Uko wapi baba?

Uko wapi baba?

Prisss

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2013
Posts
233
Reaction score
735
HAbari wana Jamvi. Hope your weekend is great kama ambavyo yangu pia ingekuwa kama Hili lingetimia. Mniwie radhi kama hapa si mahala pake as nimeona pananifaa zaidi kuwasilisha hili niweze pata walau msaada toka kwenu.

Namtamtafuta Baba yangu Enock Rugangira niliyempoteza since nikiwa na umri wa kutoweza hata kumtambua (6 month)

Here is my Short Life Story
Naishi na mama pamoja na wadogo zangu wawili, Mmoja wa kike na wa mwisho wa Kiume. Nilizaliwa mwaka 1988 mkoani Arusha na mamayangu Marry Pascal Kundi wakiwa wakiishi na ambaye ni baba yangu mkoani Arusha, wakati huo Baba akiwa mfanyabiashara wa madini. Kwa maelezo ya mama yangu, Nilipofikisha umri wa miezi 6 baba yangu alitoweka akiwa katika mizunguko ya kibiashara. Mbaya zaidi tangu nilipojitambua nimekuwa nikikosa ushirikiano kwa mama yangu kila ninapotaka kujua kuhusu alipo baba yangu, jambo linaloashiria mazingira waliyopotezana naye hayakuwa mazuri kwa maana ya namna flani ya ugomvi. Majibu ninayoyapata mara nyingi toka kwake ni simply "baba yako amekufa kwenye ajali ya MV Bukoba" with no any narration jambo linalonipa mashaka kuwa ni majibu ya kunipotezea nisifuatilie zaidi kumhusu baba yangu.

Now am grown up na namhitaji Baba yangu kuliko kitu chochote, walau kumuona then i think my Life will be complete.
I know JF is wide and i believe somehow somewhere this can help.

Kwa yeyote baina yenu wana jamvi aliye walau na clue ya Hili jina "Enock Rugangira" anifunulie hili tafadhali.

kabila gani?
mtu wa wapi?
ukoo wa nani?
akiishi mji gani, mtaa gani?
Akiuza madini gani, na akiuzia wapi?

je umemuliza mama ako kama anawajua jamaa wa baba ako?
au rafiki wa baba ako?

Pengine huyo baba ako kaoa na mama yako alikuwa nyumba ndogo.
Ama baba ako amekukataa toka upo tumboni
Ama baba ako alimnyanyasa mama ako
Ama upo hatarini ukimjua baba ako
 
Haya ubarikiwe....umeishi miaka zaidi ya 20 bila yeye vipi tena leo unamhitaji zaidi. Yeye pia anawajibika kukutafuta, yawezekana kweli alikufa kwenye MV Bukoba.
 
You dont know the pains ambavyo mtu anapata anapoona wenzie wapo na wazazi wao wakati yeye hana wazazi na haambiwi ukweli. Nina uhakika kuna orodha somewhere ya wahanga wa MV Bukoba. Anayefahamu amsaidie huyu binti
 
Pole sana. Mungu akujalie umpate. Jaribu kuongea pia na ndugu wa karibu wa mama wakupe detail nying zaidi.

Pia unaweza kumtafuta kupitia vipindi mbali mbali vya redio.. Mfano cha radio one sterio

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sijawahi kuelewa kwa nini mtu amtafute baba yake, baba ambaye hajamtafuta.

Human psychology is very complex Kiranga. Kuna mambo hata waliobobea katika fani hii hawajaelewa wakamaliza.
Na hili ni la kawaida sana. Ungependa kujua character traits zako zinatoka wapi. Inakupa raha kujitambua.... Kujitambua Kiranga; that's all.

Nadhani catch ni kumtafuta rafiki yake mama aliokuwa msichana kipindi kimoja, na sasa ni mtu mzima. Atatoa details
tu. Wasichana hawanaga siri hata kidogo wakiopoa kidume kinaaminika kuwa na hela. Lazima watakuwapo marafiki zake mamake huyu binti wanajua habari za baba huyo; na kutoka kwa huyo sasa tafuta marafiki zake babako wa kiume. Marafiki zake mama watamhurumia tu mtoto wampe details....

Haya we kabinti tafuta marafiki zake mamako wa enzi hizo... Kama mamako hajui JF atakuwa hajaona haya maelezo. Unaeza hata kumuuliza yeye mwenyewe eti marafiki zake wa enzi hizo wanakaa wapi: "anza hivi...hivi we mama mashosti zako wa enzi hizo wako wapi siku hizi"... pata wawili watatu; anzia hapo.
 
mwambie huyo mama yako akueleze ukweli kama alikuficha mweleze unakwenda kuangalia kwenye orodha ya watu waliokufa kwenye MV Bukoba, utaipata nafikiri kwenye ofisi zinahusiana na maafa au majanga,mwambie ukikosa jina patachimbika! ....halafu uone kama kaficha atababaika halafu uwe serious sawa eh.
 
Human psychology is very complex Kiranga. Kuna mambo hata waliobobea katika fani hii hawajaelewa wakamaliza.
Na hili ni la kawaida sana. Ungependa kujua character traits zako zinatoka wapi. Inakupa raha kujitambua.... Kujitambua Kiranga; that's all.

Nadhani catch ni kumtafuta rafiki yake mama aliokuwa msichana kipindi kimoja, na sasa ni mtu mzima. Atatoa details
tu. Wasichana hawanaga siri hata kidogo wakiopoa kidume kinaaminika kuwa na hela. Lazima watakuwapo marafiki zake mamake huyu binti wanajua habari za baba huyo; na kutoka kwa huyo sasa tafuta marafiki zake babako wa kiume. Marafiki zake mama watamhurumia tu mtoto wampe details....

Haya we kabinti tafuta marafiki zake mamako wa enzi hizo... Kama mamako hajui JF atakuwa hajaona haya maelezo. Unaeza hata kumuuliza yeye mwenyewe eti marafiki zake wa enzi hizo wanakaa wapi: "anza hivi...hivi we mama mashosti zako wa enzi hizo wako wapi siku hizi"... pata wawili watatu; anzia hapo.

Kujitambua hakuji kwa kuangalia nje. Bali kwa kuangalia ndani.

Kuna human elements za kujisikia incomplete hapa, ambazo ni the opposite of kujitambua.

Baba ambaye hana habari na mtoto hana haki ya kujua habari za mtoto.

For all we know kakaa raha mustarehe na mke na watoto wake. Kwa nini kumpelekea unwanted dramatic intrusions into his life kama mwenyewe hataki kumtafuta mtoto?

I could easily see the stepma drama, the precarious position the father will be in, all the hazards of a mixed family in our settings.

I only raise these points, brutal as they may seem, because they are very pertinent.
 
Haya ubarikiwe....umeishi miaka zaidi ya 20 bila yeye vipi tena leo unamhitaji zaidi. Yeye pia anawajibika kukutafuta, yawezekana kweli alikufa kwenye MV Bukoba.
kama a
mekufa ni sawa but ningemfaham pia ningefrah
 
You dont know the pains ambavyo mtu anapata anapoona wenzie wapo na wazazi wao wakati yeye hana wazazi na haambiwi ukweli. Nina uhakika kuna orodha somewhere ya wahanga wa MV Bukoba. Anayefahamu amsaidie huyu binti
asante
 
kama mama yako ana tabia ya kuandika andika mambo kama kumbukumbu jaribu kufanya ufukunyuzi katika chumba cha mama yako. unaweza ukapata hata kijikaratasi chenye mambo yanayomhusu Dad wako. ukikipata utaanzia hapo! mathalani ukipata majina ya ukoo ya baba yako na mwenyeji wa wilaya ipi au mkoa upi utaanzia hapo. kwa information hizo unaweza hata kutuma Tangazo kwenye radio ukieleza particulars za baba yako, mama yako na wewe pamoja na namba yako ya simu ili atakayehisi anahusika awasiliane nawe.
 
Haya ubarikiwe....umeishi miaka zaidi ya 20 bila yeye vipi tena leo unamhitaji zaidi. Yeye pia anawajibika kukutafuta, yawezekana kweli alikufa kwenye MV Bukoba.

With all due respect, mwiba uliopo mguuni kwa mwenzio huwezi kujua maumivu yake. Tatizo sio baba peke yake, kuna swala la identity hapa na kama ni mtoto wa kiume ni ngumu sana kuishi bila kujua your roots.
 
Ningekuwa mie wewe, kwanza ningempongeza mama for being there. Angeweza kuwatelekeza. Lakini ameonyesha yeye ni mwanamke kweli na kukomaa na wanawe. Baba ambae hana time na mimi, hata tukikutana kwa bahati mbaya atahitaji kuwa na sababu nzuri sana sana za kwa nini hakuweza kuwa kwenye maisha yangu japo kwa barua!

Move on, like ur mom! Kafa huyo kwenye ajali ya mv maisha! Unaweza kumjua akaishia kukumess up tu! Na kukuvuruga for the rest of your days. Haumuhitaji kwa ajili ya maisha yako kuwa complete!
 
unamuhitaji baba yako ambaye hajakulea wala kuwa na uchungu nawe kuliko kitu chochote? ( mf yupo hai) ili iweje?
 
Ningekuwa mie wewe, kwanza ningempongeza mama for being there. Angeweza kuwatelekeza. Lakini ameonyesha yeye ni mwanamke kweli na kukomaa na wanawe. Baba ambae hana time na mimi, hata tukikutana kwa bahati mbaya atahitaji kuwa na sababu nzuri sana sana za kwa nini hakuweza kuwa kwenye maisha yangu japo kwa barua!

Move on, like ur mom! Kafa huyo kwenye ajali ya mv maisha! Unaweza kumjua akaishia kukumess up tu! Na kukuvuruga for the rest of your days. Haumuhitaji kwa ajili ya maisha yako kuwa complete!

Umenena, anaweza kumtafuta akaja kumpata alafu baadae ikawa nongwa,......inatokea sana katika maisha mtu hajui ulikuwa unaishije, alafu unamtafuta ukimpata anajiona yeye ndo anastahili kufanyiwa kama mzazi. Anasahau yote aliyokutendea.....mambo ya binadam hayooo
 
Mtu ambae hajajishughulisha na shida na challenges zangu za maisha out of nowhere aanze kunihusisha na matatizo yake? Hell no, huyo angechangia mbegu yu aisee. Agu wanakuwaga very demanding manake hawana huruma wala nini!

pole sana.
Zungumza vizuri na mama,atakupa pakuanzia kumtafuta.
 
Mtu ambae hajajishughulisha na shida na challenges zangu za maisha out of nowhere aanze kunihusisha na matatizo yake? Hell no, huyo angechangia mbegu yu aisee. Agu wanakuwaga very demanding manake hawana huruma wala nini!

Mimi ni victim wa hii kitu, usiombe ukutane na watu wa hivi.....mara amesusa, mara anashitaki ohh humjali, humheshimu.,,,duhh yani ni majanga! I even regret why nilikutana nae....
 
Back
Top Bottom