Michepuko ya mume wangu ni ndugu zake wa damu

Smart AJ

JF-Expert Member
Mar 21, 2022
5,540
5,752
PART 1
MICHEPUKO YA MUME WANGU NI NDUGU ZAKE WA DAMU

Zamani nilikuwa nikisikia mtu anasema Ndoa sio ya kukimbilia au mwingine akisema ndoa sio kitu cha mchezo nilikuwa naona kama wananionea wivu. Kabla sijaolewa Shangazi yangu aliniambia hakikisha kabla hujaingia kwenye ndoa umemjua huyo Mwanaume anaekuoa vizuri yeye pamoja na familia yake. Hakikisha unawajua ni watu wa aina gani na wanaishije. Kiukweli nilimsikiliza Shangazi na kumuitikia kana kwamba nilifanyia kazi kile alichonishauri lakini haikuwa hivyo. Akili yangu yote ilikuwa kwenye Ndoa, nifunge ndoa nipendeze siku ya harusi tufurahi na kushangilia.

Nilifunga Ndoa na Mume wangu Fabian mwaka 2021, kweli tulikuwa tunapendana sana na wote tulikuwa na hamu ya kuoana na kuishi pamoja. Mume wangu hakuwa Mtu wa starehe wala wanawake. Kipindi chote cha uchumba kama hayuko na Mimi au hayuko kazini basi atakuwa pamoja na ndugu zake kwani aliniambia kuwa familia yake ni familia yenye umoja ambayo Ndugu huwa wanapanga siku za kutoka na kukaa pamoja. Hivyo hata tulivyoowana kuna muda huwa anatoka na kurudi usiku sana na maranyingine asubuhi kwani anakuwa yupo na Ndugu zake na sikuwa na tatizo na hilo.

Nakumbuka siku yangu ya Mahari familia ya Fabian ilikuja kwetu, walikuja Ndugu zake wengi wakiwemo wadogo zake watoto Shangazi, Mama wakubwa na wadogo. Ila kitu cha kushangaza ni kwamba ulipofika muda wa pete, mmoja wa mabinti ambaye ni Mtoto wa Mama yake Mdogo alianza kulia akatoka nje. Ndugu zangu waliniuliza yule ni nani na mbona alikuwa analia wakati unavalishwa Pete nikawaambia ni Dada yake Fabian Mtoto wa Mama Mdogo, wakasema sasa kwanini alie vile. Nikanyamaza sikuwa na majibu nikajua labda anadeka tu.

Chakushangaza hata Siku ya Harusi, wale mabinti ambao ni ndugu zake hawakuwa na furaha kabisaaa, walikuwa wamenuna tofauti na nilivyotarajia. Nikajiuliza sana maswali, ila nikahisi hawanipendi labda walitaka kaka yao aoe Mwanamke mwingine na sio Mimi. Baada ya harusi nilimuhadithia rafiki yangu akasema wakwe ndivyo walivyo, unatakiwa uwazoee tu, mradi ushaolewa wavumilie tu. Kwasasa wapotezee mbeleni watakuelewa na mtaishi vizuri tu. Basi nikatulia hofu ikapungua.

ITAENDELEA PART 2
 
PART 2
MICHEPUKO YA MUME WANGU NI NDUGU ZAKE WA DAMU

Tukiwa Honeymoon kuna muda nilimuoma Mume wangu yuko busy sana na simu mara anapokea mara anakata, mwishoni akaniambia "Unajua leo nilimuahidi Mercy kuwa nitampeleka kula Ice cream, sasa bahati mbaya tuko honeymoon ila naomba nimpekele maramoja akachukue Ice cream then narudi, asijisikie vibaya. Sitaki wanihisi vibaya au waone nawatenga sababu nimeoa.

Nikamwambia sawa wapeleke tu, na Mimi uniletee. Basi Mume alitoka akaniambia niende Salon nikafumue nywele za harusi maana zilikuwa zimejaa kichwa kinakuwa kizito. Hivyo nilienda Salon yeye akatoka na Mercy Mdogo wake. Mume wangu alirudi saa sita Usiku na Ice cream lakini nilikuwa nimeshalala so siku ila. Siku iliyofwata tukatoka Hotel kurudi nyumbani.

Baada ya kufika nyumbani, Wakwe zangu waliandaa sherehe ndogo ya kunikaribisha nyumbani kwao. Hivyo siku hiyo tulijiandaa tukaenda nyumbani kwa wakwe kwa ajili ya sherehe. Sherehe ilikuwa nzuri, ndugu walikuwa wengi na ilipendeza sana. Lakini cha kushangaza, hapo kwenye sherehe Mume wangu na wadogo zake walikuwa wanacheza mziki, mara wakumbatiane sikuelewa ila nikaamua nitulie maana ni ndugu zake nisije haribu familia ya watu. Kiukweli kwa ule ukaribu hata Mimi siwezi fanya vile na kaka yangu.

Wakati wa zawadi, wote walitutunza kwa pamoja lakini nikashangaa Mercy kanunua Tshirt, jeans na saa kwa ajili ya kaka yake tu. Na akashika Mic akasema nakupenda sana kaka yangu wewe ndio kila kitu kwangu, japo umeoa lakini sitaacha kukupenda, baadae akaenda kumkumbatia akaliaaaa watu wakaja kumshika. Nilikuwa kama naona vihoja, sielewi.

Baada ya pale nikamwambia Mume wangu, mbona huyu Mercy ni mdogo wako lakini ukaribu wenu unatia mashaka na kwanini alilia vile kuna shida gani? Akakasirika akanifokea, akasema ishia hapo hapo naomba usinitenganishe na wadogo zangu, hawa ni wadogo zangu na Mimi ndio kaka yao naomba usituingilie. Wewe ni Mke wangu wale ni wadogo zangu ni vitu viwili tofauti. Acha wivu usio msingi.

Kiukweli sikuwa na amani kabisaa na huyu Mercy na hao ndugu wengine, nilihisi kuna kitu ila sikutaka kuamini kwa wakati ule ilikuwa mapema sana kuanza kusema.

ITAENDELEA PART 3
 
PART 3
MICHEPUKO YA MUME WANGU NI NDUGU ZAKE WA DAMU

Kuna siku nimekaa nyumbani, shangazi wa Mume wangu akanipigia simu akasema Mkwe mwanangu amefunga chuo wiki mbili, na amezoea chuo kikifungwa huwa anakaa kwa kaka yake yani Mume wangu baadae wakifungua anarudi chuo. Akasema naomba umpokee ukae nae nikasema sawa.

Kweli jioni Mume wangu alinipigia akasema Lisa kafunga chuo naenda kumfwata nije nae, nikasema sawa. Jamani nilikaa mpaka saa sita usiku ndio Mume wangu anarudi kalewa chakali na kadogo kake Lisa. Nilishangaa, nikamuuliza Lisa amekufwata saa ngapi mbona kalewa sana, akasema tulikuwa wote tangu jioni tulienda mziki, nikasema kama hivyo sawa. Basi wakaingia ndani tukalala.

Lakini cha kushangaza yule Binti Lisa alikuwa anavaa nguo fupi mnoo pale ndani, nguo za uchi kabisa na kila jioni lazima atoke amfwate Kaka yake kazini warudi wote. Kifupi ni kwamba tangu Lisa kafika kwenye nyumba yangu, mahusiano yangu na Mume wangu yaliharibika. Mume wangu hana mda na Mimi kabisaaa. Wiki zote mbili yuko busy na Lisa hakuna kunikiss wala tendo, yeye ni kurudi Usiku kalewa. Nikaanza kuchanganyikiwa nikahisi kwamba labda Lisa ana rafiki yake wanasoma wote chuo ambaye ndio anatoka na Mume wangu. Kwahiyo nikasema nianze kufwatilia simu ya Mume wangu nijue.

Wiki mbili ziliisha Lisa akarudi shule, siku aliyoondoka Lisa ndio Mume wangu alirudi mapema sana nyumbani na akawa na mapenzi na Mimi. Yani kwa wiki mbili ndio nikaanza kupendwa tena. Sio siri iliniuma sana. Nikasema hapa kuna kitu, haiwezekani haka katoto kalivyokuja humu ndani mapenzi hakuna mpaka kaondoke lazima nimjue huyo mwanamke wanaemuunganishia Mume wangu. Nikasubiri Mume wangu alale usiku nichukue simu niangalie. Kiukweli sinaga desturi ya kuchukua simu ya Mume wangu lakini ilinibidi nichukue maana nilikuwa sina amani.

Jamani ule usiku Mume kalala nikachukua simu nikaenda Sebleni aisee nafungua Message za Lisa naona kaandika "WEWE NDIO MWANAUME WANGU NIKUPENDAE, UMENIFUNDISHA MAPENZI NA SIWEZI PENDA MTU MWINGINE ZAIDI YAKO", nyingine kaandika "WEWE NI MUME WANGU NAKUPENDA SANA, Mara nimekumiss, wewe mtamu. Kiufupi ni kwamba Mume wangu alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Lisa mtoto wa shangazi yake. Na yanaonekana ni ya muda mrefu tu.

Baadae nikaingia kwenye Message za Mercy, huyu ndio nilikuwa na hamu nae sana. Kwa Mercy ilikuwa inaonyesha kuwa wana ugomvi tangu kaoa Mercy hana raha anamwambia "KWANINI UMEOA NA UNAJUA NAKUPENDA, MIMI NAUMIA NIKIKUONA NA MKEO NAOMBA UACHANE NAE, NITAJIUA SIWEZI" na nikaona message za Mume wangu akimbembeleza akimwambia hanipendi kama anavyompenda yeye, na message za miamala ya hela. Inaonekana Mume wangu anampa sana pesa huyu Mercy.

Niwe mkweli sikuwahi waza kitu kama hiki kuja kunitokea, bora Mume wangu angekuwa na michepuko huko nje lakini kutembea na wadogo zake tena wa damu, niliona kama nimemwagiwa maji ya moto naungua. Nilihisi mwili kuisha nguvu, hapohapo nikaanza kulia mwenyewe nikalala chini. Nililia sana sana sikuamini nilichokuwa nakiona.

ITAENDELEA PART 4
 
PART 4
MICHEPUKO YA MUME WANGU NI NDUGU ZAKE WA DAMU

Baada ya kusoma message ndio nikagundua kuwa Mume wangu anatembea na Mercy Mtoto wa Mama yake Mdogo na Lisa mtoto wa shangazi yake. Nika ziscreen shot zile message zote nikajitumia kama ushahidi. Halafu Mume wangu alipoamka sikumwambia chochote niliona nitulie kwanza nisikurupuke.
Maisha yakaendelea, tulikaa kwa amani kabisa sikusema chochote wala sikuonyesha ishara yoyote. Japo nikawa naona Mume wangu anawasiliana na Mercy anatoka nae. Nikatulia tu.

Siku moja nilimuaga Mume wangu kuwa naenda nyumbani Bibi yangu alikuwa mgonjwa, na nilimwambia nitakaa kama siku mbili ndio nitarudi. Jirani na kwangu kuna Mdada ambaye tulikuwa marafiki sana nikamwambia naomba uangalizie nyumba yangu, ukiona chochote nijulishe.
Nikiwa nyumbani usiku akanipigia simu yule jirani yangu akasema namuona mumeo na kabinti kadogo wameingia ndani, nikamuuliza kapoje akanielekeza nikajua tu huyo ni Mercy. Roho iliniuma sana. Kesho yake Mume wangu alinipigia simu akaniuliza mgonjwa anaendeleaje? Nikamwambia hajambo akasema naomba usirudi jumamosi nitakuja kukufwata ili na Mimi nije kumuona Mgonjwa, nikasema sawa. Akanitumia hela za kutosha tu. Na nikawasiliana na jirani akasema yani tangu walivyoingia jana mpaka mida hii hawajatoka hata kazini hajaenda wapo ndani, nikasema sawa.

Akili ikanicheza nikasema huyu nikisema nikamsemee kwao tu anaweza kataa na nikaonekana mbaya, nikawaza nitengeneze fumanizi ili wote tukose. Nikaamua kumpigia Lisa simu, nikamwambia nataka nimtoe outing wifi yangu. Kanavyopenda Outing weeeh kakakubali faster, nikamfwata tukaenda mahali mbezi beach kula chakula jioni, tulivyotoka nikamwambia nataka niende nyumbani kwangu nikachukue nguo then nimuwahi mgonjwa, nikamwabia nisindikize nyumani halafu nitakurudisha chuo, akasema sawa. Basi tukawasha gari mida ya saa tatu usiku nikaendesha mpaka kwangu. Kufika getini nikamwambia chukua funguo Mume wangu hayupo, kitandani utakuta nguo zangu na vitenge chukua niletee. Kwakuwa ni mwenyeji akaingia bila shida.

Bwana weeeh baada ya kama dakika chache naona kimya mtu harudi, nikampigia simu nikasikia analia, anasema Wifi njoooo, nikamuuliza kuna nini akasema we njoo tu. Basi nikashuka kwenye gari, nikaingia ndani. Ile naingia chumbani nakuta ugomvi, Lisa na Mercy wanapigana huku Mume wangu na Mercy wakiwa uchi. Lisa akasema nimemkuta kaka Fabian na Mercy wanafanya mapenzi sijapenda. Lisa akaanza kulia anasema Wifi nisamehe nimekukosea sana lakini siwezi kaa kimya, akasema kaka Fabian nikiwa Form Four alianza kuniingilia, yeye ndio kanitoa Bikra na kipindi hicho chote naenda shule na rudi alikuwa ananiingilia mpaka leo tumekuwa wapenzi. Lakini nashangaa namkuta Mercy kitandani inamaana anatembea na Mercy pia hapana, hapana. Lisa alianza kulia kwa nguvu sana na kwa uchungu mnoo.

Nikasema hapa silazi damu nikamtoa Lisa sebleni nikampigia simu Mama Mkwe nikamwambia Mama nakuomba uje sasahivi ukichelewa utakuta nimeshauwa mtu, nikampigia wifi yangu pia Dada yake mkubwa Fabian nikamuomba aje. Nikakaa sebleni na Lisa nambembeleza analia ana galagala chini.

ITAENDELEA PART 5
 
PART 2
MICHEPUKO YA MUME WANGU NI NDUGU ZAKE WA DAMU

Tukiwa Honeymoon kuna muda nilimuoma Mume wangu yuko busy sana na simu mara anapokea mara anakata, mwishoni akaniambia "Unajua leo nilimuahidi Mercy kuwa nitampeleka kula Ice cream, sasa bahati mbaya tuko honeymoon ila naomba nimpekele maramoja akachukue Ice cream then narudi, asijisikie vibaya. Sitaki wanihisi vibaya au waone nawatenga sababu nimeoa. Nikamwambia sawa wapeleke tu, na Mimi uniletee. Basi Mume alitoka akaniambia niende Salon nikafumue nywele za harusi maana zilikuwa zimejaa kichwa kinakuwa kizito. Hivyo nilienda Salon yeye akatoka na Mercy Mdogo wake. Mume wangu alirudi saa sita Usiku na Ice cream lakini nilikuwa nimeshalala so siku ila. Siku iliyofwata tukatoka Hotel kurudi nyumbani.

Baada ya kufika nyumbani, Wakwe zangu waliandaa sherehe ndogo ya kunikaribisha nyumbani kwao. Hivyo siku hiyo tulijiandaa tukaenda nyumbani kwa wakwe kwa ajili ya sherehe. Sherehe ilikuwa nzuri, ndugu walikuwa wengi na ilipendeza sana. Lakini cha kushangaza, hapo kwenye sherehe Mume wangu na wadogo zake walikuwa wanacheza mziki, mara wakumbatiane sikuelewa ila nikaamua nitulie maana ni ndugu zake nisije haribu familia ya watu. Kiukweli kwa ule ukaribu hata Mimi siwezi fanya vile na kaka yangu.

Wakati wa zawadi, wote walitutunza kwa pamoja lakini nikashangaa Mercy kanunua Tshirt, jeans na saa kwa ajili ya kaka yake tu. Na akashika Mic akasema nakupenda sana kaka yangu wewe ndio kila kitu kwangu, japo umeoa lakini sitaacha kukupenda, baadae akaenda kumkumbatia akaliaaaa watu wakaja kumshika. Nilikuwa kama naona vihoja, sielewi.

Baada ya pale nikamwambia Mume wangu, mbona huyu Mercy ni mdogo wako lakini ukaribu wenu unatia mashaka na kwanini alilia vile kuna shida gani?. Akakasirika akanifokea, akasema ishia hapo hapo naomba usinitenganishe na wadogo zangu, hawa ni wadogo zangu na Mimi ndio kaka yao naomba usituingilie. Wewe ni Mke wangu wale ni wadogo zangu ni vitu viwili tofauti. Acha wivu usio msingi

Kiukweli sikuwa na amani kabisaa na huyu Mercy na hao ndugu wengine, nilihisi kuna kitu ila sikutaka kuamini kwa wakati ule ilikuwa mapema sana kuanza kusema.

ITAENDELEA PART 3
@Moderator , msaidieni kuunganisha uzi wake, Uzi Huu unafunza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom