Ukurasa wa Hayati Magufuli umefungwa kama zilivyofungwa za wengine

Case closed!

Kuna watu wasiojielewa wamejitokeza na kutaka ionekane Mheshimiwa Marehemu Raisi Magufuli yupo hai,tuseme tu Mheshimiwa Magufuli amefariki na kuzikwa Rasmi, kwao Chato ni rais wa tatu kuzikwa wakwanza akiwa Karume, wa pili Nyerere na Magufuli anaifanya idadi iwe ya watatu.
Watatu kiaje sasa?

Mbona mnaanzisha nyuzi kwà papala?
 
Siyo kwamba hatuamini kwamba Magufuli (Rip) ameshafariki, tunalijua hili na tunaamini hivyo. Tunachofanya hapa ni kupambana na wafuasi ya yule mshikishwa ukuta, (aka dish limeyumba, au chizi, kamanda msaliti/mtundulisu).

ambao pamoja na yeye mwenyewe wamekuwa wakifanya juhudi kuwa sana za makusudi kumtukana, kulichafua jina lake na ku-paint picha isiyoendana na uhalisia wake. Hao tutakula nao sahani moja mpaka kieleweke.

Pili, wewe ni nani mpaka uwapangie watu cha kusema? Watu wana uhuru wa kujinafasi bhana, acha hizo.
 
Kuna watu wasiojielewa wamejitokeza na kutaka ionekane Mheshimiwa Marehemu Rais Magufuli yupo hai, tuseme tu Mheshimiwa Magufuli amefariki na kuzikwa Rasmi, kwao Chato ni rais wa tatu kuzikwa wakwanza akiwa Karume, wapili Nyerere na Magufuli anaifanya idadi iwe ya watatu...
Kwa orodha yako ya marais waliokwisha fariki ukianza na Karume, basi umewasahau akina Idris Abdul Wakil na Aboud Jumbe, ingawa Mkapa ambaye ni wa juzi tu kutangulia hukumweka kwenye hiyo list.
 
Wawe watatu wanne au sita ,cha kuzingatiwa ndio wameshatoweka na tukubali yao yamesita,jamhuri ipo na inaendelea,kuna ulazimishaji eti ni lazima mikakati na misimamo yake ifuatwe ,mnaobakia hapo hamna tofauti na wale askari wanaopiga marktime,Sasa yupo Raisi mupya na kile anachokisema yeye ndio hicho kinachotakiwa kusikilizwa. Magu is gone.

Na kiuhalisia Magufuli alishindwa kuwa mweledi katika baadhi ya mambo hasa kwenye kusimamia haki au amani pale panapotokea tukio kuu katika nchi ,kama mabarabara na madaraja mbona yalijengwa tokea na kabla ya Uhuru ? Kwa hayo alichokifanya ni kule kunakoitwa kuboresha.

Mepya ambayo yalitingisha Taifa na kupotea kwa watu maarufu,kupigwa risasi,kuokotwa watu baharini ndani ya vipolo,raia kupigwa viboko hadharani ,sikuwahi kumsikia Magu akilikemea au hata angalau kulitaja na kumtaka mhusika japo ababaishe,kwa sababu za kiccm,hamna.

Tuseme ukweli na sio kutetea mambo maovu au kwa vile halikukuta wewe mwana kuliafuta? Sio mlazimishe tuendelee na tabia zake ndio nikasema ,yeye ameshafariki na nyie mnaotaka tuendelee na mambo yake ndio msiomtakia kheri mnafukua na kusababisha makaburi yachunguzwe upya.

umemzika Magufuli na tuzike na mambo yake mnapoambiwa kazi iendelee,basi jiongezeni kwa akili zenu.magu sasa yupo kaburini peke yake nyinyi mliobakia ambao pengine mkinufaika kwa kukingiwa kifua na yeye na kujiona au mlijiona kama ndio maraisi sasa mpo peke yenu, kama ulikuwa ni mtenda maovu na kuruka hukumu, ile ngao yako ujue sasa haipo, kuendelea kumshobokea Magu ni kama vile huelewi au hukubali jamaa hatunae na unataka kuendeleza siasa zake. Utaishia jela achana nae na kuwa mtii na mfuata sheria kwa waliokuwepo.
 
Kuna watu wasiojielewa wamejitokeza na kutaka ionekane Mheshimiwa Marehemu Rais Magufuli yupo hai, tuseme tu Mheshimiwa Magufuli amefariki na kuzikwa Rasmi, kwao Chato ni rais wa tatu kuzikwa wakwanza akiwa Karume, wapili Nyerere na Magufuli anaifanya idadi iwe ya watatu...
Karume yupi au Mkapa?
 
mbona unasisitiza nawewe umewaamini hao watu,ambao hata hawajulikani ni akina nani na ni wapi waliyasema hayo!...
Dr. Ali Juma alikuwa makamu wa Rais 1995-2001 akafariki 4 July 2001 nafasi yake ilichukuliwa na Dr Sheni, weka kumbukumbu vizuri.
 
IMG-20210608-WA0049.jpg
 
Kuna watu wasiojielewa wamejitokeza na kutaka ionekane Mheshimiwa Marehemu Rais Magufuli yupo hai, tuseme tu Mheshimiwa Magufuli amefariki na kuzikwa Rasmi, kwao Chato ni rais wa tatu kuzikwa wakwanza akiwa Karume, wapili Nyerere na Magufuli anaifanya idadi iwe ya watatu.

Tusiwe wajinga kama watu tulikosa muelekea japo chini ya CCM ndivyo wanavyotaka tuone hivyo,imekuwa mtu akifanya hivi au vile anaogopa au anavunja ,anapinga maneno maneno mengi ya kuvunjana moyo na mtu aonekane anenda kinyume na Magufuli.

Kama mtu akifanya kazi kwa kumuogopa Magufuli, Rais Magufuli ameishafariki na hatorudi tena na kama mtu akifanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi basi sheria zipo na zinafanya kazi yake kwa mujibu wa mazingira ya kutumiwa sheria hizo.

Ndio mara nyingi tunasikia kazi iendelee, kama ulikuwa unamtegemea Magufuli kwa mabaya au mazuri yako, unatakiwa ujue kuwa Magu ameishafariki kitambo. Ulikuwa mwizi ulikuwa kiongzi bora, waliopo hawatafanana na yeye na kuendelea kukulinda kama ilikuwa hivyo na inaoenakana wengi wameanza kupata tabu baada ya kufariki Magufuli, kama walitegemea kuwakingia kifua au kuwavunja kifua sasa hofu zimetawala na faraja imekuwepo.

Tusiwe kama tuliogandishwa kila kitu Magu,siku mtu anapokufa kama hamuelewi ndio na yeye mambo yake yote husimama isipokuwa yatakayompa faida ni yale mema na hayo hayahusiani na sisi tuliokuwepo hai.
Mkuu shida gani? Kwanini unahangaika na kivuli cha waliolala?
MAGUFULI AMELALA Na wewe laza akili yako kuhusu yeye, Kama umesahahu Mkapa naye kama Rais wa Awamu ya 3 Ya uchaguzi naye alilala.
Funga huo ukurasa akilini mwako achana na watu wengine.
 
Back
Top Bottom