Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,176
- 157,169
Tumeenda vizuri na hili mbunge la kutafuta baba mpotevu. Ila kitu kimoja ndugu Mentor ningependa kuongezea hapa kuhusu hawa mabinti wa humu JF. Na huyo Kiranga wao.
Mi naona kama wana underestimate sana mapenzi ya baba kwa mtoto. Mtoto anakaa tumboni mwa mama, lakini nakuhakikishia hakuna faraja inafanana na ile unaipata unapojua mtoto huyo tumboni umeweka wewe. Ufahamu ule unapandisha sana thamani ya huyo mama aliyebeba huyo mtoto wako. Furaha inaongezeka mtoto huyo anapokuja kutoka sasa, na wewe unajiona katika huyo. Sasa unakuwa na vitu viwili vya thamani sana katika maisha yako: mama na mtoto wako.
Hapa lazima kulikuwa na conflict ya si mtoto wangu. Hakuna baba mwenye akili timamu atakataa mtoto wake. Pigia mstari neno akili timamu. Mimi namjua mtu ambaye alimzalisha mwanamke mmoja kwa taarifa ya siri kuwa mume alikuwa hana kizazi. Huyu mwanamume aliteta nami akasema hakuna kitu kinaumiza roho yake kama kuona mtoto wake analelewa na mtu ambaye si baba yake wakati haiwezekani kutangaza rasmi nini kilifanyika pale kijijini. Anasema nilifanya kosa sana kukubali kumzalisha mama yule. Anajutia kukosa haki ya kujulikana yeye ndiye baba wa mtoto yule, ambaye hivi karibuni anamalizia masono yake ya Advanced level.
Nani ana underestimate mapenzi ya baba kwa mtoto? Mimi ninayesema baba asiyeonyesha mapenzi ha deserve kumuona mtoto au wewe unayesema it's no big deal?
Unajuaje kwamba huyu baba ana akili timamu?
Kama ana mapenzi yote hayo kwa nini hajamtafuta mwanawe?
Kwa nini mwanawe ajipandikize sasa?