Ukitunga sheria kumbuka kuwa inaweza kukugeuka

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,045
Mwaka 1880 Malkia Sunanda Kamiriratana wa Thailand akiwa kwenye boat ndogo ya kifalme, boat hiyo ilipata ajali kwa kugongana na boat kubwa.

Watu waliokuwa kwenye boat ndogo yani malkia, binti yake, vijakazi na walinzi wake wote walidumbukia kwenye maji.
Shida ikawa ni je wamuokoe malkia au wamuache azame?

Sheria ya wakati huo, hawakuruhusiwa kumgusa malkia. Yani kumgusa malkia lilikuwa ni kosa kubwa na adhabu yake ni kifo.

Hivyo, walimuacha akazama yeye na mtoto wake na kufa. Hakuna mtu mwingine aliyekufa kwenye ajali hiyo isipokuwa malkia na binti yake maana hawakujua kuogelea.

Mazishi yao yaliandaliwa kwa miezi kumi, na yalikuwa mazishi ya kihistoria.

Jamani ukitunga sheria jua inaweza kurudi na kubite your ass.
 
Muulize Tawio Adamafye waziri wa Habari wa Ghana enzi ya NKWAME NKURUMA.
Sheria alizotunga zilianza kumuwajibisha mwenyewe. Tusiende mbali anza na NAPE NNAUYE maliza na JOBO NDUGAI kanuni walizoziasisi wao wenyewe ziliwanyoosha na wao wenyewe.
Ebu nipe hicho kosa cha Tawio mkuu
 
Muulize Tawio Adamafye waziri wa Habari wa Ghana enzi ya NKWAME NKURUMA.
Sheria alizotunga zilianza kumuwajibisha mwenyewe. Tusiende mbali anza na NAPE NNAUYE maliza na JOBO NDUGAI kanuni walizoziasisi wao wenyewe ziliwanyoosha na wao wenyewe.
Ndungai sijui yuko wapi
 
Ni funzo zuri japo ...
SmartSelect_20220314-075838_Chrome.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom