Riwaya: To the End (Mpaka Mwisho)

THE SPIRIT THINKER

JF-Expert Member
Sep 9, 2019
392
555
HII NI SIMLIZI YA KISAYANSI NA KITEKNOLOJIA. MTUNZI NI YULEYULE TARIQ HAJJ.
HAYA NI MAONO YA MAISHA YAJAYO.

RIWAYA NYINGINE ZILIZO TANGULIZIA NI
1. CODE X
2.CODE. X 2 MCHEZO WA KIFO.
3.COD X 3 ASKARI WA KUTENGENEZWA.
4.CODE X 4 HII MTUNZI NI FRENK MASAI.

NA NYINGINEZO ZA KISAYANSI NA MAPIGANO.

TO THE END (mpaka mwisho)
KITABU CHA KWANZA

1

Na Tariq Hajj

Kalenda ya stela mwaka mia nne na tisini na tisa tokea dunia ilivyobadilisha kalenda yake. Kalenda hiyo imebadilika baada ya dunia kupata wageni kutoka anga za mbali, wageni hao hawakuwa na nia njema na dunia hata kidogo. Hivyo vita kubwa ikazuka na baada ya binadamu kugundua hakuna uwezekano wa kushinda, wachache wakaamua kuungana na wavamizi ili kunusuru maisha yao.

Ni katika nyakati hizo ngumu binadamu wakafanikiwa kupiga hatua moja mbele kiteknolojia. Silaha ya kwanza yenye uwezo wa kuwaumiza wavamizi ikaundwa. Ilikuwa ni robot ambalo liliebdeshwa na binadamu, ilikuwa imebeba silaha nzito ambazo zilikuwa na uwezo wa kusababisha madhara kwa wavamizi.

Hata hivyo halikudumu sana kutokana na marekebisho yake kuwa magumu na yenye kuchukuwa muda. Hata hivyo taratibu binadamu wakaanza kuendelea kiakili na kimwili. Na ni katika huwo binadamu wakagundua uwepo wa chembechembe maalum katika hewa aina 'itharion'.

Chembechembe ambazo ziliwapa uwezo wa ajabu katika kupambana na wavamizi wao. Kwa kupitia majribio mengo hatimae binadamu wakafanikiwa kuunda seli maalum ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya itharion kutoka katika hewa na kuzisambaza katika mwili wa binadamu.

Hilo likapelekea kuzaliwa kwa kizazi cha kwanza binadamu wapya ambao walitumika kama wanajeshi katika vita dhidi ya wavamizi. Miaka baadae binadamu wakapiga hatua nyingine na kusababisha mageuzi makubwa ya kiteknolojia.

Kwa kutumia vyuma vilivyong'oka kutoka katika mashine za wavamizi walifanikiwa kutengeneza maroboti yenye uwezo wa hali na ustadi mkubwa. Na kutokea hapo vita ikawa nyepesi na pia binadamu wakafungua kurasa mpya katika maisha yao. Kalenda ikabadilishwa na kuitwa kalenda ya stela ikiwa na maana mwaka ambao dunia ilishuhudia uvamizi na pia milango mipya ikafunguka.

**********

Republic of Iron City (mji wa chuma).

Taratibu na maandalizi ya kushherekea siku ya uhuru mwaka mia nne na tisini na tisa ziliendelea. Kila mti alionekana kuzama katika maandalizi hayo.

"Mlemavu anapita" minong'ono ilisikika kila alipokuwa akipita, kijana mwenye nywele nyeusi kuliko na macho ya rangi hazel. Alikuwa akiburuza kitoroli ambacho kilikuwa na maji ya sabuni ndani kwa ajili kufanyia usafi.

"Oooow! Kama sio Baston" kija mmoja mwenye nywele za kijani kibichi akasimama mbele ya kitoroli hicho na kumfanya Baston ashindwe kuendelea na safari yake. "Edward, unataka nini" aliuliza Baston akimuangalia usoni kijana huyo aliesimama mbele yake.

"Inaonekana kipigo cha nyuma hakijakutosha, nilikwambia unaponiona mimi huruhusiwi kuniangalia usoni" aliongea Edward na kuwapa ishara vibwengo wake.

"Inatosha" sauti laini ya mtoto wa kike ikasikika ikitokea mbali kidogo na wakipokuwa wamesimama. Ikafuatiwa na harua za taratibu kabisa ambazo kila zilipokanyaga ardhi zilitoa tafsiri ya mtu huyo aliekuwa anakuja.

"Shanequeen, hilo halikuhusu. Wewe endelea na mambo yako" aliongea Edward akimuangalia binti huyo aliekuwa anatembea kwa mwendo wa madaha.

Shida nyingine iliyozuka baada ya binadamu kugundua uwepo wa itherion ni matabaka. Japo mwanzo yalikuwepo lakini baada ya miaka kadhaa kupita yakaongezeka na kuwa makubwa zaidi. Baada ya miaka miambili wakaanza kuzaliwa watoto ambao moja kwa moja walizaliwa na uwezo wa kunyonya itherion kutoka kwenye hewa.

Hawa waliitwa kizazi cha nne na hilo likapelekea kutokea kwa familia ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya itherion kwa wingi mno hivyo kuwafanya kuwa na nguvu kuliko wengine wa tabaka hilo na pia kuwa na uwezo zadi kuliko raia wa kawaida.

Yakatengezwa madaraja ambayo yaliwawakilisha watu wenye uwezo wa kutumia itherion. Yalianza na F ambayo iliwakilisha wale wenye uwezo wa chini zaidi ambao hawa walikuwa ni raia wa kawaida.

E iliwawakilisha wale wenye wa juu kidogo kuliko F lakini hawakuwa na uwezo wa kuingia vitani. Hawa wao walikuwa ni kundi lilihusika na marekebisho ya maroboti ya kivita.

D iliwawakilisha wale ambao walikuwa na uwezo wa karibia na kati. Kundi hili lilikuwa la watu waliongia vitani lakini kwa ajili ya kutoa msaada tu.

C iliwawakilisha kundi la wanajeshi wa kawaida, walihusika na kupanda na viumbe wenye uwezo wa chini.

B iliwawakilisha kundi la majenerali, hawa walipambana na viumbe wenye uwezo wa kati.

A iliwawakilisha kundi la makomanda, hawa walikuwa wachache na walikuwa na uwezo wa kupambana na viumbe wenye uwezo wa juu.

S iliwakilisha kundi la asilimia moja tu la binadamu wote, hawa walikuwa na uwezo wa hali ya juu sana na waliweza kupambana na viumbe waliokuwa na uwezo zaidi.

SS, kundi hili lilichangia asilimia sifuri nukta tano ya watu wote duniani, na waliotambulika kuwa katika hili hawakuzidi hata kumi. Ni kundi la watu maalum ambalo halikuwa na mfano wake mpaka wavamizi walikuwa wakiliogopa kundi hili.

Kwa kesi ya Baston, yeye hakuingia katika kundi lolote kati ya hayo nane. Alizaliwa na kutokuwa na uwezo wa kunyonya itherion kabisa. Hivyo kundi la watu kama yeye lilipewa jina la walemavu na uwepo wao haukuwa na tofauti na takataka.

Edward na Shanequeen walikuwa ni daraja A huku Shanequeen akiwa juu kidogo kiuwezo kuliko Edward.

"Ahsante" Baston aliongea na kuvita kitoroli chake nyuma, akapita pembeni na kuelekea ilipo henga namba tano ambako ndipo alipopangiwa kufanya usafi. Katika henga hiyo kulikuwa roboti moja tu ambalo lilikuwa kongwe mno. Pamoja na kutelekezwa huko Baston alihakikisha kila siku analisafisha.

"Fuata upepo, utasafiri katika gharika" ndio maneno yaliokuwa yameandikwa kwenye kifuoa chanroboti huyo. Baada ya usafi, Baston akakaa pembeni ya roboti hilo na kuongea "thamani yako inakuwepo pale unapokuwa na jambo la kuwapa tu" aliongea na kuliangalia.

"Sijui nani alikuwa rubani wako lakini naamini kabisa kipindi chako ulikuwa bingwa" aliendelea na kugusa mkono wa roboti hilo.

"Mpaka sasa nahisi hamu yako ya kuingia vitani", Baston alikuwa akiongea mwenyewe na kufanya kama vile chuma hicho chakavu kilikuwa kinamsikia. "Hata mimi nilikuwa na ndoto ya siku moja kusimama vitani kupigania nchi yangu lakini wachache wakaamua kuwa siwezi kufanya hivyo kutokana na mwili wangu kushindwa kunyonya itherion kutoka katika hewa".

Ghafla kigora kikasikika na taa nyekundu za henga hiyo zikaanza kuwaka, "vikosi vyote katika henga zenu na mjiandae na vita, tunasoma mawimbi ya itherion ya wavamizi" sauti ilisikika kutoka katika speaker maalum ndani ya henga hiyo.

"Wale ambao siyo wanajeshi mnatakiwa kuwa watulivu"

"Vikosi vyote katika henga zenu na mjiandae na vita" kauli hiyo.

"Nichukue vitani, nataka kusimama kwa mara ya mwisho", Baston akasikia sauti lakini eneo hilo alikuwa yeye peke yake na roboti huyo.

"Upweke wangu naona sasa unanifanya kusikia sauti" alijisemea.

"Nichukue vitani, nataka kwenda zangu kama shuja na siyo chuma chakavu" alisikia tena sautu. Alipogeuza uso kuangalia akakutana na macho ya roboti huyo yaakiwa yanawaka taa nyekundu.
_ca2b3fe1-00e3-411e-9792-65c33b1d8d82.jpeg
 
Attachments

  • Screenshot_20231208-180319_Canva.jpg
    Screenshot_20231208-180319_Canva.jpg
    176.4 KB · Views: 17

"Nichukue vitani, nataka kwenda zangu kama shuja na siyo chuma chakavu" alisikia tena sautu. Alipogeuza uso kuangalia akakutana na macho ya roboti huyo yaakiwa yanawaka taa nyekundu. View attachment 2853408
Carry on
 
SEHEMU YA KWANZA: KUKUTANA.
Na Tariq Hajj

To the End (mpaka mwisho) 02

"Naona sasa nimekuwa mwendawazimu" alijisemea Baston, bado macho yake yalikuwa yakiangaliana mashine hiyo ya kivita iliyokuwa imelala hapo kwa zaidi ya miaka mia tatu.

"Nichukue vitani, sehemu yangu ni vitani na sio humu ndani" alisikia tena sauti. Baston akaona isiwe tabu akajifinya ili kujiridhisha kwamba hiyo haikuwa ndoto. Mamumivu aliyoyapata yalilithibitisha hilo.

"Lakini mwili wangu hauna uwezo wa kunyonya itherion kutoka katika hewa. Hata nikitaka kufanya unachotaka sitaweza"

"Mimi nina itherion ya kutosha, nahitaji rubani tu ambae ataniazima nafsi yake" roboti huyo aliongea na sehemu yake ya kifua ikafunguka. Cockpit kubwa ikaonekana, Baston kuona ampeta nafasi ya kuingia katika mashine hiyo ya kivita hakutaka kupoteza. Akapanda na kuingia kisha akakaaa kwenye kiti na kufunga mkanda.

Ile sehemu ya kifua ikajufunga, taa ikawaka ndani na mitambo ikaanza kupata uhai. Ajabu ni kwamba ndani humo hakukuwa na vitufe vyovyote. "Vaa kofia ilokuwepo juu kiti chako".

Baston akaangalia juu kushusha kofia kubwa ya chuma akaivaa. Papo hapo akapitiwa na usingizi mzito.

Synchronization has started, progress 1%....

"Karibu katika Emerald Space, jina langu ni Gilbot" Baston alizinduka baada ya kusikia sauti. Akajikita katika eneo ambalo lilikuwa ni la kijani ya kioo.

"Hapa ni wapi?" aliuliza Baston bado kichwa chake kikiwa na wenge.

"Hapa ni eneo la Emerald, eneo ambalo rubani na mashine wanakutana na kuungana" sauti ilimjibu.

Synchronization has started, progress 10%....

"Mbona sikuoni" aliongea tena Baston akiamgalia kushoto na kulia ila bado hakuona mtu. "Usihangaike sana mpambanaji kijana, muunganiko ukikamilika mwa asilimia moja utajua kila kitu" sauti ilimjibu.

**********

Henga namba moja.

"Captain wote tupo tayari" aliomgea kijana mmoja.

"Kumbukeni maisha yako ni muhimu, urakapohisi kuendelea kupambana hakuna maana rudi nyuma" aliongea Shanequeen ambae ndie nahodha wa kikosi cha vijana henga namba moja. Kikosi chake chote kilihusisha wataalamu wa masafar marefy hivyo maroboti yao yote yalikuwa na bastola.

Geti kubwa likafunguka na kwa kutumia reli maalumu, maroboti haya yakatoka kwa kasi na kutua nje ya ukuta mkubwa uliotengenezwa kuzuiia wavamizi.

"Wanajeshi wote, kitisho kilicho mbele yenu ni daraja la kadet. Kuweni makini huenda kukawa kitisho daraja la sajenti kati yao.

Kikosi kilichokuwa chini ya Shanequeen kilikuwa na watu kumi ambao wote walikuwa ni long ranger Fighters (LRF). Kati yao, ni Shanequeen peke yake aliekuwa na uwezo wa kufanya mashambulizi masafa marefu zaidi. Na kutokana na daraja lake kuwa ni daraja A, hivyo hata roboti lake lilikuwa na uwezo zaiidi kuliko mengine katika kikosi chake.

Henga namba mbili.

Kikosi cha vijana katika henga hiyo kilikuwa chini ya Edward, wao walihusika zaidi na silaha nzito hivyo kuwafanya kuwa washambulizi masafa ya karibu. Isipokuwa mmoja ndanj ya kikosi hicho alikuwa ni mshambuliaji wa masafa marefu na alijulikana kama mdunguaji hatari zaidi. Uwezo wake wa kudhibiti silaha kubwa ya masafa marefu ulizidi mpaka uwezo wa Shanequeen.

"Micky, ukipata nafasi nataka umuondoe Shanequeen kwenye mchezo. Usimuue, hakikisha tu unamjeruhi kiasi cha kushindwa kuendelea kushiriki katika hii vita ya leo. Ukifanikiwa kufanya hivyo nitakupa chupa mbili za kemikali ya itherion busta za kiwango cha hali ya juu. Nina uhakika ukizitumia uwezo utaongezeka na kufika daraja A" aliongea Edward.

"Ukifanikiwa pia nitatumia njia ninazozijua kuhakikisha unakuwa nahodha wa kikosi cha vijana henga namba moja" akamalizia na kuondoka bila kuruhusu kujibiwa.

Kikosi kutoka henga namba mbili kikawasili uwanjani dakika tano baada ya kikosi cha Shanequeen na kuunga mpambano.

Kikosi cha Shanequeen kilifanya kwa kasi na umakini wa hali ya juu katika kupunguza idadi ya wavamizi. Wepesi wao ulikuwa ukiendelea kuwashangaza raia wa kawaida waliokuwa wakishuhudoa pambano hilo kupitia runinga maalum ndani mji huwo.

"Edward, mimi na kikosi changu tutawafungulia. Wewe na kikosi chake itumieni nafasi hiyo kusogea karibu ili kuvunja ukuta wao wa kwanza wa ulinzi.

Wakati huwo huwo Micky alikuwa juu ya ukuta mkubwa mbali sana na uwanja vuta. Bunduki yake kubwa yenye urefu wa mita kumi na tano na upana wa mita tano ilikiwa imeelekea uwanjani. Lakini mlengwa wake hakuwa adui wa binadamu bali Shanequeen ambae hakuwa akijua nini kinaendelea.

Mucky hakuwa mtu mjinga jinga, alikuwa ni kijana mjanja sana. Alijua kabisa kwake huwo ulikuwa mtego, kama ingetokea wadadisi na wachunguzi wangegundua kuhusika kwake kwa makusudi bali kifungo kingemuhusu. Hivyo akawa anapiga hesabu nyingi na kuchora matokeo kedekede.

Baada ya vurugu za dakika moja hatimae Shanequeen akatengeneza nafasi iliyomfanya Edward na kikosi chake kufanikiwa kuvunja safu ya ulinzi ya maadui zao.

Shanequeen akasogea pembeni kidogo kutafuta pembe nzuri ya kufanya shambulizi. Loh! Wakati huwo huwo risasi iliyosafiri kwa kasi mno kutoka kwa Micky ikatengenesha kuanzia bunduki, bega na mkono mzima wa roboti la Shanequeen.

"Miss shot" bila kuchelewa Micky akaripoti akibadilisha nafasi na kabla hajakaa sawa akaachia risasi nyingine iliyopita pembeni kama nusu mita hivi kutoka kwa Shanequeen na kuzama katika kichwa ch adui zao.

Hilo likatoa taswira ya moja kwa moja kuwa Shanequeen alokuwa katika mstari wa mashambulizi. Hivyo ikahesabika kama ajali kazini.

Ndani ya roboti Shanequeen taa nyekundu ilikuwa ikiwaka, kompyuta ikaonesha kiwango cha uharibifu uliyotokea. Kilikuwa ni asilimia sitini na moja, namba hiyo iliashiria kwamba mashine hiyo haikuwa na uwezo wa kuendelea na vita.

"Purple Butterfly, rudi nyuma. Umepata jeraha kubwa hivyo ofisi ya amri imejiridhisha huezi kuendelea na vita" amri ilitoka kutoka makao makuu.

"Affirmative" Shanequeen aliitika na kugeuza roboti lake kwa ajili ya kurudi nyuma. Hatua ya kwanza, hatua ya pili mara king'ora kikali sana kikasikika kuashiria hatari imeongezeka.

"Kitisho daraja la sajenti kimehisiwa, vikosi vyote mnatakiwa kirudi nyuma" amri ikatoka. Shanequeen alipoangalia akagundua kuwa kuna baadhi yao wasingeweza kufanya hivyo.

Purple butterfly likadondokea mikono na kuwa kamam mnyama wa moguu minne. Vyuma kadhaa vikatoka na kujikita ardhini. Sehemu ya mgongo ikafunguka na bunduki yenye bomba ndefu ikatoka na kukunjuka. Ilikuwa na urefu wa mita ishirini na tano.

"Rubani wa purple butterfly ukifanya hilo shambulizi, chaji ya mashine yako itaisha kabisa" alisikia sauti.

"Shambulio hili moja lina uwezo wa kuokoa maisha ya wote waliokuwa mstari wa mbele. Hivyo naomba ruhusa ya kufanya shambulizi" aliongea Shanequeen huku bunduki hiyo ikijichaji tayari kwa kufanya shambulizi.

"Una maneno yeyote ya mwisho, huenda ikawa tamati yako"

"Waambieni wazazi wangu, binti yao amekwenda kifua mble. Bila kafara hakuna ushindi"

Fully charged! Sauti ya mashine ikasikika.

Fyum!

Risasi ikafyetuka kutoka kwenye bomba hiyo na kusafiri kwa kasi mno na kutandika ngao ya mvamizi.

Power 2%.

Alipoangalia sehemu ya betri akakuta kuwa chaji ilikuwa imebakia kidogo mno. "Umefanya vyema Purple butterfly" aliongea Shanequeen.

****

Synchronization has started, progress 99%.
 
SEHEMU YA PILI: IMANI ISIYOTIKISIKA.
To the end (mpaka mwisho) 03

Synchronization complete, System rebooting.

Ghafla Baston akapatwa na kiza, kilipoondoka akashangaa kujikuta ndani ya henga namba tano. Ghafla akaanza kuona taarifa za vitu mbali mbali vilivyokuwemo humo. Akainua mkono kutaka kuangalia saa akashangaa kuona mkono wake ulikuwa wa chuma.

"Knowledge transfer has started, progress 1%" akasikia sauti na ghafla ubongo wake ukaanza kupokea taarifa za ajabu. Taarifa hizo zilikusanya mifumo mbali mbali ya kivita, taaluma juu ya mashine hiyo na jinsi ya kuitumia. Aina mbali mbali za kombat ambazo zilitumika na mashine hiyo.

"Knowledge transfer, complete" akasikia tena sauti ila safari hii hakushangaa sana. Alijikuta akiwa tulivu kama vile veterani wa kivita.

"Gilbot angalia kama kila kitu kiko sawa" alioangea sauti nzito.

"Kila kitu kipo sawa" Gilbot alijibu.

"Chaji iko asilimia ngapi?"

"Sitini"

Baston akatabasamu na kusimama, roboti hilo nalo likasimama. Mwanzo alipata shida kidogo kutembea lakini baada ya dakika moja akawa tayari ameshazoea.

Akatembea mpaka sehemu ambayo ilikuwa na vutufe vitatu. Akabonyeza cha kijana na sehemu ya juu ya henga hiyo ikafunguka. Moshi laini ukaanza kutoka katika nyayo za mashine hiyo kubwa yenye urefu wa takriban mita hamsini.

************

"Captain, twende" aliongea mmoja kati ya wa wafuasi wake, "nendeni mashine yangu imekata moto kabisa" alijibu Shanequeen kwa tabu. Hata kupumua kwake ilikuwa ni mzigo kutokana mashine hiyo kushindwa kuingiza na kutoa hewa ndani humo.

Edward alikuwa ni miongoni mwa wa mwisho kurudi nyuma. Alipokaribia alipokuwa purple butterfly akapunguza mwendo "ni jambo baya sana unakufa na utamu wako, ungenikubali leo usingekuwa katika hali hiyo" alijisemea na kuachia tabasamu la kejeli kabla ya kuongeza kasi.

Zeatra, jina ambalo walipewa wavamizi na binadamu baada ya shambulio lile kutoka purple butterfly akaweweseka na kukaa sawa. Sehemu ya kifua ya kiumbe huyo ikaanza kunyumbuka na kuwa bomba la bunduki.

Baada ya sekunde kadhaa muonzi wa kijani ukatoka kwa kasi na kuelekea Purple butterfly. Japo Shanequeen alishajitolea kufa lakini bado moyoni alikuwa anaomba muujiza utokee.

Peeeeeng!!

Sauti kali ya kugongana kwa kitu ikasikika na kusababisha vumbi nyingi. Mbele ya Purple butterfly kulikuwa na kivuli kikubwa kilichokuwa kimesimama kama kisiki cha mti mnene.

"Bado aliekuwepo ndani ni mzima" Gilbot akatoa taarifa, Baston akageuka na kushika sehemu ya kifua ya purple butterfly na kuinyofoa.

Koh! Koh! Koh!

Shanequeen akakohoa baada ya kupata hewa nyingi, macho yake yalikuwa yameganda kwa roboti kubwa la rangi ya kahawia yenye mabaka mabaka kijani iliyopauka.

"Umefanya vyema" aliongea Baston, Gilbot akashika mipini miwili na kutoa visu virefu vye urefu wa mita sita. Akaanza kukimbia kuelekea alipo Zestra katika mstari uliyonyooka. Alijua kutoka katika mstari kungemuweka Shanequeen katika hatari hivyo alitumia visu vyake kupanga mionzi yotw iliyotoka kwa adui yake.

Wakati huwo huwo, zestra wa daraja la kadet wakaanza kukimbia kuelekea anapotokea Gilbot. Bila ya kujua kuwa walikuwa kama swala waliokuwa wakikimbilia katika moto kwa sababu tu waliona muangaza.

Na kwa sababu Baston hakuwa na uwezo mkubwa wa kuimudu mashine alifanya kazi ndogo sana. Mashambulizi yote yalifanywa na Gilbot mwenyewe.

Power 40%

Chaji ya mashine hiyo ilikuqa inapungua kwa kasi na mpaka purukushani na Zestra wa daraja la kadet inasiha. Chaji ilikuwa ni asilimia ishirini na tano tu na alikuwa amebakia Zestra wa daraja la sajent ambae alikuwa na uwezo mara nne zaidi ya wale wengine.

"Baston nasikitika kuwa sitaweza kummaliza huyo" aliongea Gilbot.

"Ulinambia nikuchukue vitani kwa mara ya mwisho, huna haja ya kuhifadhi kitu. Weka kila kitu katika shambulio moja tu na mimi nitakupeleka katika ushindi wako wa mwisho" aliongea Baston.

"Imekuwa ni faraja kwangu kusimama na wewe vitani japo ni mara moja. Natamani ningeendelea lakini wakati wangu ulishapita miaka mia tatu nyuma" aliongea Gilbot. Sehemu ya mgongoni ikafunguka, mpini mkubwa ukaonekana.

Akashika na kichomoa upanga mkubwa uliekaribiana na urefu wake. Macho ya mashine hiyo yakabadilika rangi na kuwa menkundu. Mashine ikanguruma na kutoa moshi mweusi. Mngurumo huwo ulisababisha mpaka aedhi kutikisika.

"To the end" aliongea Gilbot

"To the end" nae Baston akajibu

Kiwango cha itherion kilichokuwa kikiingia katika mashine hiyo kupitia kwa Baston kilikuwa ni kikubwa kuwahi kusomeka.

Gilbot na Zestra walibadilisha shambulizi moja tu na baada ya hapo Gilbot akazungusha upanga wake na kuuchomeka ardhini.

"Kwa heri komredi" aliongea

"Umefanya vyema Gilbot" ghafla Baston akazinduka kutoka usingizini. Alihisi mwili wake wote ukiuma kama kidonda.

Booom!!

Mlipuko mkubwa ukasikika baada ya Zestra kusambaratika. Walioshuhudia pambano hilo waliamini mungu alikuwa amewabariki kwa kuwashukia katika nyakati ngumu.

Sekunde chache baadaw ndege sita zikamzunguka Gilbot.

"Rubani wa mashine isiyotambulika, tafadhali zima mashine yako na utoke" ilisikika sauti kutoka katika moja ya ndege hizo. Baston hakuona haja ya kujibishana nao, akabonyeza sehemu na kifua cha roboti huyo kikafunguka.

Akatanguliza mikono juu akionesha kusalimu amri, akakanyaga sehemu na kushushwa mpaka chini. Akasimama pembeni ya roboti hilo na kuliangalia kwa mara mwisho.

"Pumzila Gilbot" yalikuwa maneno ya mwishonya Baston na papo hapo mashine iliyokuwa inanguruma katila roboti hilo ikazimika na taratibu Gilbot akaanza kusambaratika na kupotelea katika upepo. Upanga wake mkubwa tu ndio uliokuwa umebakia umesimama.

Ndege zile zikatua na wanajeshi kadhaa wakashuka na kumzunguka Baston huku mitutu yao ikiwa imeelekea kichwani kwake. Akapita mmoja na kumshika Baston mikono, akamvalisha pingu na kumuamuru asimame.

"Kuanzia sasa utakachokisema aidha kitatumika kwa ajili yako au dhidi yako, hivyo nakushauri ukae kimya" aliongea mwanajeshi akimsindikiza Baston katika ndege moja wapo. Baada ya zoezi hilo kukamilika, ndege zote zikapaa na kuelekea ndani ya mji.

"Baston" huku macho yakiwa yamekodoka, Shanequeen akajikuta akilitaja jina hilo baada ya kumuona rubani alieshuka kwete roboti lililosambaratika upeponi.

"Captain" alisikia sauti ikitokea nyuma, alipogeuka akakiona kikosi chake kikirudi.

"Hujaumia popote" wote waliongea kwa wakati mmoja wakishuka kutoka maroboti yao. Shanequeen akawaangalia na kuachia kabla ya kuachia tabasamu na kupoteza fahamu. Mambo yaliyotokea siku hiyo, ukichanganya na ukaribu wake na kifo kilichomkosa wakati huwo. Akili yake ilizidiwa na kushindwa kuratibu mambo yote hayo kwa wakati mfupi.

Ndege sita za kijeshi zinatua nje ya jengo kubwa katika kiwanja maalum. Wanatangulia wanajeshi kadhaa, nyuma yao anafuata Baston ambae yupo katika pingu. Wakaingia ndani ya jengo hilo na moja kwa moja akapelekwa katika lifti, ikaanza kushuka chini.

Iliposimama na kufunguka wakatoka na kuelekea katika chumba kimoja. Kikafunguliwa na Baston akafunguliwa pingu na kupewa amri ya kuingia katika chumba hicho kisha mlango ukafungwa.

*************
_e107d4eb-81cc-4f71-a6b7-ca995e0031e1.jpeg
 
SEHEMU YA TATU: SHUJAA.

To thee end (mpaka mwisho) 04

Tariq Haji

0624065911

Shanequeen anafumbua macho na kujikuta hospitali, alipojaribu kukaa akazuia na mtu aliekuwa pembeni.

"Mama" aliita.

"Endelea kupumzika" aliongea mwanamke mtu mzima kiasi, ila katika sauti yake kulionekana kuna hali fulani ya majonzi.

"Mama, mbona unaonekana una majonzi sana" ilibidi Shanequeen aulize.

"Tutaongea ukitoka hospitali" aliongea mama ake na kuinuka, akatoka nje na kuufunga mlango kisha akuegemea. Taratibu machozi yakatengeza michirizi mashavuni mwake.

"Usilie, mtoto wetu ni jasiri sana ila kuna mambo huwa no nje ya uwezo wetu" aliongea mwanaume mtu mzima akijaribu kumbebembeleza mkewe.

"Wewe nenda nyumbani, mimi nitakaa nae" aliongea na kuwapa ishara walinzi waondoke nae. Baada ya mama huyo kuondoma, mzee Rozaliv baba mzazi wa Shanequeen akafungua mlango na kuingia ndani.

Shanequeen alikuwa amekaa kitako kitandani akiangalia nje kupitia dirisha kubwa.

"Baba" aliita baasa ya kumuona baba ake akiingia ndani ya chumba.

"Unaendeleaje"

"Nahisi uchovu tu, ila sina shida nyingine yeyote" alijibu.

"Hito ni dalili nzuri ya kupona" aliongea mzee huyo.

"Baba kuna nini? Mama ametoka hapa akionesga kuwa na huzuni sana" aliuliza Shanequeen. Mzee Rozaliv akavuta kiti na kukaa kisha akamshika binti yake mkono.

"Nashukuru Mungu angalau hali yaki imetengemaa lakini kuna habari mbaya, unataka kuzijua"

"Ndio"

"Ni kweli umesalimika lakini mwili wako umepoteza uwezo wa kunyonya na kuhifadhi itherion. Chombo chako cha kuhifadhia itherion kimesambaratika" alipngea mzee huyo.

"Oh! Hiyo ni bahati mbaya sana kwangu" aliongea na kujitahidi machozi yasimtoke lakini hisia za uchungu zikamsaliti.

"Bora uhai mwangu, kupoteza uwezo wa kunyonya na kuhidhadho itherion siyo mwisho wa maisha. Kuna mambo mengine mengi tu ya kufanya ukiachia kuwa mwanajeshi" aliongea mzee huyo.

"Naelewa" aliitika Shanequeen, moyoni alikuwa na majonzi makubwa sana. Yeye ndie aliekuwa mtoto wa pekee katika familia na amezaliwa wazazi wake wakiwa katika umri mkubwa. Si hilo tu, amepatikana baada ya majaribio kadhaa. Kwa baba ake alikuwa tumaini pekee la kuiendeleza historia ya familia yake ila sasa amekuwa mlemavu.

"Vipi kuhusu Baston" aliuliza

"Unakusudia yule kijana alieingia vitani na roboti ambalo halikuwa limesajiliwa"

"Ndio"

"Serekali imeamua kuwa atahukumiwa na mahakama ya kijeshi" aliongea Mzee Rozaliv

"Lini"

"Leo mchana"

"Naweza kuhudhuria kipindi atalachokuwa anasiliza mashtaka yake"

"Kwanini"

"Kuna jambo tu nataka nithibitishe"

"Sawa nitafanya mpango uletwe mahakama kuu ya kijeshi ila usine ukafanya kitu chochote kwa sababu haki zako za kijeshi zimezuiliwa" aliongea mzee Rozaliv.

"Usijali, sitafanya kitu nataka tu niwepo wakati wa hukumu"

*********

Mahakama ilikuwa imejaa watu wenyw vyeo mbali mbali, wengi walikuwa hapo kushuhudia hukumu ya kijeshi ambayo ilisifika kuwa ni ya kikatili zaidi kuliko hukumu ya mahakama ya kawaida.

Sheria za mahakama hiyo zilimtaka mshtakiwa apande kizimbani na kujibu mashtaka yake. Sheria hazikumruhusu mshtakiwa kuwa na wakili.

Mlango mdogo ulifunguliwa, Baston akatangulia akiwa na pingu mikononi. Baada kupanda kizimbani zikafunguliwa na mikono yake kuwa huru. Minong'onk ya hapa na pale ikasikika, watu walikuwa wakimnyooshea vidole.

Order!!

Sauti kali ikasikika na mlango mwengine mdogo ukafunguliwa, wakaingia watu watano wakiwa katika magwanda ya kijeshi. Wakakaa kwenge viti nyuma ya meza kubwa. Baada ya taratibu za mwanzo pamoja na kuapishwa hatimae kesi ikaanza kusikilizwa.

"Jina lako ni Baston"

"Ndio"

"Miaka kumi na tisa"

"Ndio"

"Kutokana na taarifa zako zilizokuwepo kwente kanzidata ya jeshi, zinaonesha wewe ni mlemavu. Mwili wako hauna uwezo wa kunyonya wala kuhifadhi itherion, kweli au si kweli"

"Ni kweli" alijibu Baston, hakuonesha wasiwasi wowote ule.

"Baston, unajua kufanya udanganyifu wowote ule katika jeshi ni kosa la jinai"

"Najua"

"Kama taarifa zako ziko sahihi, tunataka kufahamu umewezaje kuendesha roboti ambalo lilikuwa henga namba tano"

"Kabla sijajibu swali ningependa kujua haki zangu na fungu langu kutokana na msaada niliyotoa"

"Eti" mwingine kati ya wale watano aliongea na kupiga meza.

"Usifoke, rudia sehemu ya tano ya katiba ya jesh, kifungu cha sheria namba xx234 kifungu kidogo xx234a kinasemaje" aliongea Baston.

"Kij... "

"Court Marshal Gel" yule mzee aliefoka mara ya kwanza alitaka kuongea tena lakini akakatizwa kwa sauti nzito.

"Samahani" aliomba msamaha na kujiinamia.

"Sehemu ya tatu ya katiba ta jeshi, kifungu xx234, kifungu kidogo xx234a kinasema" alianza kuongea Court Marsha Sal. "Mshtakiwa ambae amefanya makosa ya kijeshi lakini katika makosa hilo akasababisha nchi kuepuka majanga, atapewa nafasi tano za upendeleo kuomba chochote na jeshi litamtimizia. Ila nafasi hizo hazitafanya kazi ikiwa mshtakiwa atataka kuzitumia kubadilisha adhabu" alimalizia.

"Baston umesikia haki yako" aliongea aliongea aliekuwa akiendesha keshi hiyo.

"Ndio na naomba nitumie nafasi mbili kati ya hizo kufanya maombi yangu"

"Umeruhusiwa"

"Naomba nitumie henga namba tano kwa maswala ya kijeshi"

"La pili naomba aliekuwa Squad leader (SL) wa henga namba moja, SL Shanequeen arudishwe jeshini na ahudumu katika henga namba 5 kama mwanajeshi wa kawaida" aliongea.

Mahakama nzima ikazizima, wengi wakabaki na mshangao. Alikuwa anasema nini huyu mwehu, hapo alipo alikuwa anasubiri hukumu ambayo isingepungua miaka mitano katika migodi ya mawe angani.

"Gruntes" Court Marsha Pit aliongea na kugonga nyundo.

"Sasa ningependa kujua fungu langu endapo nitatoa taarifa muhimu" aliongea Baston. Utulivu wake uliwatisha wengi, kumi na tisa lakini alikuwa na miaka wa kiwango cha Admiral jeshi.

Zzzzz!!

Kimyabm kikatawala, watu hawakuelewa nini kinaendelea. Wengi walikuwa hapo kushuhudia nguvu ya mahakama ya kijeshi kutokana na kuwa ni muda mrefu sana haikuwa kazini. Lakini sasa ofisi kama mahakama inahukumiwa na Baston.

"Kifungu xx120, kifungu kidogo xx120c kinasema, ikiwa mtuhumiwa atatoa taarifa muhimu na zana msaada basi atasamehewa makosa yake yote. Isipokuwa atavuliwa vyeo vyote vya kijeshi na kurudi kuwa mwanajeshi wa kawaida"

"Endelea" aliongea Court Marshal Shimo.

"Nina taarifa mbili muhimu sana na nina imani zitasaidia jeshi kuchukua hatua moja mbele"

"Ya kwanza ni lengo na shambulizi la kukusudia dhidi ya SL Shanequeen wakati vita ikiendele" aliongea.

"Unataka kusema wapelelezi wa kijesh wamekosea katika taarifa yao" Court Marshal Gel alifoka.

"Baston tambua kwamba kila kitakachotoka mdomoni mwako kitatumika kwa ajili au dhidi yako" aliongea Court Marshal (CM) Pit.

"Natambua na napenda kuendelea na kile nilichokisema mwanzo"

"Endelea"

"Ningependa ubao kuelezea kilichotokea"

"Umeruhusiwa"

Baston amatoka kizimbani na kwenda ulipo ubao, akachukuwa kalamu na kuanza kuchora kitu. Kadri muda ulivyokwenda ndivyo maajabu yalivyoongezeka. Baston aliuchora uwanja wa vita kama ulivyo.

"Hapa ndipo alipokuwa mdunguaji wa henga namba mbili (akionesha kwa kidole), na roboti alilokuwa anatumia ni Midas73 type V. Umbali ambao wanaweza kupiga bila makosa ni mita elfu tatu na inabeba risasi za kawaida" aliongea Baston.

"Mahakama haina muda wa kusikiliza porojo zako" aliongea CM Gel.

"Risasi za kawaida haziwezi kupenya ukuta wa sumaku uliozunguka roboti zetu na kutumia risasi za itherion kupitia amri maalum kutoka juu. Je nahitaji kuendelea?" aliuliza Baston.

"Umesema una mambo mawili, tuambie la pili" aliongea CM Shimo.

"Sidhani kama ni sahihi kulisema katika umati huu" aliongea Baston. Majaji watano wakaangaliana na kupeana ishara fulani kisha mmoja wap akainuka.

"Tunaomba watu wote watoke nje, atabakia mtuhumiwa na sisi majaji tu" aliongea CM Phil. Baada ya amri hiyo kutoka, watu wote wakatoka nje ya mahakama na milango ikafungwa.

"Baston, endelea"

"Baada ya kushuhudia vita ya juzi, nimegundua mapungufu katika roboti zetu" aliongea na kushika kalamu akaanza ubaoni.

***********
 
***********

SEHEMU YA NNE: PRODIGY

To the end (mpaka mwisho) 05

Tariq Haji

0624065911

Mlango wa mahakama ulifungulinguwa, Baston anatoka akiwa mtu huru kabisa. Watu wote waliofika hapo kushuhudia akichezea kifungo wakabaki wametoa macho. Wakati huwo Shanequeen alikuwa mbali kidogo na umati wa watu.

Baston hakushughulika na watu wengine, moja kwa moja alienda mpaka alipo binto huyo na babaake.

"Vice Squad Leader (VSL) nategemea baada ya mapumziko utarudi kambini. Nitakuwa nakusubiri" aliongea akimuangalia Shanequeen machoni.

"Lakini binti yangu hawezi kutumia miguu yake mpaka sasa"

"Mr Rozaliv, Shanequeen hana tatizo lolote. Kesho mlete henga namba tano utashuhudia hichi ninachokwambia" aliongea Baston na kuondoka.

Saharan Empire ni moja kati ya nchi kubwa tatu katika bara la Yurasia. Baada ya Zestra kuvamia nchi nyingi duniani ziliangamia na kusababisha dunia kugawanyika katika mabara makuu manne badala ya saba yaliyokuwepo mwanzo.

Bara Amerika likapewa jina Ingrasia, bara Yuropa (Europe) likaitwa Perasia, bara asia likaitwa Nerasia na bara Afrika likaitwa Yurasia.

Bara la Yurasia lilikuwa na ngome kubwa tatu ambazo zilikuwa ni ngome ya kaskazini ambayo iliitwa Sahara Empire, ngome ya Yurasia ya kati ambayo iliitwa Victorian Empire na ngome ya kusini ambayo iliitwa Soweto Empire.

Ngome ya Sahara ilikuwa imegawanyika katika sehemu tano, sehemu hizo zilifanya kama vile kuta za ulinzi japo kulikuwa na makazi ya watu. Pia sehemu hizo zilikuwa vigawanyishi asili kwa matabaka ya watu.

Baina ya ukuta namba tano na nne, yalikuwa ni makazi ya watu wa kawaida. Hili lilikuwa kundi la wafanya kazi wa chini kabisa ambao walihusika na ukulima na ufugaji. Baina ya ukuta namba nne na tatu kulikuwa na kundi jingine la wafanya kazi. Hawa wao walikuwa ni wafanya biashara wadogo wadogo, walihusika na ununuzi wa bidhaa kutoka mji wa tano na kuuaza kwa wale wa mji watatu.

Baina ya namba tatu na mbili lilikuwa sehemu ya viwanda, na hili ndio lilikuwa eneo kubwa zaidi. Vitu vingi vilitengenezwa katika eneo hili isipokuwa vya kijeshi tu. Kati ya namba mbili na namba moja lilikuwa eneo la kijeshi. Eneo hili lilihusika na utenegenezaji wa silaha, ndege pamoja na maroboti yaliyotumika kupambana na Zestra. Pia eneo hili lilikuwa na shule nyingi za kijeshi kwa ajili ya mafunzo.

Katika eneo namba moja ndio kulikuwa na mji mkuu, katika eneo hilo ndio kulikuwa na qasri la kifalme la nchi ya Sahara. Pia waliishi watu wa tabaka la juu zaidi, watu waliokuwa na uwezo mkubwa kimali na kiwadhifa.

***********

Henga 5.

"Karibu" aliongea Baston akimpokea Shanequeen kutoka kwa baba ake.

"Ahsante" aliitika binti huyo, baada ya salamu na maongezi kidogo, Mzee Rozaliv akaaga na kuondoka akiwaacha Baston na Shanequeen wakiwa na maongezi yao. "Umejaribu kutembea?" aliongea Baston

"Siihisi miguu yangu kabisa"

"Umejaribu kuhisi itherion"

"Nimejaribu lakini sijafanikiwa, najua unataka kunisaidia lakini nilipofika sasa sidhani kama kuna msaada wowote" alinung'unika Shanequeen.

"Mara ya mwisho ulipofanya lile shambulizi ulivuja mipaka yako na kusababisha chupa ya kuhifadhia itherion katika mwili wako kupasuka. Kawaida chupa hiyo ikipasuka huchukuwa muda mpaka kujijenga upya na inakuwa kubwa zaidi. Sasa kuanzia leo unatakiwa ujaribu kuhusi itherion katika hewa mpaka pale utakapofanikiwa. Ukifanikiwa kufanya hivyo mwili wako utajijenga upya na shida zote zitajirekebisha" aliongea na kufafanua Baston.

"Una uhakika gani kuhusu hilo, hakuna kitu kama hicho katika vitabu vyote nilivyowahi kusoma"

"Nilipokuwa mdogo na mimi yalinikuta kama yaliokukuta wewe. Niliusukuma mwili wangu kupita mipaka yake na kusababisha chupa kupasuka, kwasababu nilikuwa sijui nikaishia kuwa mlemavu mpaka siku ya ile ya vita. Ndio nikapata taaluma ya uwepo wa kitu kama hicho, mwili wangu umejirekebisha na sasa nina uwezo wa kuhisi na kunyonya itherion kutoka katika hewa"

"Umejuaje?"

"Hiyo ni siri nitakwambia siku nyingine, kwasasa anza kufanya nilivyokwambia". Shanequeen akafumba macho na kuanza kufanya kama alivyoelekezwa. Wakati yeye akiendelea kufanya hivyo, Baston akatandika karatasi kubwa mezani na kuanza kuchora roboti. Kila mmoja alifanya kazi yake mpaka jua lilipozama, mzee Rozalive akafika na kumchukuwa Shanequeen.

Siku iliyofuata mapema Shanequeen alifika na kuendelea na kazi ya jana yake. Aliendelea kufanya kila siku bila kulalamika, hata kama moyoni mwake hakuwa na imani tena ya kupona lakini aliamini katika kujaribu.

Siku saba zimepita.

Akiwa kafumba macho ghafla akaanza kuhisi hali ya ubaridi ikiingia mwilini mwake. Taratibu akafumbua macho na kukutana na mionzi ya rangi mbali mbali ikiingia mwilini mwake kwa kasi mno.

"Baston naona mionzi ya ajabu" aliongea.

"Unachokiona sasa ni nguvu ya cosmic (cosmic energy), hiyo ni nguvu ya asili inayozaliwa na mazingira. Nguvu ya cosmic ndio sisi tunaita punje punje za itherion" alifafanua.

Akafumba macho na kuendelea kunyonya mionzi hiyo iliyozidi kuingia mwilini mwake kwa kasi. Taratibu misuli yake ya miguu ambayo tayari ilishaanza kusinyaa ikaanza kutanuja na kuwa inadunda kama misuli ya moyo. Mishipa ya damu na ya fahamu iliyokuwa imepoteza uwezo wa kufanya kazi ikaanza kukuwa na kuunga upya.

Mwili wake mzima ukaanza kupitia mabadiliko ambayo hata yeye mwenyewe hakuwa akiyaelewa. Baada ya kuwa katika hali ya ukimya tulivu kwa zaidi ya saa tatu, hatimaye akafumbua macho na kusimama. Kutokana na kukaa kwa muda mrefu akajikuta akiyumba na kutaka kuanguka.

Baston akamuwahi na kumshika kiunoni japo halikuwa kusudio lake kufanya hivyo. "Taratibu kila kitu kinakwenda kwa wakati wake" aliongea akimrudisha kwenye kiti. Shanequeen kutokana na aibu akajikuta akikosa la kuongea.

"Kwasasa usimwambie mtu kuhusu hili, endelea kuishi kama miguu yako haifanyi kazi" aliongea Baston.

Shanequeen akatikisa kichwa tu huku akiangalia chini. Jioni ilifika na baba yake akafika kumchukuwa.

"Mzee Rozalive tunaweza kuongea kidogo" aliongea Baston.

"Sawa, Shanequeen nisubiri hapo nje" alijibu.

"Kuna jambo gani?"

"Nina wazo, nina uhakika litakuwa na faida zaidi kwako kuliko kwangu"

"Usizunguke mbuyu"

Baston akatabasamu na kuongea "Nina dizaini chache za maroboti ya kivita, ila ni wewe pekee ninaekuamini.

Unaonaje tukaingia makubaliano kwamba nikukabidhi tenda hiyo".

"Mimi nitapata nini katika tenda hiyo"

"Nitakukabidhi hati miliki ya dizaini chache zitakuwa zako na ukiwa utakubali kufanya biashara nitakukabidhi asilimia arobaini na tisa ya hisa zote"

"Unafahamu kama familia yangu imekuwa katika kazi ya kusambaza na kutumia roboti za kivita kwa miaka mingi mno. Dizaini zina kitu kipya ambacho kitanifanya niweze kuwashawishi wazee wa ukoo"

"Hujawahi kuziona, kwa leo tuishie hapa. Nenda kafikirie tutaongea vizuri kesho" aliongea Baston na kutabasamu. Mzee Rozalive alikuwa ni mfanya biashara na popote pale kwenye pesa zake zilifanya kazi vyema mno. Akaagana na Baston na kuondoka.

Kivumbi kinaanzaaa huku yaan movie inaanza upyaaa🤌
 
SEHEMU YA TANO: NGUVU YA COSMIC

To the end (mpaka mwisho) 06

Tariq Haji

0624065911

Siku ya pilu mapema, Shanequeen aliletwa. Baada ya baba ake kuondoka akasimama na kukisogeza kiti pembeni. Usoni mwake tabasamu kubwa lilikuwa limechanua.

"Unajisikiaje baada ya kuweza kutembea tena" aliongea Baston, macho yake yalikuwa yamepiga weusi. Ni wazi hakuwa amelala kwa muda mrefu.

"Unaonekana umechoka sana, kwanini usipumzike" aluongea Shanequeen akimuangalia Baston ambae hata sura yake tu ilionekana kujaa uchovu.

"Usijali, kwanza twendw huku ukaone kitu" aliongea akimfanyia ishara ya kumfuata. Shanequeen hakutaka kuuliza ni kitu gani, aliunga na kuelekea katika chumba kidogo kilichokuwepo sehemu hiyo. Ndani ya chumba hicho kulikuwa vitu viwili vilivyofunukwa na mashuka mawili tofauti.

"Shanequeen wewe ni mpambanaji mzuri, ila umekosa roboti ambayo ingeuwanika uwezo wako wote hewani. Ninachokwenda kukuonemesha si kitu halisi bali ni frame tu ya kitu chenyewe" aliongea maneno hayo na kuvuta shuka moja.

"Nakuletea mbele yako Golden Raven Basic Version" aliongea. Shanequeen akakodoa macho asiamini macho yake, lilikuwa ni roboti kubwa la plastiki. Kila mkono lilikuwa limeshika bastola ndogo na mgongoni kulikuwa bunduki kubwa iliyotokea kwa juu.

"Ikiwa roboti hili litatengenezwa kwa vile maelezo yangu yalivyo, basi litakuwa na uwezo wa kufanya kile ambacho maroboti yote ya mwanzo yalishindwa kufanya" alifafanua.

"Ni zuri mno, nina imani likishatengezwa litakuwa zuri zaidi. Vipi kuhusu hili shuka la pili" aliongea Shanequeen akivuta shuka. Kwa sekunde chache akatulia kwanza akiangalia roboti hilo la plastiki. Ilikuwa ni kitu ambacho hajawahi kukiona katika maisha yake.

Kilicho mstaajabisha zaidi ni kwamba, roboti hilo halikuwa na silaha ya masafa marefu hata moja. Mkononi lilikuwa na visu viwili vikubwa. Na mgongoni kulikuwa na visu vingine vinne pamoja na panga kubwa.

"Tempest Dragon Basic Version, ni mpambanaji wa ana kwa ana na roboti ambalo nitakuwa natumia mimi" aliongea Baston. Miaka mingi baadae Fleet Vice Admiral Shanequeen ataandika kwenye kitabu chake mwanzo wa maajabu Fleet Admiral Baston.

Baada ya dunia kupitia upatizo wa moto na Zestra, jeshi la kila nchi likabadilisha mfumo mzima wa madaraja. Kikosi cha chini kabisa kikipewa jina la Ordinart Squadron (OS) kikifuatiwa na Elite Squadron (ES) na Super Elite Squadron (SES). Hivyo vilikuwa ni vikosi vya chini kabisa na vilihusisha wanajeshi walio chini ya umri wa miaka ishirini.

Baada ya vikosi hivyo vilifuatiwa na vikosi vya Komando ambavyo navyo viligawanyika sehemu tatu Ordinary Komando Squadron, Elite Komando Squadron na Super Elite Komando Squadron na viongozi wa vikosi hivyi vyote walikuwa majenerali wa jeshi.

Baada ya vikosi hivyo vilifuata vikosi aina ya Fleet ambavyo viliongozwa na admiral. Na katika daraja la juu kabisa kulikuwa na watu waliotambulika kama Fleet Admiral ambao walikuwa ndio watu wenye cheo cha juu zaidi katika jeshi. Na katika wakati huu kulikuwa na Fleet Admiral (FA) watatu tu.

Baada ya Baston kumuonesha maroboti hayo wakatoka katika chumba hicho kidogo. Shanequeen akatafuta sehemu na kuendelea kufanya alichokuwa akikifanya kwa wiki nzima. Baston akaenda kukaa kwenye kiti, akaanza kuwaza mambo fulani na baada ya dakika chache usingizi mzito ukamchukuwa pasi na yeye kutambua.

***************

"Baston, Baston!! Amka", Baston anafungua macho kivivu na kujikuta kitandani. Ndani ya eneo hilo kulikuwa na chumba kikichokuwa na vitanda kwa ajili wahusika wa eneo hilo.

"Ushamaliza kufanya mazoezi, unataka kuondoka" aliongea. Shanequeen akabaki anamuangalia na kisha kutabasamu. Baston akamuanfalia mrembo aliezidi kurembeka baada ya kutabasamu.

"Vipi nimetoka ute mdomoni au" alihoji Baston.

"Hapana, umelala tokea jana asubuhi"

"Doh!! Usinambie wewe ndio umenibeba kunileta hapa kitamdani" aliongea kwa kukodoa macho.

"Hahaha!! Sina uwezo huwo, jana jioni alikuja baba pamoja na mtu mwengine mmoja ndio walokuleta hapa"

"Oh mi nilidhani ni wewe"

Wakati Baston akiendelea na utani akasikia mtu akisuuza koo, akainua kichwa kuangalia nyuma ya Shanequeen akakutana na sura ya mzee Rozalive. Akarudisha macho yake kwa Shanequeen ambae alikuwa amesimama mbele yake.

"Nimeona hakukuwa na haja ya kuwaficha, jana nimewaeleza wazee wangu" aliongea Binti huyo kusafisha sintofahamy alokuwa nayo Baston.

"Alaa!! Kama umeamua hivyo ni sawa, lakini ni matumaini yangu taarifa hizo zitabakia katika familia yako tu kwanza. Ikiwa zitafika ngazi za juu nina uhakika watakutembeleeni. Naelewa unafahamu ninachoongea Mr Rozaliv" aliongea Baston.

"Ndio"

"Basi sawa, nisubirini nje hapo nijieke sawa nitakuja muda si mrefu", baba na mwana wakatoka nje na kumuacha Baston akijiandaa.

Dakika kumi na tano baadae akatoka akiwa kashabadili nguo, alikuwa amechangamka kuliko jana yake.

"Samahanini kwa kuwaweka sana" aliongea.

"Usijali kuhusu hilo, ila kwanza naomba ni kushukuru kwa kumsaidia binti yangu kwasababu sisi hatukuwa na namna nyingine tena" aliongea mtu mzima huyo na sura yake ilionesha nia yake ya dhati ya shukrani hiyo.

"Ah, ahahaha! Hakuna haja ya kunishukuru, Shanequeen amekuwa msaada mkubwa sana kwangu. Tokea nilivyogundulika kama ni mlemavu, watu wengi walinilenga kama kituko na mara kadhaa wakawa wananionea. Ila mara nyingine Shanequeen amekuwa akisimama na kunitetea, kuna msemo wa kale husema wema hulipwa kwa wema"

"Basi kama ni hivyo sitaendelea kukushukuru, kitu

kingine kilichonileta hapa ni kuhusu jambo tuliloongea

juzi"

"Anha, nimeandaa michoro kadhaa kwa undani zaidi pamoja na maelezo ya kina. Nitakupa michoro hiyo, ila miwili ya mwanzo ni hatimiliki yangu. Itakuwa ni makhususi kwa ajili yangu" aliongea Baston. Kisha abonyeza Comlink yake, na kichukuwa nambari ya comlink ya mzee huyo. Baada ya hapo akahamishia kushindwa zima kwa mzee Rozaliv.

Comlink ni kifaa ambacho kilivaliwa mkononi kama saa, ila kilifanya kazi ya simu. Baada ya dunia kupitia ubatizo na kuingia katika kalenda ya stela. Teknolojia nayo ikakuwa kwa kasi mno kutokana na mahitaji ya binadamu. Na comlink ni matunda ya ukwaji wa teknolojia hiyo.

"Nitaenda kupitia kisha tutajadili zaidi"

"Hakuna shida ila naomba sasa iwe kati yetu"

"Shusha pumzi kijana, mimi ni mfanya biashara naelewa ninachofanya. Ikiwa hakuna zaidi, acha niwaache muendelee na mazoezi" aliaga na kuondoka.

Wakati wote hao Shanequeen alikuwa kimya, biashara haikuwa biashara yake hata kidogo japo amezaliwa katika familia ya wafanya biashara.

"Najua una maswali mengi kichwani lakini kwasasa baki nayo, utapata majibu wakati ukifika"

"Sawa"

"Hatua ya kwanza imekamilika sasa, hatua ya pili ni kuifanyia kazi hii"

"Lakini unajua kama hii henga haimo kwenye bajeti ya serekali kabisa, kama unataka kutekeleza itakugharimu pesa nyingi sana" aliongea Shanequeen. "Najua ila katika akaunti yangu ninazo pesa za kutosha kwa ajili ya wingi ya msingi. Ikiwa mpango wangu utaenda vizuri basi muda mrefu mrefu pesa itakuja tu" aliongea Baston na kutabasamu.

**********
 
SEHEMU YA SITA: MWANZO

To the end (mpaka mwisho) 07

Tariq Haji

0724065911

Katika jengo kubwa lililokuwa na urefu wa zaidi ya mita mia nane kwenda juu. Ndani ya ofisi iliyokuwa ghorofa hamsini na moja, mzee Rozaliv alikuwa amekaa katika kiti akipitia micboro aliyopewa na baston. Kadiri muda ulivyokwenda ndivyo mapigo yake ya moyo yalivyoongezeka.

Kilichomfanya azidi kushangaa ni pale alipokutana na michoro ya aina mbili mbili. Mmoja ukiwa ni wa ndege na mwingine ni mnyama. Ifahamike kuwa katika kipindi hichi maroboti yenye maumbile ya wanyama na ndege yameacha kuzalishwa kutokana na ugumu wake wa kuyatumia.

Binadamu anatembelea miguu miwili ila wanyama wengi wanatumia miguu minne katika kutembea. Hili limesababisha ugumu kwa marubani wengi kuweza kutumia maroboti ambayo yalitumia miguu minne na hivyo maroboti hayo yakaacha kutengenezwa na kufifia ndani ya wakati.

Vivyo hivyo kwa maroboti yenye maumbile ya ndege, haikuwa siri kwamba binadamu hakuwa na uwezo wa kupaa yeye kama yeye. Hilo lilikuwa wazi hata kwa watoto wadogo mno. Huvyo kutengeza maroboti yaliokuwa na uwezo wa kupaa kama ndege ilikuwa ni nje ya matumaini ya wengi.

Japo wanasayansi baadhi walikaa na kujaribu kutengeneza lakini yalipofika kipindi cha majaribio yalifeli kutimiza vigezo na huku kigezo kikubwa kikiwa na kutumika bila shida na binadamu.

Tofauti na mawazo ya wengi, alichokieleza Baston katika michoro hiyo kilibadilisha kabisa mtazamo wa mzee Rozaliv kuhusiana na roboti za aina hiyo. Hata hivyo kulikuwa na mambo mengi ambayo aliyaandika Baston na mzee Rozaliv akashindwa kuyaelewa.

Baada ya kujifikiria kwa muda mrefu, akabonyeza sehemu kwenye comlink yake na kutafuta jina la Baston, akapiga. Baada ya sekunde kadhaa picha ya Baston ikatokea. "Mr Rozaliv" aliita

"Unaweza kufunga safari kuja ofisini kwangu tujadili mambo kadhaa, pia kutakuwa na watu wengine wawili ambao nina waamin sana" aliongea bila kupindisha maneno.

"Lini na saa ngapi"

"Kesho asubuhi, nitamwambia Shanequeen akulete"

"Sawa"

Baada ya maongezi hayo, mzee Rozaliv akakata na kuwapigia watuwl wengine wawili.

Usiku, katika mtaa fulani ukuta namba tano.

"Baston mboja nimekueleza mapema tu, kwa namna yeyote ile siwezi kufika ukuta namba mbili. Hiyo nafasi mnayo nyinyi tu ambao mumejiunga na shule za jeshi. Mimi ruhusa yangu inaishia ukuta namba tatu tu" aliongea kijana mmoja mpana kidogo.

"Naelewa Malik, lakini wewe ni mfanya biashara mzuri sana. Mimi sina kipaji hicho, ikiwa hili dili ninalokwambia litaenda vizuri basi tutakuwa tumepiga hatua kubwa"

Malik, alikuwa ni rafiki wa muda mrefu sana wa Baston tokea udogoni. Tofauti kati ya yeye na Baston ni kwamba Malik alipenda sana maisha yake hivyo pasi na kufaulu mtihani wa jeshi alikataa katakata kwenda jeshini na kuamua kuwa mfanya biashara tokea akiwa na miaka kumi na tatu. Kitu kingine, alipenda pesa mno.

"Malik siongelei vipesa vidogo, naongelea mchuzi wa maana"

"Hebu ngoja kwanza, kama kiasi gani" Baston alifahamu fika kama pesa ndio kitu pekee ambacho kingebadilisha mawazo ya kiumbe huyo japo hakuwa tayari kutumia kadi yake hiyo.

"Naongelea dola za stela kama ndoa moja hivi"

"Bi.. Bi.. Bi... Bilioni moja, ashhhh" Malik akasimama na kuzunguka, akaenda kukaa kwenye kiti cha pembeni na Baston.

"Baston si unajua mimi na wewe ni marafiki wa tokea enzi na enzi, mimi Malik niko tayari hata kuingia shimoni pamoja na wewe" aliongea akitaka kumkumbatia.

"Hebu nitolee sura yako hapa" Baston akamkwepa.

"Nini, sura yangu ina nini. Mimi ni handsome wewe watoto wananigombania"

"Nenda zako huko, kama sio vijisenti kidogo ulivyokuwa navyo ungesimama umesimama"

"Aaayyy, Baston unanikosea heshima sasa, mimi kufa nimesimama"

"Acha na hayo kwanza, kesho asubuhi natakiwa kwenda kuonana na Boss wa kampuni ya Real Steel na wewe utakwenda na mimi kama utawala wangu wa biashara. Fanya uchawi wako usiku huu upate ruhusa ya muda mfupi kuingia ukuta mbili"

"Sawa ila ujue ni pesa nyingi hizo"

"Pesa zako zitarudi ukifanikisha dili", baada ya maongezi ya muda mrefu wakaagana na kila mmoja akaelekea kwake. Wazazi wa wote wawili walitangulia mbele za haki tokea wakiwa na miaka miaka. Na basi wakiishia peke yao katika kipindi chote hicho.

Baston akawasili nyumbani kwake, ilikuwa ni nyumba kubwa ilioonekana kuchakaa kutokana na kuwa ni ya muda mrefu. Akaingia ndani na kukaribishwa na vumbi. Alikuwa na muda mrefu sana hajarudi katika nyumba hiyo. Kwa namna moja ama nyingine aliichukia nyumba hiyo kwa sababu aliachiwa na wazazi wake.

Lakini kiuhalisia aliyoichukia si nyumba bali ni wazazi wake ambao walijitolea kuingia vitani kipindi ambacho nchi hiyo ilikumbana na kisanga cha maana. Hivyo mfalme akatoa wito kwa raia wa kawaida kuitumikia nchi yao na kuwaahidi kiasi kikubwa cha malipo.

maoni mwa waliojitolea na wazazi wake walikuwemo ila miongoni mwa waliorudi wazazi wake hawakuwemo. Na baada ya vita kuisha Baston akapokea fedha nyingi mno kama sehemu ya malipo ya wazee wake kujitolea. Aliichukia sana fedha hiyo na hakuitumia hata senti moja tokea siku aliyopewa mpaka siku hii.

"Baba, mama najua nimekosea kwa kuwakasirikia kwa kipindi chote hiki ila kwanini mlijitolea kwenda vitani wakati mafunzo hamkuwa nayo. Mnajua taabu niliyopitia katika miaka hii kumi na tatu ila sitaki kuendelea kulaumu. Leo ndio itakuwa siku ya mwisho katika nyumba hii. Nitawafanya mpate faraja. , naomba mniangalie" aliongea mbele ya picha ya wazazi wake.

Akaelekea chumbani kwake na kufungua kabati, ndani ya kabati hili ligi na mlango mdogo wa siri. Akaufungua na kutoa mabegi makubwa matatu. Yalikuwa yamejaa vumbi kutokana na kuwa muda mrefu alikuwa katika sehemu hiyo.

Akayafungua yote na kumwaga pesa zilizokuwepo ndani ya mabegi hayo kitandani. Zilikuwa zimefungwa na mifuko maalum hivyo bado zilionekana mpya kabisa. Akatoa ingine kubwa zaidi na kuanza kuzipanga katika begi hilo. Alikamilisha kazi hiyo, akachukuwa picha ya pamoja ya wazazi wake na kutekeleza juu kabisa kisha akafunga.

Alfajiri ya siku ya pili akatoka na begi na kusimama nje ya nyumba. Akaiangalia kwa mara ya mwisho kabla ya kupandisha begi lake katika hoover bike(huva bayk). Akawasha, pikipiki hiyo kubwa haikuwa na matairi bali ilikua ikielea sentimitathalani kutoka ardhini.

Akaweka gia na kuondoka kwa mwendo wa kawaida.

Kutoka ukuta namba tano mpaka namba mbili ni umbali saa takriban nne. Alipofika katika eneo hilo moja kwa moja akaelekea benki na kuweka pesa kisha akaelekea henga namba tano. Alipofika alimkuta Shanequeen akimsubiri.

"Ulikuwa wapi" aliuliza binti huyo

"Nilikuwa naagana na mambo ya zamani" alijibu na kutabasamu ila macho yake yalionesha huzuni kwa mbali.

**********
 
**********

SEHEMU YA SABA: KUACHANA NA YALIYOPITA

To the end (mpaka mwisho) 08

Tariq Haji

0624065911

"Kama uko tayari tunaweza kuenda" aliongea Shanequeen

"Kuna mtu namsubiri akifika tu, tunakwenda",

Shanequeen alitaka kuhoji ni nani huyo lakini akajizuia.

Wakati wakiendelea kuongea mara mlango ukasukumwa.

Mtu mpana kiasi akaingia akionekana kuchoka sana, katika paji lake la uso kulionekana chembe chembe za jasho. Baston alipomuona akatabasamu, Malik macho yake yakatua kwa Baston sekunde ya kwanza na sekunde ya pili yakahamia kwa Shanequeen.

Akapiga hatua za haraka haraka mpaka walipo, Baston akatoa mkono kutaka kumsalimia lakini Malik akampita na kusimama mbele ya Shanequeen.

"Mrembo unaonaje huyu tajiri hapa akakufanya ukawa mkewe" aliongea akijinyooshea kidole yeye mwenyewe. Shanequeen kuona mambo asiyoyaelewa akasogea pembeni na kujificha nyuma ya Baston.

"Ayyy, kwa hiyo unakataa hizi nyama kwasababu ya huyo kimbaumbau" aliongea Malik akitikisa kichwa.

"We ngiri hebu acha mambo ya kijinga" aliongea Baston.

"Ah kaka unanonaje ukaniachia mimi huyo wewe ukatafuta mwingine", Baston akamuangalia rafikie huyo kisha akatikisa kichwa na kutabasamu na kumgeukia Shanequeen.

"Shanequeen huyu ni Malik, ni rafiki yangu tokea utotoni. Na kuhusu tabia aliyoionesha usiiweke moyoni, ndivyo alivyo" aliongea na kumgeukia Malik.

"Malik huyu ni Shanequeen, komredi mwenzangu na mtoto wa mwenye kampuni ya Real Steel"

"Ayyy! Dada mkubwa huyu Malik hapa amekuwa na macho lakini ameshindwa kuona, tafadhali usiichukulie tabia yangu ya mwanzo moyoni mwako" aliongea akilipiga piga tumbo lake kubwa. "Halafu amekwambia kama tulikuwa tunavaliana soksi?".

Ppfff

Shanequeen akajikuta akishindwa kujizuia na kuangua kicheko, Baston alimuangalia Malik na kutaka kumtwanga konzi lakini akajizuia. Alimjua rafiki yake huyo vizuri, na kuhusu suala la kuvaliana soksi hilo ni jambo kujadili siku nyingine.

"Habari yako Malik, nafurahi kukufahamu" aliongea Shanequeen.

"Vivyo hivyo", baada ya utambulisho wakajadiliana kidogo kuhusu mambo kadhaa kabla ya kukubaliana wakati wa kuondoka. Shanequeen akampa taarifa baba yake muda ambao wangewasili ofisini kwake kwa ajiki ya kuepusha sintofahamu.

Muda wa kuondoka ulipofika, Shanequeen akakaa kwenye kiti chake cha walemavu. Baston akawa ndio msukumaji, Malik akafuata nyuma. Wakatoka katika jengo hilo na kuita taksi, japo Shanequeen hakuwa tayari lakini hakuwa na namna. Baston alimbeba na kumuingiza katika gari. Akakikunja kiti na kukiweka nyuma. Malik yeye akapanda mbele na safari ikaanza.

Wakati wote wa safari mashavu ya Shanequeen yalikuwa na wekundu uliotapakaa mpaka kwenye masikio. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakipiga misere bila kufuata njia maalum. Hata yeye hakuelewa kwanini ilikuwa hivyo, alijitahidi sana kuvuta pumzi ili hali hiyo itulie. Baada ya jitihada na muda mrefu hatiamae mapigo yake ya moyo yakapoa na kurudi kuwa ya kawaida.

Baada ya safari ya dakjka takriban ishirini na saba, wakawasiki nje ya jengo kubwa. Wakashuka, safari hii Shanequeen akagoma kusaidiwa na Baston. Akajivuta mwenyewe na kukaa kwenye kiti chake. Maliki alikuwa nyuma akiangalia mchezo wote kisha akatikisha kichwa "kweli Mungu hakupi kila kitu".

Kwa kufuata maelekezo ya binti huyo wakaingia ndani bila shida yeye na kuelekea mpaka ghorofa ya sitini na mbili ambako kulikuwa na ukumbi mdogo wa mikutano.

"Karibuni, Boss anawasubiri ndani" aliongea mwanaume aliekuwa amesimama mlangoni, alikuwa amevalia suti nyeusi na machoni alikuwa na miwani nyeusi. Kwa muonekano tu alikuwa ni mtu alijazia kisawasawa.

Baston akatangulia akisukuma kiti cha Shanequeen, nyuma yake akafuata Malik. Ndani ya ukumbu kulikuwa na watu wengine wawili baada ya baba mzazinwa Shanequeen. Na wote walionekana kuwa kati ya umri wa miaka sitini na sabini.

"Karibuni" aliongea mzee Rozaliv macho yake yakiangukia kwa Malik.

"Ah, huyu ni Malik na ni mshauri na msimamizi wangu wa mambi yote yanayohusiana na biashara" alimtambulisha. Baada ya utambulisho huwo mzee Rozaliv akashusha pumzi na kuwaonesha sehemu ya kukaa.

"Kulia kwangu ni profesa Martin Ashdawi, ni profesa katika asili na sayansi ya Itheria. Kushoto kwangu ni profesa Ahmed Bagani na ni mtaalamu na sayansi ya kiroboti" mzee Rozaliv aliwatambulisha wazee aliokuwa nao.

Ghafla meza waliokuwepo ikawaka na kuonesha mafaili mbali mbali ambayo yalikuwa yakielea hewani.

"Baston iki tusipoteze muda, kuna mambi tutakuuliza ili kupata uelewa zaidi ya kile ulichonipa" aliongea mzee Rozaliv.

"Itakuwa ni jambo jema sana" aliitika na kutabasamu. Machi yake yalikuwa tulivu kama bahari kipindi kisicho na upepo. Utulivu wake huwo uliwafanya mpaka watu wazima hao kushtuka.

"Katika moja ya mawazo yako, umetaja sababu chache za kwanini marubani wengi hawawezi kutumia roboti zao katika kiwango cha juu. Unaweza kufafanua zaidi" aliongea profesa Ashdawi.

"Sababu kubwa ni kwamba marubani wengi wanatumia miili yao kama chanzo cha itherion jambo linalopelekea kuchoka sana. Si hilo tu, tunafahamu kama roboti hizi ni kubwa mno na zina mifumo migumu na 'complex'. Kwa mantiki hiyo ni sawa na kuchukuwa betri ya hoover bike (huva bayk) na kutaka kuzalishia umeme wa mji mzima. Hata betri hiyo iwe na uwezo kiasi gani haitafanikiwa kuzalisha umeme utakaowasha mji mzima".

"Rubani ni sawa na betri na mji ni hizo mashine kubwa (roboti), ili mtu kuzimudu atahitaji atumie kiwango kikubwa cha itherion na ndio maana marubani wengi wanaishia chini ya saa tatu na kuhitaji kurudi kwa ajili ya kupumzika"

"Na moja kati ya suluhisho lako umesema ni moyo" alihoji profesa Ashdawi.

"Ndio"

"Kivipi?"

"Binadamu ana moyo, kwanini na roboti zisiwe na moyo. Wote hapa tunafahamu kuwa mwili wa binadamu unanyonya itherion kutoka kwenye mazingira lakini moyo ndio unaofanya kazi ya kuisambaza maeneo tofauti ya mwili. Lakini ifahamike kuwa moyo ni kipande kidogo sana

nyama ambayo kinafanya kazi chenyewe bika mtu kukipa amri"

"Ila tutambue kuwa moyo utafanya kazi ya ziada pale utakumbana na hali isiyo ya kawaida na kadri utakavyokwenda moyo utachoka na mwisho utashindwa kufanya kazi yake. Na hiyo ndio sababu kunwa kwanini marubani wengi hupoteza maisha kati ya miaka thalathini na arobaini" akanyamaza kidogo, kisha akabinyeza faili na kulifungua.

Kisha akaendelea "lakini itakuwaje ikiwa na roboti atakuwa na moyo wake, kwa maneno mengine atakuwa na uwezo wa kunyonya itherion. Hilo litapunguza kaza na kupunguza mzigo kwa rubani husika"

"Profesa Ashdawi nina uhakika umewahi kusikia kuhusu almasi ya damu (blood diamond)?"

"Ndio"

"Unajua kwanimi imeitwa hivyo!?"

"Hilo limtokana na almasi hiyo kukaa ardhini muda mrefu tena katika kina kirefu"

"Hapana, katika historia kuna almasi zilizogundulika kuwa ardhini kwa zaidi ya miaka elfu kumi lakini zilikuwa katika hali yake ya kioo"

"Unakusudia kusema nini"

"Almasi ya damu ni almasi ambayo imebadilika rangi kwa kunyonya itherion" kauli hiyo ikawashtua wote waliokuwemo ndani ya ukumbi huwo.

**********
_672e3313-a55d-497e-93c3-3ceb12763fd4.jpeg
 
SEHEMU YA NANE: ALMASI YA DAMU

To the end (mpaka mwisho) 09

Tariq Haji

0624065911

"Kwa hiyo unamaanisha kwa kuitumia hiyo tutafanikisha ulichoandika"

"Ndio"

"Ila unafahamu kama kupatikana kwake ni kazi sana"

"Najua ila si lazima ipatikane iliyolala mchangani muda mrefu, kinachohitajika ni kupata almasi ambayo ina dalili tu za itherion. Baada ya hapo" akanyamaza tena kisha akachagua faili jingine na kubonyeza, mchoro wa mashine isiyoeleweka ukaonekana.

"Hii inaitwa ither reactor (itha riacta), kazi yake ni kuielekeza itherion ichuruzike kuelekea uoande fulani", profesa Bagan akashtuka na kumuangalia bastona ambae alikuwa akiendelea na maelekezo.

Akaingilia "kutumia ither reactor tutafanikiwa kutengeneza almasi yenye itherion ya kutosha".

"Ndio" alijibu Baston.

"Shabbash, kwanini usije kujiunga na kitengo changu.

Mahali unapotakiwa kuwa siyo vitani bali ni jukwaa la wasomi" aliongea profesa Bagani macho yake yakimweka mweka.

"Ahsante kwa ofa yako, lakini jukwaa la wasomi si sehemu yangu". Profesa Bagani akakunja ndita na kumuangalia Baston kisha akashusha pumzi na kujiweka sawa.

"Kitu kingine ulichokiandika ni kuhusu uchelewaji wa roboti kupokea maelekezo kutoka kwa marubani, fafanua" aliuliza profesa Bagani.

"Ndio kwasababu marubani wengine wanafikiri kwanza kabla ya kutoa maelekezo, ile nusu sekunde ya kufikiri kwanza kusha kucheza vitufe vya mashine inapelekea ucheleweshaji wa roboti kufanyia kazi amri hiyo. Ila hilo tatizo litaondoka ikiwa kutakuwa na mfumo kamili wa neurolink (nyurolink) kati ya rubani na roboti wake" aliongea Baston.

"Kumaanisha kuwa roboti na rubani kuwa kitu kimoja, mawazo ya rubani yasafirishwe moja kwa moja katika mfumo roboti" aliongea profesa Bagani.

"Ndio"

"Lakini hilo lishawahi kufanyika, ila likaachwa kutokana na kuwa na hatari nyingi"

"Ndio lishawahi kufanyika lakini ni mwaka gani?, ni miaka mingi sana kipindi ambacho teknolojia ilikuwa bado ni changa. Kwa ilipofika sasa nina uhakika inawezekana kutengeneza mfumo rafiki. Nimeeeleza kila kitu mpaka pale uwezo wangu ulipofikia, sehemu ikiyobaki ni kwenu wataalamu".

"Nitalifanyia kazi, swali langu ka mwisho. Kwanini roboti lenye kufanana na ndege", miongoni mwa michoro aliyoichora Baston. Kulikuwa na mchoro wa roboti lenye umbile la ndege. Ila ifahamike kuwa watu walishajaribu na matokeo hayakuwa mazuri sana hivyo wakaachana nayo. Na kutengeza mfumo maalum ambao ukiwasaidia maroboti mengine kuweza kupaa angani.

Baston akasita kidogo kabla ya kujibu swali hiko, ni kama vile alikuwa akiwaza jambo kichwa. Mmmfffh!! "Ninaamini tunategemea sana mifumo ya kisasa ya ukusanyaji taarifa, lakini mimi siamini kama taarifa zote hizo ni sahihi. Tambueni kuwa sikosoi mifumo iliyokuwepo laa!! Ninacho sema ni kuwa kuna taarifa muhimu tunazikosa" alitulia na kuwaangalia.

"Na hapo ndio unakuja umuhimu wa roboti hizo, roboti aina ya ndege si kwa ajili ya vita. Ila ni kwa ajili ya wepesi wa kurudisha taarifa pale kikosi kitakapokwenda katika misheni ya uchunguzi. Ifahamike kuwa ndege ni kiumbe mwenye mifupa yenye matobo na mepesi hivyo kumfanya kuwa mwepesi na kusafiri kwa kasi zaidi huku akipunguza msuguano na upepe".

"Unataka kunambia kama unakusudia kukirudisha tena kikosi cha kazi za nje ya ngome" aliuliza mzee Rozaliv.

"Ndio, henga namba tano haitakuwa kikosi cha ndani. Sisi tutakuwa nje ya ngome kwa kazi za muda mrefu, hatutakuwa waoga ksujifungia ndani. Tutakwenda kuufungua ulimwengu tena, ulimwengu ambao binadamu watakuwa na uwezo kuzurura bila kuhofia maisha yao".

Wote waliokuwepo hapo ukiachilia Malik walidhani hiyo ilikuwa kauli ya mwendawazimu. Malik alimfahamu vyema Baston, ni mtu hakutumia hata senti moja katika malipo ya roho za wazee wake. Hata baada ya kugundua kuwa alikuwa mlemavu (bila uwezo wa kunyonya itherion) lakini bado aligoma kuacha kujiunga na jeshi hata kama alikuwa mfagiaji.

Alimtambua Baston kama mtu aliechonga muelekeo wa maisha yake. Pale anapoamua kuwa jambo fulani liko hivyo, hata dunia na washirika wake wote hawataweza kubadilisha maamuzi yake, kisiki kisicho ng'oka. Na kauli hiyo itathibitishwa baadae na profesa Bagani katika makala yake iliyobeba jina la "kauli ya mwendawazimu iliyoleta mabadiliko".

Maswali yalikuwa mengi mno kwasababu mambo mengi aliyaoandika yalikuwa mageni kwa watu hao. Ila kiuhalisia hayakuwa mageni, yote hayo Baston aliyarithi kutoka katika kumbukumbu za Gilbot. Kwa maneno mingine, taaluma yote hiyo ilikuwepo miaka mia tatu nyuma ila kwa namna moja ama nyingine ilizikwa kabisa.

Hivyo kumfanya Baston kuwaza kwanini ilikuwa hivyo, tayari katika kichwa chake alikuwa na mashaka mengi lakini alifahamu kabisa majibu ya mashaka yake asingeyapata kirahisi. Hivyo moja kati ya malengo yake ya kutengeneza kikosi ambacho kitakuwa nje kwa muda mrefu ni kusaka majibu.

Baada saa mbili nzima kupita cha maswali, majibu na maelezo, hatimaye kikao kikafikia tamati. Japo ndani ya ukumbi huwo kulikuwa na ac, Baston alikuwa akitokwa na jasho.

"Baston twende nikutembeze uone baadhi ya kazi za kampuni yetu, tunaweza kuwa sio miongoni mwa kampuni tatu bora katika uzalishaji wa roboti lakini nina uhakik zetu ziko sawa na nyingine" aliongea mzee Rozaliv.

"Itakuwa bora, kuna msemo wa kale unasema. Mwengine hajui thamani thamani ya kitu kama hajaona mizizi yake" aliongea Baston akisimama. Mzee Rozaliv akatabasamu na kuinuka, akaonesha njia na kutangulia.

Watu sita wakaelekea kwenye lifti na kuingia, ikaanza kushuka chini kwa kasi ya wastani. Baada ya dakika mbili ikasimama na mlango ukafunguka. Mbele ya kulikuwa na eneo kubwa sana, kulikuwa na watu wengine katika mavazi mbali mbali na kila mmoja alikuwa na shuguli yake.

Sauti mashine zikinguruma ndizo zilizotawala eneo hilo pamoja na cheche za moto.

"Karibu katika kitovu cha uzalishaji,The Hub (hab)" aliongea mzee Rozaliv. Kauli yake hiyo ilikuwa na alama majigambo na furaha. Wakashuka ngazi na kuelekea katika eneo hilo la mashine, kila walipopita, wafanya kazi waliacha kazi zao na kutoa heshima kisha wakarudi kuendelea na kazi zao.

Waliendelea kuzunguka maeneo mbali mbali huku mzee Rozaliv akitoa maelezo ya kina ya vitu mbali mbali. Safari ilikomea nje ya mlango mkubwa. Maneno ya wino mweusi yalisomeka "sector 2".

"Humu ndimo tunapoweka kazi zilizokamilika" aliongea mzee Rozaliv akipitisha kadi yake katika sehemu fulani. Mtikisiko mdogo ukasikika, na mlango huwo mkubwa ukafunguka. Ndani wakakaribishwa na maroboti mengi yaliokuwa yamekamilika yakisubiri wateja tu.

"Kampuni yangu mpaka sasa inazalisha brand tatu za maroboti, kutoka katika hizo tunazalisha brand za sekondari ambazo zinatoka katika asili ya hizo lakini zinakuwa na utofuati kidogo" aliongea mzee Rozaliv.

Akaendelea "kulia kwangu ni Indigo 72 ni aina ya roboti zito na kazi yake ni ulinzi. Inashambulia kakini nguvu yake ya mashambulizi sio kubwa. Ila linapokuja suala la kulinda, limetengenezwa na ngao maalum ambalo linaweza kuzuia hata kichwa cha nyuklia". Baston akatikisa kichwa kama sehemu ya heshima.

************
_0122ae19-3cc2-4537-ba1d-06254afb7bbc.jpeg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom