Ukuaji wa lugha ya Kiswahili: Neno Mbashara

Jamani. Naomba kuuliza, neno MUBASHARA linalotumiwa na kituo cha luninga cha ITV ni la Kiswahili sanifu?[/
Muundo wa Lugha nyingi duniani hutegemea lugha nyingine. Lugha ya kiswahili kwa kiasi kikubwa imetokana na maneno ya kiarabu mfano

Kiswahili-Kiarabu
Shukurani-Shukran
Dhahiri-Dhaahir
Iliyo wazi, inayoonekana kwa dhahiri-Mubaashara

So to conclude, mubaashara ni neno la kiswahili
 
Nashukuru kwa kunielemisha. Lakini tukubali ukweli mmoja kuwa maneno ya lugha nyingine huingia na juanza kutumika kwenye lugha nyingine kurokana na mazoea. Sio kwa kulazisha neno la lugha nyingine ambalo halitumiki popote na kulifanya neno rasmi.
Kutokana na ujio wa luninga, na kuanzishwa kwa matangazo ya moja kwa moja kwenye luninga na kwa sisi uelekeo wetu na mazoea ni kiingereza na neno la kiingereza linalotumika na tunaloliona ni LIVE, na kwa kuwa neno hili lina tafsiri rasmi ya kiswahili, HAI. Basi ingekuwa rahisi tu kugeuza neno LIVE na kuwa HAI. Kwa mfano ni rahisi kusema "tunawaletea matangazo hai ya mpira kutoka uwanja wa Kirumba..." kuliko kusema ".....matangazo mubashara..."
Kunyumbulisha tafsiri kutoka maneno ya lugha nyingine ambayo hayakuzoeleka kwa kiswahili ni kukifanya kiswahili kuwa kigumu zaidi.
Kutokana na hili ndio maana sio vituo vingi vinatumia neno hili.
 
Ili kukuza Lugha yetu Si lazima tuige lugha za wao tuliowaiga kwa miaka mingi.
Tuzingatie cost ya coding ya hilo neno kwenye aina zote za kumbukumbu (ukiangalia livochukua nafasi kubwa ya screen hupendezwi nalo).
 
Kwanini wasiseme LAIVU au wanapenda kula winga boda la pili kwa waarabu kuiba neno lao ili walilengeshe kwenye tafsiri halafu waseme wameunda neno ...wangesema LAIVU kwa kingereza LIVE
 
Nineno lililo anza kutumika rasmi na idala ya lugha ya kiswahili ya chuo kikuu Cha Udsm na ITV kwa Mara ya kwanza walisikia siku ya uzinduzi Wa maktaba ya kisasa chuon DSM iliyo zinduliwa na Mh Rais JPM
 
Nashukuru kwa kunielemisha. Lakini tukubali ukweli mmoja kuwa maneno ya lugha nyingine huingia na juanza kutumika kwenye lugha nyingine kurokana na mazoea. Sio kwa kulazisha neno la lugha nyingine ambalo halitumiki popote na kulifanya neno rasmi.
Kutokana na ujio wa luninga, na kuanzishwa kwa matangazo ya moja kwa moja kwenye luninga na kwa sisi uelekeo wetu na mazoea ni kiingereza na neno la kiingereza linalotumika na tunaloliona ni LIVE, na kwa kuwa neno hili lina tafsiri rasmi ya kiswahili, HAI. Basi ingekuwa rahisi tu kugeuza neno LIVE na kuwa HAI. Kwa mfano ni rahisi kusema "tunawaletea matangazo hai ya mpira kutoka uwanja wa Kirumba..." kuliko kusema ".....matangazo mubashara..."
Kunyumbulisha tafsiri kutoka maneno ya lugha nyingine ambayo hayakuzoeleka kwa kiswahili ni kukifanya kiswahili kuwa kigumu zaidi.
Kutokana na hili ndio maana sio vituo vingi vinatumia neno hili.

Mkuu maelezo yako ni Kama hukubali ukweli kuwa lugha ya
Kiswahili imekopa maneno toka lugha ya kiarabu. Yafutayo ni maneno yaliyotokana na lugha ya kiarabu:
-Habari-habar; asubuhi-subhi; alasiri-l asri n.k
 
Sijakataa kukopa lakini kopa neno ambalo ni rahisi kutumika au lililokuwepo. Halafu utaratibu wa kukopa kutoka lugha nyingine huwa hauji kwa kulazimishia. Kulingana na historia yetu, maneno mengi ya kwanza yalikopwa kutoka lugha ya kiarabu kwa kuwa ndio lugha iliyokuwa inatumika, lakini baadaye utaona wareno walipokuja tukakopa, wajerumani tukakopa na waingereza na kiingereza chao tumeendelea kukopa. Hapa suala lilikuwa la kungalia neno gani ambalo limezoeleka kwenye jamii kuliko kuanzisha neno jipya kisa limekopwa. Bado nafikiri kuwa neno hai lingekuwa bora zaidi kuliko mubashara
 
Nimekupata vilivyo Mkuu, all in all ndivyo lugha zinavyokuwa.........SHATI-SHIRT; RULA-RULER; MENEJIMENTI-MANAGEMENT....hahaha
 
Wandungu naomba kujuzwa neno Mubashara lina maana gani hasa maana limekua gumzo sasa na je ni kiswahili sanifu kwenye kamusi lipo? Mimi binafsi neno hili nimelisikia mwaka jana kwenyesherehe za Uhuru 9 desemba ambapo lilitumiwa na kituo cha ITV wakitangaza matangazo ya live kutoka uwanja wa uhuru. So mwenye kuelewa atujuze na kama kuna maneno mengine mapya ya kiswahili weka hapa ili tuyafahamu tutoke ushamba wa lugha yetu....
 
Back
Top Bottom