Ukizaa na mume wa mtu, mtoto ni wa kwako

Mtoto anakuja katika mazingira mengi. Wengi wangependa wazaliwe au wazae kwenye ndoa. Kuna wengine humuomba mume wa mtu azae naye tu kwakuwa anahitaji mtoto.

Wengine ni one night stand, mlienda field huko baridi ikawapiga mkafunga ndoa ya dakika kadhaa. Wengine ni michepuko ikatokea mimba ikaingia.

Basi ikitokea umezaa na mume wa mtu, ilhali ulijua yule bwana ana ndoa yake au japo hukujua, basi lea mwanao usitake kuvunja ndoa za watu.

Mpe mtoto ubin wa baba yako. Mbegu ya mume wa mtu ni zawadi yako.

Ukianza ooh mtoto ajue mila za kwao, mfyuu huo ni umbea, kwani wale watoto wa dogo dogo centre wanajua mila za kwao?

Wengi wanaotafuta baba wa watoto zao ni wale wa baba wenye pesa zao. Baba asiye na kitu hasumbuliwi labda mtoto mwenyewe awe mkubwa yake tu kujua asili yake.
Mi niligoma kutumia ubini wa mama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana anakaa na mama yake, mke amekataa, kadai atakaa nasi kama mama yake asipokuwa duniani, mrs wangu yuko very strong...
Kama anakaa na mama yake kulikuwa na haja gani ya kumwambia mkeo? Si unge provide kila kitu akiwa huko kwa mama yake?
 
Daah sisi waume za watu tuna kazi sana.. Sijui kwanini nyie mabinti mnatupenda kiasi hicho ata tukiwatongoza hamkatai mpaka na mimba zetu mnadaka..! Tuhurumieni jamani
Halafu ni kama mambo yanabadilika.... siku hizi liketokea wimbi la waume za watu kupenda wake za watu na wake za watu kupenda waume za watu. Wenyewe wanasema huo ndio uchepukaji wenye afya
 
Kuna mazingira mengine kama mama hayaweki wazi ni kheri ukae kimya.

Ila kingine nilichogundua, kuna wakati wamama mnawaharibia maisha watoto wenu bila kujua. Wewe mama ulikua na mtu (mume wa mtu ama la) mkapeana mimba, then mkaja kugombana au mkashindwana. Mama unabaki na kinyongo mtoto akizaliwa unaanza kumjaza maneno kwamba baba yako si mtu, mshenzi sana yule, sitaki hata kumsikia, nk. Ugomvi wako na mwanaume, unauhamishia kwa mtoto! Matokeo yake mtoto anakosa huduma muhimu kutoka kwa baba, pengine unakuta baba anao kabisa uwezo wa kusaidia lakini mama anaweka kauzibe kwa kiburi chake tu mwisho mtoto anaishia kutaabika.
 
Basi tutakuwa hatuwaambii...

Kwani Sky si kashatangaza hawatakiwi kutambulika

Wanazaa kwa raha zao, mtoto unaletewa wewe ulee..... wakati wewe uko busy kuwatunzia mtoto wao wenyewe wanaendeleza kula maraha
Mimi nitalea niliyemkuta tuu
 
Ila kingine nilichogundua, kuna wakati wamama mnawaharibia maisha watoto wenu bila kujua. Wewe mama ulikua na mtu (mume wa mtu ama la) mkapeana mimba, then mkaja kugombana au mkashindwana. Mama unabaki na kinyongo mtoto akizaliwa unaanza kumjaza maneno kwamba baba yako si mtu, mshenzi sana yule, sitaki hata kumsikia, nk. Ugomvi wako na mwanaume, unauhamishia kwa mtoto! Matokeo yake mtoto anakosa huduma muhimu kutoka kwa baba, pengine unakuta baba anao kabisa uwezo wa kusaidia lakini mama anaweka kauzibe kwa kiburi chake tu mwisho mtoto anaishia kutaabika.
Kuna wanaume wanasema kabisa hiyo mimba hesabu sio yangu. Kama hutaki kuitoa hata mtoto utakaemzaa simtambui na usinihusishe na mambo yake.... bado unazaa na yeye anaendelea kumkataa mtoto. Hapo mama anafanya nini zaidi ya kumuasili mtoto
 
Halafu ni kama mambo yanabadilika.... siku hizi liketokea wimbi la waume za watu kupenda wake za watu na wake za watu kupenda waume za watu. Wenyewe wanasema huo ndio uchepukaji wenye afya
ila kuna kaukweli hapo hahahh et uchepukaji wenye afya :D huo ndo mwanzo wakulea watoto ambao si wako unajikuta ujui mimba ya mume au mchepuko
 
wanaume tungekuwa na aklili nzuri tungekuwa tunasubiri tu watoto wa ndoa yaani ukishachanganya nyumba hainaga amani kabisa na ukute unapenda watoto kama mimi yaani ukimleta nyumbani kila analofanyiwa na wife home utaona anaonewa maana abadan hawezi kupata malezi sawa na wa kwake
 
Back
Top Bottom