UKUTA wakosa waandamanaji

UKUTA wakosa waandamanaji

MBONA POLISI WAMESHA ANDAMANA NCHI NZIMA KUTANGAZA UDIKTETA WA MAGUFULI NA RAIA WAMEMCHUKIA SANA KWA KITENDO HCHO NDIO MAANA ASILIMIA 99.9 RAIA WENGI WALIFURAHIA KUUAWA KWA POLISICCM
mkuu alishasema wananchi wawaogope polis
 
Usipoziba Ufa utajenga Ukuta...inaonesha wapinzani walichelewa kuziba Ufa nw wanataka kujenga Ukuta.

Hakuna kitu kizuri kama kufika muafaka wa jambo llte lile kwa njia ya mazungumzo.
Sisi kama Watanzania tunajulikana kwa upole,upendo,ukarimu,uvumilivu na umoja wetu ni vitu vya kujivunia sana
Isifike mahali kundi la watu wachache watake kuharibu Tunu zetu tulizoachiwa karne na karne,hakuna anayependa kusikia milio ya mabomu,risasi wala kuona vifaru vikirandaranda mitaani

Ni jukumu langu mm na wewe kuilinda Amani ya nchi yetu kwa hali yyte ile.

Wapinzani bado wana muda wajipange kwa sera nzuri 2020 ila sio kwa mipango mingne yyte ile itakayokuwa kinyume na sheria na taratibu za nchi.

Mfano pale Misri ilianza kama utani tuu lakini yaliyokuja kutokea kila mtu anajua,ukiwanacho hutaona thamani yake ngoja kipotee sasa.

Nawasilisha.
 
Nchi inaongozwa na ushabiki
Kuanzia Rais mwenyewe anaongea kishabiki tu. Amekosa busara na hekima kabisa huyu Rais. Hata hajui ni wakati gani aongee nini yeye lolote linalokuja kinywani mwake ni kuachia tu.
 
Unajua unacho wakilisha? Nani kakwambia ni watu wachache? Amani soup kukaa kimya.
 
Hakuna atakayeandamana siku hiyo. Watu wapo busy na kazi zao.
 
Haya ahsante, nenda sasa ukafanye kazi! Rais alisema hakuna maandamano ili watu waachwe wafanye kazi ila nikashangaa kuwaoneni ninyi uvccm mnasahau agizo la rais la kufanya kazi eti nanyi mfanye maandamano ya kumpongeza rais, mmesikia wapi kazi zimeisha kwa mafanikio mpaka muandamane kupongeza? Waambie na wenzio wakafanye kazi, ahsante!
tulia ccm tunajitambua
 
Hata huku kwetu wanainchi wamewapuuza ukuta kwani wamesharidhishwa na kazi ya magufulii haaa haaa itakuwa ni aibu ya mwaka kwa wanachademaa ukuta
 
Sisi huku kwetu watu hawajui hata maana ya UKUTA.
 
Jiulize kwa nini jpm hataki kuwasikiliza wapinzani ili ukuta usitishwe
 
Ndugu wana bodi,
Tukiwa timebakiwa na siku chache kuifikia siku ya Septemba mosi ambayo chama cha CHADEMA kimetangaza kuwa siku ya mikutano na maandamano nchi nzima, hali iko tofauti katika mji wa songea mkoani Ruvuma. Hakuna maandalizi yoyote yale yanayofanyika katika mji huo kama kuunga mkono tamko la viongozi wao.

Katika kupita kwangu katika mitaa mbali mbali nimeweza kukutana na wananchi wa kawaida na hata wale wanachama wa Ukawa hususani CHADEMA. Wengi wao wanahofia familia zao hasa wakiona polisi wanafanya mazoezi hadharani kama kujiandaa kukabiliana na maandamano hayo.

Uelewa pia wa masuala ya kitaifa kwa wananchi wengi wa mji huo ni mdogo sana. Kwa mfano ukimuuliza mwananchi wa kawaida anayeuza nyanya Soko kuu pale mjini kuhusu utawala wa Rais mpya anakuambia anatenda vyema tu. Hakuna sheria aliyokiuka. Nawashangaa tu hawa kina Mbowe wanaosema tuandamane wakati mafisadi saizi wanashughulikiwa.

Hayo ni maneno ya wananchi wengi tu mjini. Polisi kwa upande wa Mkoa huu wa Ruvuma wala hawana wasiwasi juu ya tukio hilo kwani hawataona mtu kuandamana. Huenda maandamano hayo yakafanyika kwenye baadhi ya mikoa tu. Huku ni ccm tu. CHADEMA mkoa bado wana hasira na ugawaji mbovu wa viti maalum katika uchaguzi wa mwaka jana octoba 2015.

Hayo ndiyo niliyoweza kuyaona. Viongozi wa CHADEMA wana kazi nzito kwenye mkoa huu.

Mimi napita.
 
Back
Top Bottom