Ukiwa na mibaka usoni wakusengenya eti umekanyaga miwaya. Kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiwa na mibaka usoni wakusengenya eti umekanyaga miwaya. Kuna nini?

Discussion in 'JF Doctor' started by Rutashubanyuma, Oct 13, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kwa nini mtu siku hizi akiwa na mabaka usoni minong'ono na masengenyo yamwandama kuwa huyo kwisha habari yake...Amekanyaga miwaya huyo kwa maana ameshikwa na vvu na tusubiri kuitwa kuhudhuria mazishi yake.

  Zamani watu walikuwa na mibaka usoni lakini walikuwa hawanyanyapaliwi hivyo. Tusaidiane wanajamvi wenzangu kuna nini?
   
 2. njugilo

  njugilo Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ni kweli hilo huwa lipo lakini ni ufinyu wa ufahamu wa hao wanaokuangalia ,lakini basi ni vema jamii ikatambua kuwa vvu au aina yeyote ya mabaka si ukimwi wala haimaanishi kuwa umeambukizwa kwani yaweza kuwa ni matokeo ya mojawapo ya mabmbo yafuatayo ;-

  1.Ugonjwa wa ngozi ambao umesababiswa na upungufu wa chembe chembe fulani mwilini.

  2.Tatizo au adhari za matumizi ya dawa wakati wa matibabu fulani (side effect) chukua mfano wa
  dawa za malaria zilipobadilishwa wengi walipata ulemavu mfano mzuri ni zile SP.

  3.Sumu inayopatikana ndani ya chakula na haishabihiani na chembe chembe zilizopo mwili.Hili wengi
  huwa wanasema ni allegy.Unakula chakula ambacho kinaudhuru mwili bila mwenyewe kujitambua.

  Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanasababisha hii hali .Ingawa basi yawezekana ikawa kama wanavyotafsiri lakini hiyo haimaanishi atengwe au aonekane yupo tofauti.Kikubwa ni kwanza mgonjwa mwenyewe yaani mwenye mabaka ajitambue na kujikubali huku akiwa anatafuta ,ufumbuzi wa hilo tatizo hilo na pia jamii iweze kutambua kuwa si kwamba naye kapenda hiyo hali lakini imemtokea .

  Nategemea sana kwa wana JF kuwa wanamsaada mkubwa endapo watakutana na mtu au watu wenye tatizo kama hili.na kwa maoni yangu ,endapo kuna yeyote anayeweza kujua au kutoa tiba ya hilo tatizo ,amsaidie / kuwasidia mtu/watu hao endapo wanapatikana.
   
Loading...