Ukombozi ni kiherehere cha kutafuta kipigo

Ukombozi ni kiherehere cha kutafuta kipigo

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
798
Reaction score
865
Mzee Nyerere na wenzake walimaliza zamu yao ya ukombozi wa Afrika.

Sisi tumebaki na zamu ya kupambana na maisha yetu, kulipa bili na kutafuta hela za kula bata kidogo.
Kujifanya mkombozi wa awamu ya pili ni kiherehere cha kutafuta kupigwa ili ulie, na ukipigwa ukakaa kimya unapigwa tena na tena ili ulie, mpaka ubaki unalia kama mbwa koko aliyekwama kwenye mtego wa kuku bandani.

Linda afya yako ya akili, pambana na hali yako, kula bata kwa kiwango chako!

2fb6c41b-1073-4922-a71b-717fec8fb89a.png
 
Utakuta mleta mada ni baba wa Familia, watoto wake wamepata baba Zezeta kwelikweli.
Kwahiyo Jeshi lifutwe ili kila mmoja apambane kula bata?
Huelewi topic, kaa utulie.
 
Wazungu wakiuonea aibu uongozi wa nchi uliopo madarakani hutumia vibaraka wao, hizi siasa nyingi za kutafuta uhuru wa pili zinafadhiliwa na hao hao wenye hasira na uongozi wa SSH.

Wasipokuonea aibu watakuua huku kila mtu akijua wamekuua kama walivyomfanya Patrice Lumumba kwa kumchoma ndani ya pipa la acid.
 
sijawahi kuelewa, hivi ni kwa nini tanzagiza watu wanapenda sana kupiga walio mzidi nguvu? sababiu hasa ni? ningeelewa kama ingekuwa confined kwa watu wachache ambao wana psychological problems, lkn ni nchi nzima mni hivyo aliye kuzidi nguvu anakupiga, why? ...

View: https://www.youtube.com/shorts/4K7oORA_adM
 
“Tunataka kuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini , si vijana waoga ,akina ndiyo bwana mkubwa, vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga Vita mfumo wa jamii isiyo shabihiana na matakwa na matalajio ya jamii ya Kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mfumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa”.

Mwalimu JK Nyerere v.
 
Hizi blue tick za JF zinatolewa kwa vigezo gani?

Mbona mpaka machizi wanazo!.
Zipo za aina mbili kuna wale walijisajiri kwa majina yao na vitambulisho ameviasubmit.
Na nyingine ile ya platinum member unalipia
Mengine Soma mwongozo wa Jf
 
Uzuri tunaandamana sisi, tunakimbilia majumbani na mitaani, ninyi mnaojificha ndani ndo linawakuta jambo sasa. Uzuri Risasi za wahuni hazichagui.
 
Mzee Nyerere na wenzake walimaliza zamu yao ya ukombozi wa Afrika.

Sisi tumebaki na zamu ya kupambana na maisha yetu, kulipa bili na kutafuta hela za kula bata kidogo.
Kujifanya mkombozi wa awamu ya pili ni kiherehere cha kutafuta kupigwa ili ulie, na ukipigwa ukakaa kimya unapigwa tena na tena ili ulie, mpaka ubaki unalia kama mbwa koko aliyekwama kwenye mtego wa kuku bandani.

Linda afya yako ya akili, pambana na hali yako, kula bata kwa kiwango chako!

na mimi nasema wapigwe tu maana hakuna namna nyingine sasa 🐒
 
Wanaanza hivyo hivyo halafu baadaye wanaanza kulialia miili ya ndugu zao , wapumbavu acha wapigwe
 
Mzee Nyerere na wenzake walimaliza zamu yao ya ukombozi wa Afrika.

Sisi tumebaki na zamu ya kupambana na maisha yetu, kulipa bili na kutafuta hela za kula bata kidogo.
Kujifanya mkombozi wa awamu ya pili ni kiherehere cha kutafuta kupigwa ili ulie, na ukipigwa ukakaa kimya unapigwa tena na tena ili ulie, mpaka ubaki unalia kama mbwa koko aliyekwama kwenye mtego wa kuku bandani.

Linda afya yako ya akili, pambana na hali yako, kula bata kwa kiwango chako!

Nanukuu hapa: "Linda afya yako ya akili, pambana na hali yako, kula bata kwa kiwango chako!"
1.Unalindaje Afya ya akili ikiwa umezamishwa kwenye lindi la ukandamizwaji kwa lazima?? Yumkini lazima utapata msongo wa mawazo kwani unatamani kujinasua lakini njia imefungwa kwa makusudi. Hilo ni Gereza kimawazo.
2. Unapambanaje na hali yako ikiwa mikono yako ya kupambana imefungwa? au Nyenzo/Silaha muhimu katika mapambano hayo zimezuiliwa au ni marufuku kwako(Umewekwa fungu moja la voiceless).
3. Aisee; unakulaje bata wa kiwango chako ambaye unajua fika 100% huyo bata sio saizi halali kwako halafu ni bata Feki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom