Ukizeeka unataka kuwa nani?

Ukizeeka unataka kuwa nani?

Pole pole yupo 55 yrs Ila Kama Ana 40 hivi
kwakwel toka niwe alone, kipaumbele changu namba 1 ni afya yangu. Zoezi kali , maji mengi na kupumzika vya kutosha.
Nimeanza ku prepare my retirement life from now. Mungu akinijaalia uzima, natamani kuja kuishi nikiufurahia uzee wangu.very Few people around me, more resourses to support me.
 
Natamani niwe mpole no story za ujinga na watu yaani nakuwa mpole na mshauri wa mambo ya kijamii kwa watu wataokuwa wanakuja kuniambia mambo yao .

Ila sasa nawaza kuwa je nitaweza maana hapa nilipo naitwa Google na wanakijiji maana hakuna nisilolijua na pia kwenye kundi la wengi mimi ndiye nakuwa kinara wa maongezi ukweli uongo humo humo kikubwa niwe main speaker .

Nisaidiwe ikiwa kuna namna ya kuwa mpole hapo badaye ili niwe nimeziishi ndoto zangu
Utaweza kuwa mshauri wa watu? Friji linagandisha? Usije kuambiwa issues za watu ukazimwaga hadharani
 
Natamani kuja kuwa mfugaji tena ufugaji wenye tija be it cows, mbuzi, kuku ama samaki. Ila pia ninapenda niwe mwalimu wa watoto wadogo darasani, ninapenda sana kuona namna watoto wanavyofurahia maisha namna wanavyodadisi mambo na namna wanavyojifunza. Ninaamini kama walimu wa chekechea na primary hadi darasa la tatu au nne hapo wanaishi kwa raha sana kama wanaipenda kazi yao. It is stress free na una una interact na watu innocent, charming na wakweli. Cha msingi niwe na hela tu.
 
Ujana unasemwa ni maji ya moto.. Hivyo harakati ni nyingi na ndoto ni nyingi na mipango ni mingi pia.. Lakini taratibu umri unavyosogea vyote hivyo hupungua na hatimaye kwisha kabisa..
Kuna mambo ya kufanya ujanani ambayo mtu hapaswi kufanya uzeeni
Uzee una mengi yasiyopo ujanani na ndio maana wanasema fainali uzeeni
Ila kama kuna mambo hukuyafanya ujanani kina uwezekano mkubwa ukayafanya uzeeni
Kumbuka wahuni pia huzeeka.. Na baadhi huzeeka na uhuni wao... Na ni rahisi kuwa mwanga uzeeni kuliko ujanani kwasababu ya upweke
Mimi nikizeeka nataka niwe pastor.. Vipi kuhusu wewe... ( kama utazeeka lakini😂)
Aisee,mimi nilipanga nikizeeka niwe mpishi,na hasa niwe baba ntilie,nilijaribu kama mara 3 hivi,nikakodi eneo nikaweka vifaa vyote,nikaajiri watu 2,watoto wangu hawakupenda.Siku moja wakanilia njama,nilitoka kurudi nyumbani,wakamtuma kijana mmoja walimlipa pesa,akaenda hapo wakaitwa hao wafanyakazi wote wakalipwa mishahara ya miezi 6,akabeba kila kitu kwenye kenta na akarudisha eneo kwa mwenyewe,ile saa 1 usiku naenda najua biashara imechanganya nakuta hola,namkuta huyo kijana,akaniambia baba nimetumwa na wanao nipafunge na kila kitu nimelipa na vifaa vyote vipo kwenye gari nielekeze nivipeleke wapi.Niliduwaa,kwakuwa yeye katumwa na pia namjua maana amekua na wanangu nilimwambie avipeleke nyumbani.Nilikaa kimya,basi kesho yake first born wangu akanipigia na kusema baba tulia nyumbani,timekuandalia bajeti yako kila mwezi utapata matumizi,nikasema sawa.Sasa nafanya kibustani kidogo hapa nyumbani
 
Back
Top Bottom