Ukiwa hujaalikwa Eid na unataka Kutengeneza Mazingira ya Kualikwa ili ukale Pilau la bure utumie mbinu gani?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Vyakula ndiyo vinaanza Kupikwa sasa tafadhali wengine hatujaalikwa ila kuna sehemu kadhaa dalili zote za Pilau zinajionyesha je, tutumie Mbinu gani ili tulazimishe Kualikwa?

Kama sijaalikwa Leo au hata sijatengeneza Mazingira ya Kualikwa Mchana wangu na Jioni yangu naona itakuwa mbaya na nitaishia tu kutizama Mijusi inayokatiza kila mara kwa Kukimbizana katika Kuta na Kenchi za Chumba changu.

Na kuna Nyumba naiona kabisa mbele yangu Chakula kinapikwa na najua Kitabaki tu na Kutupwa hivyo nataka Kutengeneza Mazingira nialikwe ili nikienda nichote kabisa Chakula cha Leo hadi Jumapili kabla ya Kuonana na Mhindi wangu Jumatatu.

Wazee wa Kuzamia Msaada tafadhali.
 
Singizia umekufa halafu waombe michango.😂😂😂
 
Hivi inakaa hawajui uko ndani labda. Sasa wewe kama una system ya music basi weka ngoma za uswazi hapo, sauti iskike vizuri nje alafu mlango wacha wazi. Kama vipi waweza improvise kwa kutoa nguo nje na kufua, hakikisha ni mrudo wa nguo, yaani usiishe haraka kuzifua. Hapo Biri mpaka lilitwe tu. Usisahau kuja na mrejesho! 🤣 🤣 🤣
 
Tualikane mkuu,mimi hapa najaribu kulala ila tumbo linakataa kukipa kichwa ushirikiano ili nilale japo niisahau njaa kwa muda,

Yaani nimeishia kuhesabu mistari ya mabati tu.
Kwani kaka jirani kwa mama zuhura hapo hujapeleka chapati kweli
Au ulishakula sasa unataka ushindilie ubwabwa wangu.
 
Vyakula ndiyo vinaanza Kupikwa sasa tafadhali wengine hatujaalikwa ila kuna sehemu kadhaa dalili zote za Pilau zinajionyesha je, tutumie Mbinu gani ili tulazimishe Kualikwa?

Kama sijaalikwa Leo au hata sijatengeneza Mazingira ya Kualikwa Mchana wangu na Jioni yangu naona itakuwa mbaya na nitaishia tu kutizama Mijusi inayokatiza kila mara kwa Kukimbizana katika Kuta na Kenchi za Chumba changu.

Na kuna Nyumba naiona kabisa mbele yangu Chakula kinapikwa na najua Kitabaki tu na Kutupwa hivyo nataka Kutengeneza Mazingira nialikwe ili nikienda nichote kabisa Chakula cha Leo hadi Jumapili kabla ya Kuonana na Mhindi wangu Jumatatu.

Wazee wa Kuzamia Msaada tafadhali.

Nenda msikitini hakukosekani pilau siku ya Eid!
 
Kwani kaka jirani kwa mama zuhura hapo hujapeleka chapati kweli
Au ulishakula sasa unataka ushindilie ubwabwa wangu.
Mkuu kwa Mama Zuhura wameenda kula Eid kwa mjomba wao Kigamboni,limebaki li Mama Zena tu nalo lina roho ya uchoyo kinoma.
 
Back
Top Bottom