Naum Wana JF
Kwanza ninapongeza hatua za Rais JPM(PhD) za kuleta mabadiliko ya kweli kiuchumi,kijamii na kiutendaji serikalini ambayo kwa kiwango kikubwa wananch wanafurahia na kushiriki keki ya taifa. Tunakusihi kamwe usigeuke jiwe!...Tunashuhudia jinsi ujenzi wa miundombinu kadhaa ikiendelea kubadili taswira ya nchi yetu na zaidi umedhihirisha wewe ni raisi wa watu wote. Umekuwa nembo ya umoja,amani,uhuru na demokrasia ambapo tumeshuhudia baadhi ya wanasiasa wakikukebehi pasipo na kudhurika kama ilivyo kwa nchi za kifashisti. Tumeshuhudia jinsi Mahakama na Bunge vikifanya kazi zake kwa uhuru na weledi...na zaidi uanzishwaji wa Mahakama ya mafisadi na uamuzi wa utekelezwaji wa serikali kuhamia Dodoma.
Kwa upande mwingine wa shilingi...wajenzi wa ukuta wamegeuka kama walivyokuwa wajenzi wa mnara wa babeli....hawaelewani,wamesambaratika na kutapatapa!
-Kinara wa ukuta katokomea,hajulikani alipo kwa sasa...amekasimu madaraka kwa kiaongozi mdogo ambaye kimsingo siye msemaji wa ukuta. Hadi sasa hatuna uhakika kama yupo nchini au ughaibuni japo kuna habari kuwa yupo ng'ambo!
-Tunashangaa sasa waliotaka kushiriki ukuta wanamtumia Kingunge kutenegezeza mazingira ya mazungumzo. Badala ya Kingunge kuwaambia waache upuuzi wa ukuta yeye anakimbilia kulia lia kwa Maraisi wastaafu wamshauri Raisi azungumze na watu ambao wameapa wataandamana kumkomesha Raisi sababu ni 'dikteta'
- Zaidi tumeshangazwa na wabunge wa ukuta wamejaa Dododoma na wamethibitika kula posho kuanzia tar.22 Ogasti...na taarifa za kuaminika ni kuwa hawakosi kamati, wanahudhuria bila kukosa ili kupata fedha kuziba mashimo yaliyotokana na kumkimbia Naibu spika...!
-Imethbitika pasipo shaka ukuta hauna Baraka za wananchi...! hili halihitaji ubishi zaidi wananchi wanafikiri ukuta ni chama kipya cha siasa!
-Kibaya zaidi wasadikika wa ukuta hawajui linaloendelea