayo maswali kamwe,maana umeanza sarakasi,
Au maswali hujayaona?

Niambie UISLAMU UNAHUSIKAJE hapo?
 
Mkuu aya 5 tu unaleta sarakas , hii inaonesha ni kwavip mbaokoteza aya na kudanganya , je ningekushushia zote ?

Huu unabii 100% unalihusu kanisa la roma, ndio maana waliamua kuwaua watakatifu, ili kuficha ukweli huu, walizui pia biblia zisichapishwe na kutafsiriwa , na WILLIAM TYNDALE ALIPOAMUA kutafsir biblia , walimchoma moto

NAKUNGOJA NJOO TUHOJIHANE, ukileta mstar umeokota huku na kule , ukahitimisha et ni UISLAMU, utachekesha , maana mwingine ataibuka atasema ni urusi ,
 
Mkuu habari!
Nimekusoma kwa uzuri na nimekupata vilivyo. Ila naomba unisaidie kupata muunganiko wa amri ya sabato na mhuri wa Mungu.

Nijuavyo amri zipo 10 lakini umechomoa ya katikati na kuifanya iwe mhuri wa Mungu. Ni vigezo gani umetumia hapa mpendwa? Na kwa nini mhuri usiwe amri zote? Pia kama ulivyonukuu Ebr 10 kwamba Mungu atatia amri zake na kuziandika na wala si amri moja. Hapa huoni kama unatuchanganya kama siyo kutudanganya?

Pili kuhusu visawe naomba ujipange upya. Maana ya neno hutegemeana na muktadha. Na ndo maana hata kwenye kamusi utakuta maana zaidi ya moja ambapo wewe utachagua ile inayoendana na mktadha (mazingira) yako ya mazungumzo. Mtu wa Mungu AROON, ni vizuri ukawa makini na kila unachokisema ili usijeonekana unadanganya kama ulivyofanya kwenye hili hapa.

Tatu umetumia aya hii kuthibitisha usemacho!

“Jumapili ni ALAMA yetu ya mamlaka…kanisa liko juu ya Biblia, na uhamishaji huu wa utunzaji wa Sabato ni ushahidi wa jambo hilo la ukweli.” -–Catholic Record of London, Ontario Sept 1, 1923.

Ombi, naomba unisaidie mimi na wengine kwa kubandika huo ukurasa husika ili tuendelee kujifunza mpendwa.

Ezekiel 20:12,20 umenukuu kuwa Mungu aliwapa sabato zake kuwa ishara. Swali la msaada, kuna sabato ngapi? Kama ni zaidi ya moja je ipi ndiyo mhuri wa Mungu?

Maana ya kutakasa ni nini?
Je watu wana uwezo wa kutakasa kitu au ni Mungu peke yake?
Si Sabato ni takatifu! Kwa nini watu wanaambiwa kuzitakasa?

Asante kwa andiko zuri, nitakuja tena.
 

Okay. Amini ulichoamua kukiamini. Nilidhani ninawasiliana na mtu ambae yupo tayari kujifunza kitu kipya however strange it seems to them.
 
Kwakweli mleta mada pole sana naona bado hujakutana na Bwana Yesu.
Nakushauri mimi niliye mdogo ukubali Bwana Yesu akuokoe nawe upate kuhesabiwa haki kwa sheria ya imani uachane na sheria ya dhambi iletayo mauti ndani yako.
 
Okay. Amini ulichoamua kukiamini. Nilidhani ninawasiliana na mtu ambae yupo tayari kujifunza kitu kipya however strange it seems to them.
Nilijua lazima ukimbie tu, NAUHAKIKA USINGEWEZA KUTHUBUTU HATA MSTARI MMOJA TU KUUELEZEA

ningeshangaa sana kama ungejibu walau mstari mmoja ,

Ona unakimbia ,
 
Kwakweli mleta mada pole sana naona bado hujakutana na Bwana Yesu.
Nakushauri mimi niliye mdogo ukubali Bwana Yesu akuokoe nawe upate kuhesabiwa haki kwa sheria ya imani uachane na sheria ya dhambi iletayo mauti ndani yako.
Hayo maneno hata manabii waliojaa hapa tz wanasema hivo

Njoo hapa nipinge mada yangu kwa hoja , wapi nimekosea , na kipi ni sahihi,

Sio kukariri maneno na kutoa lawama ,haisadii
 
Mbona nimeeleza muhuri unatakiwa uweje ,soma vizuri maana nimeshalieleza kwenye uzi

Umesema Mungu atatia sheria yake moyoni,

Kwanza inaonesha hujasoma uzi ukauelewa, umeusoma haraka haraka,

Sijautumia huo mstari kuonesha ni sabato tu, nimeutumia huo mstari kuonesha MUHURI UNAPOWEKWA KWENYE AKILI/MOYON MUNGU ALIMAANISHA NINI, soma tena ,

Umezungumzia SABATO KUWA ZIPO NGAPI, sabato mpaka sasa IMEBAKI MOJA TU, AMBAYO IPO KWENYE AMRI KUMI,

Kipindi cha wana israeli sabato zilikuwepo nyingi , hizo sabato ziliishia msalabani, ndio zile ambazo zimesemwa wakolosai 2:16

Sabbaths days

Umesema nimenukuu kutoka chanzo cha kikatoliki, ndio nimenukuu kuthibitisha ALAMA.YA MNYAMA NI IBADA YA JUMAPILI,

Ukitaka ushahidi , ingia google angalia record ya hiyo makala utaikuta hiyo QUOTATION, tena utazipata nyingi,

SABATO NI TAKATIFU NA MUNGU AMESHAITAKASA ,

ILA UNAPOIVUNJA AU KUFANYA UJUAYO WEWE, UNAKUWA UMEINAJISI ,

NDIO MAANA MUNGU ANATUASA TUITAKASE

kupitia nabii isaya alisema tena

Isaya 58:13

If you keep your feet from breaking the Sabbath and from doing as you please on my holy day, if you call the Sabbath a delight and the LORD's holy day honorable, and if you honor it by not going your own way and not doing as you please or speaking idle words,

HAYA WEWE MUNGU ALIKUUMBA MTAKATIFU, ILA UNAPOFANYA DHAMBI UNAKUWA NAJISI

SIMPLE LIKE THAT..
 
Okay. Amini ulichoamua kukiamini. Nilidhani ninawasiliana na mtu ambae yupo tayari kujifunza kitu kipya however strange it seems to them.
Najua umefukua ukafukua ,ukakuta hauna ushahidi,

Umeona uage , kienyeji ,

Kiukweli Natangaza ANAYEBISHA KUWA MNYAMA SIO UKATOLIKI NA ALAMA YA MNAYAMA SIO IBADA YA JUMAPILI

AJITOKEZE HAPA ASEME MNYAMA NI NANI NA ALAMA YA MNYAMA NI NANI,

TUHOJIHANE HOJA KWA HOJA , MISTARI KWA MISTARI, HISTORIA KWA HISTORIA

NIMETANGAZA UWANJA NI WAZI
 

Tatizo lako ni kuwa upo prejudiced. Ulicholishwa na kunyweshwa kimekukolea hasa hadi ukiona rangi nyekundu ulipoambiwa utaona rangi nyeupe bado unaamini kuwa umeona rangi nyeupe kwa kuwa kina Ellen White walikuambia hivyo.

Look here; kumbuka Nabii Daniel na Mtume Yohana walionyeshwa mambo yanayotokea leo wakati wanaishi kipindi ambacho tunayoyaona leo kwao wasingeweza hata kufikiria uwepo wa hayo mambo. Kwamba ni kipi walionyeshwa ndipo akili yetu mimi na wewe tunaeishi leo hii tunapaswa kujua maana maarifa yanazidi kuongezeka (kama alivyoambiwa Daniel) na uwezo wetu wa kutafsiri unazidi kuongezeka (kwa kuwa siri zilizofichika zinafunuliwa taratibu but at an increasing rate). Nakupa mfano hapa wa kile ninachokuambia hapa.

Ukisoma Daniel 9:26 kuna utabiri juu ya kuharibiwa mji wa Jerusalem na hekalu la Mungu na "jeshi la (watu wa) mfalme (mtawala) ajae". Jerusalem ilitekwa mwaka 70 AD na Jenerali Titus wa jeshi la utawala wa Kirumi. Msingi wa dhana inayoshikiliwa na Wasabato (na baada ya watu) hadi leo hii kuwa mpinga Kristo atatokea kanisa la Romani Katoliki linatokana na tukio hilo. Lakini Daniel aliandika specifically kuwa watakaouteka mji wa Jerusalem na kuharibu hekalu ni WATU WA MTAWALA AJAE (sio mtawala aliekuwepo wakati huo au watu wa mtawala aliekuwapo wakati huo - meaning watakaouteka mji wa Jerusalem na kuharibu hekalu ni WATU WA MTAWALA AJAE). Ni kweli mji wa Jerusalem ulitekwa na Jenerali Titus wa jeshi la utawala wa Kirumi LAKINI JENERALI TITUS alikuwa anaongoza jeshi ambalo wanajeshi wake wengi WALIKUWA NI WAARABU NA WATURUKI na sio Warumi wazawa. Soma hapa

Who Are "The People of the Prince to Come"?

Mtawala ajae ambae hao wanajeshi Waarabu na Waturuki ni watu wake ni Kanisa Katoliki?

Cc
Masoud Mshahara
 



KWANZA UNAELEWA HUYO MNYAMA ANAYEZUNGUMZWA HAPO NI NANI?

JE SANAMU YA MNYAMA NI NANI?[/QUOTE]
wewe dogo nipo hapa Tunduma na hao wachungaji wako wa makambi wanaokudanganya tatizo unaaamini Unavyovipostihatuyakuviona
 
Dogo hayo makambi ujinga
 
MBONA NIMEKUULIZA MASWALI HUTAKI KUJIBU UMEBAKI UNALALAMIKA.TU,

ZAIDI UMEJITUNGIA SWALI LAKO MWENYEWE

HAYO MASWALI YANGU YAMEKUSHINDA NINI, AU HUYAONI?
 
Mkuu mbona haumjibu maswali yake ,zaidi.unayakwepa ? Tatizo nini, nimeona umeaga kukimbia ,sasa hivi umerudi na ngonjera nyingine, watu tumekaa tunasubiri kujifunza, utusaidie hizo Aya zinahusiana vipi na uislamu, cha kushangaza ni.kama huzioni, hizo aya unazokimbilia , hata hazihusiani na uislamu, ndio maana kwakuwa umedai, mnyama ni uislamu, umepewa sura ya yohana 13 , kuhusu mnyama ,ujibu ,umeshindwa hata kujibu mstari mmoja tu? Hebu jitahidi bhana ,wewe ndio utaonekana muongo
 
I give up!
Umegoma kumjibu, au maswali yake unaogopa yatakukaanga? Mimi na bet ukijibu Natoa Laki 1 . Naimani huna uwezo hata robo wa kujibu hayo maswali ,hata kujaribu huna huo uwezo, ,maana utakamatwa tu,na ndio unachoogopa ,mmebaki kushambulia tu usabato ,mara ellen white , sijui mkojo nyie watu, watu tunataka kujifunza mnaleta ujinga
 

Kuonekana muongo sio tatizo kwangu hasa baada ya kugundua aina na uwezekano wa mtu niliekubaliana nae kujadili nae (kwa lengo la kuelimishana). Kuna shida gani kwake (au kwako) kusoma nilichoshauri akisome kwanza ili nimjibu maswali yake - essentially he could have asked in a single question as almost everything is related and entwined to each other?
Nimempa link asome - na hajasoma (au kama kasoma basi hakuelewa kitu) maana vinginevyo asingeshindwa kuona kuwa baadhi ya maswali yake yanajibiwa na maelezo yangu na yaliyomo kwenye scholarly article kwenye link niliyompa. Na kama kitu kidogo hivyo kimekuwa kikubwa kwake ataelewa kweli Christian eschatology na Islamic eschatology? Bila mtu kusoma hayo japo kidogo KAMWE hataelewa kwa majira haya - japo baadae kila mtu ataelewa tu maana ni lazima mpinga Kristo afunuliwe eventually.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…