Kudanganywa Ajira Mwanza: Natures Way

Kudanganywa Ajira Mwanza: Natures Way

Nehemia Raphael

New Member
Joined
May 11, 2026
Posts
3
Reaction score
9
Mimi mkazi wa Tabora. Naomba kuwasilisha taarifa kuhusu mfumo unaotumia ahadi za ajira kuwavutia vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenda Mwanza kwa maelezo ambayo hayatoi ukweli kamili wa shughuli zinazofanyika.

Mimi binafsi nilielekezwa kuwa kuna nafasi za kazi ya kusambaza dawa katika hospitali mbalimbali nchini. Kutokana na maelezo hayo, nilisafiri kutoka Tabora kwenda Mwanza kwa matumaini ya kupata ajira ya kawaida.

Baada ya kufika Mwanza, nilitakiwa kufanya malipo mbalimbali yaliyoelezwa kuwa ni sehemu ya mchakato wa ajira. Malipo hayo yalihusisha:

• Kodi ya makazi ya miezi mitatu
• Ada ya semina
• Ada ya usajili/form
• Gharama za chakula

Jumla ya fedha nilizolipa ni Tsh 167,000.

Shughuli hizi nimezikuta zikifanyika katika kampuni linalojiita Natures Way (Empowered Consumerism), lililopo maeneo ya Mlango Mmoja, Mwanza.

Baada ya kuanza kushiriki kwenye shughuli hizo, niligundua kuwa hakukuwa na ajira ya kawaida kama nilivyoelekezwa kabla ya kuondoka Tabora. Badala yake, shughuli inayofanyika ni mfumo wa Network Marketing, tofauti kabisa na maelezo ya awali niliyopewa kuhusu ajira.

Kutokana na hali hiyo, nimeona nimepotezewa muda pamoja na fedha zangu kwa kupewa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusu kazi niliyokuwa naenda kufanya. Hadi sasa, baada ya kugundua ukweli huo, nimesitisha kushiriki kwenye semina hizo.

Aidha, kutokana na kujitoa kwenye mfumo huo, kwa sasa wanataka kuniondoa katika eneo nililolipia makazi ya miezi mitatu, huku nikiwa sina uwezo wa kupata nauli ya kurudi Tabora.

Nina wasiwasi kuwa bado kuna vijana wengi wanaendelea kuvutwa kwa ahadi kama hizo za ajira, kisha kuombwa kulipa fedha mbalimbali wakiamini wanaenda kuajiriwa.

Naomba mamlaka husika kufanya uchunguzi wa suala hili pamoja na kusaidia kupata ufumbuzi wa hali ninayopitia, ili kuzuia vijana wengine kuendelea kuathirika kwa namna hii.
 
Kua makini na kazi hasa zinazotangazwa online kupigwa njee njee japo wengine wa kweli
 
Jiajirini vijana unashindwa hata kusajili laini mtaani au kuuza mitumba mpaka uajiriwe?
Kumwambia mtu ajiajiri ni rahisi sana. Hata mimi nlikuwa najua kujiajiri ni kitu rahisi .

Mtu kama ana access ya kuajiriwa sehemu ni bora akaanzia huko ndiyo awe anajaribu miradi midogo midogo akiwa huko na back up.

Halafu siyo kila anayejiajiri anafanikiwa, unaweza ukajiajiri ukajituma hata miaka 10 bila kupiga hatua kubwa ya kuonekana na aliye ajiriwa akakuzidi
 
Kumwambia mtu ajiajiri ni rahisi sana. Hata mimi nlikuwa najua kujiajiri ni kitu rahisi .

Mtu kama ana access ya kuajiriwa sehemu ni bora akaanzia huko ndiyo awe anajaribu miradi midogo midogo akiwa huko na back up.

Halafu siyo kila anayejiajiri anafanikiwa, unaweza ukajiajiri ukajituma hata miaka 10 bila kupiga hatua kubwa ya kuonekana na aliye ajiriwa akakuzidi
Kwahiyo kwako wewe ni bora uajiriwe kwa muhindi mshahara 120k kwa mwezi kuliko kufanya biashara kisa huwezi
 
Kuna hii biashara vifaa vya simu chaja, airphone na vikolokolo vingine inalipa faida hadi ×3 ya bei ya jumla mfano betry dogo waweza nunua buku ukaliuza 3000 hadi 5000
Ni kweli kabisa kuna usb, protector unanunua buku buku unauza kuanzia buku 3-5! Shida vijana wengi hawana pa kuanzia!
 
Ni kweli kabisa kuna usb, protector unanunua buku buku unauza kuanzia buku 3-5! Shida vijana wengi hawana pa kuanzia!
Uvivu wa kufanya kazi na kujitaftia kijana anataka akitoka kumtegemea baba ake akamtegemee muajiri yeye mwenyewe hawezi kuishi kwa kujitegemea

Hivyo vitu mtaji ni mdogo sana unakuta huyo anaelalamika ajira anatumia simu ya 500k na makolokolo kibao getoni, tv sabufa kitanda kikubwa godoro inch10 lakin mtaji wa 300k au 200k hana
 
Back
Top Bottom