Ukizaa na mume wa mtu, mtoto ni wa kwako

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,588
215,184
Mtoto anakuja katika mazingira mengi. Wengi wangependa wazaliwe au wazae kwenye ndoa. Kuna wengine humuomba mume wa mtu azae naye tu kwakuwa anahitaji mtoto.

Wengine ni one night stand, mlienda field huko baridi ikawapiga mkafunga ndoa ya dakika kadhaa. Wengine ni michepuko ikatokea mimba ikaingia.

Basi ikitokea umezaa na mume wa mtu, ilhali ulijua yule bwana ana ndoa yake au japo hukujua, basi lea mwanao usitake kuvunja ndoa za watu.

Mpe mtoto ubin wa baba yako. Mbegu ya mume wa mtu ni zawadi yako.

Ukianza ooh mtoto ajue mila za kwao, mfyuu huo ni umbea, kwani wale watoto wa dogo dogo centre wanajua mila za kwao?

Wengi wanaotafuta baba wa watoto zao ni wale wa baba wenye pesa zao. Baba asiye na kitu hasumbuliwi labda mtoto mwenyewe awe mkubwa atake tu kujua asili yake.
 
34 Reactions
Reply
Back
Top Bottom