Ukizaa na mume wa mtu funga domo lako

Pillato

JF-Expert Member
Nov 23, 2021
333
307
Katika pitapita huku na kule jamaa akajikuta amezaa na mchepuko, jamaa akamwambia mtu wake"nitamjengea nyumba mtoto tutapangisha ili pesa za matumizi na mambo mengine zitoke huko na pia huo utakuwa ndio urithi wake, kwasababu mimi nina familia sitoweza kumtambulisha huyo mtoto kwenye familia yangu, nitasababisha misukomisuko kwenye ndoa yangu.

Mchepuko ukashukuru sana na ukaahidi kutunza siri maisha yote,nyumba ikajengwa wakapata mpangaji l50K kwa mwezi, wakakubaliana hiyo pesa ya pango iwekwe benki kwa ajii ya kumsomeshea mtoto atakapokuwa amefikisha umri wa kuanza shule.

Kwahiyo jamaa akawa anatoa pesa za matumizi kila mwezi,yule bibie akanogewa na zile huduma akajisahau na kujihisi naye ni mke wa jamaa, akaanza"Hooo huyu ni mtoto wa fulani hoooo baba yake anamjali sana kamjengea nyumba maneno kedekede.

Hizi habari zikamfikia mke wa jamaa ,ugomvi mkubwa ndani ya nyumba, ikabidi Yf apeleke mashtka kwa wakweze kikao cha usuluhishi kikakaa Jamaa mbele ya wazazi wake na nduguze akakiri mtoto ni wake na nyumba kamjengea kweli, kikao kikaamua mtoto atambulishwe rasmi kwenye familia na nyumba aliyojengewa itakuwa ya familia nzima, mkewe naye akawa tayari kumlea mtoto wa mumewe bila ubaguzi Ila tu mumewe amhakikishie kutoendelea tena na mahusiano na mchepuko, jamaa akafanya hivyo kwa kiapo.

Baada ya mchepuko kuambiwa maamuzi ya kikao amekubaliana na suala moja tu la kumchukua mtoto,ila kuhusu nyumba anataka iendelee kuwa ya huyo mtoto wake tu kama walivyokubaliana awali,kwa madai kwamba hata yeye ana watoto wengine ambao siku za usoni watahitaji msaada wa kifedha kutoka kwenye hiyo nyumba.

Jamaa amegoma amemwambia mdomo wake umesababisha hayo yatokee,lakini ukweli ni kwamba yeye Mchepuko hakuchangia chochote kwenye ujenzi.

Kimenuka huko hakuna cha pesa ya matumizi wala pesa kwenda benki, Mchepuko anataka aolewe na jamaa awe mke mdogo amlee mwanaye yeye mwenyewe, jamaa naye anasema hana uwezo huo wa kuoa wake wawili na sio kuoa tu hata kuchepuka hataki tena,punguzeni midomo hizo tambo zinawaharibia.
 
Hapa ndipo wanaume wanapo fail kwakweli.

Hivi mwanaume mwenye akili zako timamu, unawezaje kumjengea side chick nyumba kwa kisingizio cha mtoto?

Anyway, wazee tunasemaga mtoto havunji ndoa, na kitanda hakizai haram. Kikubwa ni hayo yote yana zungumzika.
 
Hapa ndipo wanaume wanapo fail kwakweli.
Hivi mwanaume mwenye akili zako timamu, unawezaje kumjengea side chick nyumba kwa kisingizio cha mtoto...??
Anyway, wazee tunasemaga mtoto havunji ndoa, na kitanda hakizai haram. Kikubwa ni hayo yote yana zungumzika.
Kwahiyo ukizaa nje ya ndoa na hutaki mtoto ajulikane ni wako unafanyaje?
 
Kwahiyo ukizaa nje ya ndoa na hutaki mtoto ajulikane ni wako unafanyaje?
Mkuu, ebu ngoja nikuelimishe kidogo....
Kwanza kuzaa ni matokeo ya starehe kati ya mwanamke na mwanaume.
Lakini mtoto anapo zaliwa, kumbuka yeye mtoto hakupanga kuzaliwa (sababu mlikua kwenye starehe zenu).
Sasa mtoto hawezi akakosa haki zake za kupajua nyumbani kwao ama ndugu zake eti kwasababu alizaliwa nje ya ndoa.
 
Mkuu, ebu ngoja nikuelimishe kidogo....
Kwanza kuzaa ni matokeo ya starehe kati ya mwanamke na mwanaume.
Lakini mtoto anapo zaliwa, kumbuka yeye mtoto hakupanga kuzaliwa (sababu mlikua kwenye starehe zenu).
Sasa mtoto hawezi akakosa haki zake za kupajua nyumbani kwao ama ndugu zake eti kwasababu alizaliwa nje ya ndoa.
Uko sahihi mkuu,lakini wapo wasiopojua kwao na baba zao hawana msaada wowote kwao,utachagua kipi hapo?
 
39 Reactions
Reply
Back
Top Bottom