Marufuku kumshika malkia Sunanda Kumariratana

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,701
Sunanda Kumariratara alikuwa ni malkia wa Thailand alikufa kwa kuzama maji baharini. Wasaidizi aliokuwa nao hawakumuokoa kwasababu kumshika malkia ilikuwa ni kosa na adhabu yake ni kifo!


FB_IMG_1619552059544.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app

===

Anaitwa Sunanda Kumariratana, alikuwa ni malkia wa Siam kati ya mwaka 1877 hadi anafariki May 31, 1880 akiwa na umri wa miaka 19 tuu, alifariki kwa kuzama na boti majini. Alizaliwa mwaka 1860, na alitawazwa kuwa malkia mwaka 1877 akiwa na umri wa miaka 17 tuu!. Aliolewa na mfalme Rama V wa Siam.

Siam ni jina la zamani la nchi ya Thailand, zamani ilikuwa ikiitwa Siam kama ambavyo hapo awali Zimbabwe ilivyokuwa ikiitwa Rhodesia au Tanzania bara ilivyokuwa ikiitwa Tanganyika.
Zamani katika nchi hii kulikuwa na sheria kali ambayo ilikuwa ukibainika umemgusa tuu malkia, mfalme au hata mtu yoyote kutoka katika familia ya kifalme basi moja kwa moja adhabu yako ni kifo cha papo kwa hapo!, likikuwa ni kosa kubwa sana kwa mtu wa kawaida kumgusa mtu kutoka familia ya kifalme, hii ndio sababu ya malkia huyu kufa kwa kukosa msaada huku watu wakimshuhudia tuu.
Sheria ilikuwa inasema kuwa Ikiwa mtu kutoka familia ya kifalme atakuwa akizama majini na akaokolewa, basi mtu huyo aliyemuokoa atahukumiwa kifo. Sheria ilitafsiri kuwa mwokozi atatakiwa kuuawa kwa kosa la kumgusa mtu wa familia ya kifalme, hawakufikiria kama kuna uokozi wa kutoka katika kifo!.

Lakini pia kulikuwa na tamaduni nyingi sana nchini siam, mojawapo ilikuwa ni kamwe usijaribu kumwokoa mtu anayezama majini, ikiwa utajitolea ndani ya maji kumuokoa mtu, nawewe unaweza kufa pia. Na kama utafanikiwa kumuokoa mtu majini na ukarudi salama, basi mizimu ya mto huo itarudi na kudai maisha yako wewe kama mbadala wa yule uliyemuokoa kutoka majini humo.
Malkia huyu akiwa na binti yake walizama wakati boti yao ya kifalme ikiwa njiani kuelekea katika Ikulu ya Bang Pa-In Royal.

Mashuhuda wengi wa ajali hiyo wakiwemo walinzi wake hawakuthubutu kabisa kumgusa malkia na kumsaidia wakati akizama, walishuhudia anakufa kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ajali. Toka hapo sheria ikabadilishwa.

Written By @fm_facts
 
Uongo huo.

Soma hapo from wikipedia.

"
There is an often repeated myth that the many witnesses to the accident did not dare to touch the queen, a capital offense—not even to save her life. However, this was not the case; the King's diary records that boatmen dived into the water, pulled the queen and her daughter from the entangling curtains, and carried them to another boat, where attendants worked in vain to resuscitate them.[4] No one else died in the accident.[3]"
 
Uongo huo.

Soma hapo from wikipedia.

"
There is an often repeated myth that the many witnesses to the accident did not dare to touch the queen, a capital offense—not even to save her life. However, this was not the case; the King's diary records that boatmen dived into the water, pulled the queen and her daughter from the entangling curtains, and carried them to another boat, where attendants worked in vain to resuscitate them.[4] No one else died in the accident.[3]"
Sasa wewe umeandika malkia wa wapii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom