Ukitapeliwa usifanye haya. Ni janga!

Ukitapeliwa usifanye haya. Ni janga!

Miaka ya nyuma nikiwa bado bwana mdogo ndio naanza maisha nilijikuta naiuza pikipiki yangu (niliyoipata kwa urithi na sikuwa na uwezo wa kuinunua) kwa Ml 1.2 na zote kumpatia tapeli wa mambo ya rupia! Nilifadhaika sana na kuingia unyonge haswa kwa kuwa ilikuwa ndio kitu pekee ninachokitegemea na cha thamani nilichonacho, maneno ya malawama ya mama mzazi na mke wangu yalizidi kuniumiza moyo haswa kwa kuwa walinikanya hapo kabla lakini sikuwaelewa.
Nilijikaza kiume nikajipa moyo na kuanza upya kwani hadi kazi nilishaacha nikajikuta nipo vijijini takribani miezi miwili nikiwawinda wabaya wangu na nikaambulia patupu, nilianza moja na kujipanga nikiwa na ghadhabu za maisha hatimae kazi zikakaa sawa nikanunua kwa jasho langu machine kubwa na yenye thamani kuliko ile na pia kufikia malengo kadhaa ya kimaisha kwani tukio lile kila nilipolikumbuka lilinifanya niamini zaidi kazi za mikono yangu ndio zitakazo nisogeza niongeze bidii kwani hakuna njia ya mkato.
Baadae nikahamia kwenye magari na hapo akatokea mtu ambae nilimuamini sana na kumtumia pesa mara nyingi na kunitumia spare na muda mwengine kuniletea yeye mwenyewe ila ghafla akaja kunitapeli laki nne za gear box na kubadilisha line! Maisha yana mambo mengi na mengine huja kama funzo na kukukomaza ki fikra hivyo huyu nae nilimuombea Mungu tu....baada ya miezi kadhaa nikapita mahali nikasikia vurugu kuna mtu anapigwa kufika ni yule jamaa kamtapeli mtu karibu ml 3 za mazao!!
Matukio hayo japo yalikuwa ni mabaya na kwa ambae hayajamkuta huona ni ya kizembe ila kwangu niliyageuza kuwa chachu ya mafanikio na leo hii ukisogea karibu tu nimeshakusoma ubongo wako kabla hujatoa kauli [emoji2][emoji2][emoji2]
Asante Kwa somo zuri ndugu! We learn through mistakes!
 
Usiwakumbushe wana JF waliokiwa na Forex trader. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Cc Ontario
Tuliosema kuna harufu ya utapeli tulishambuliwa kama mpira wa Kona!
 
Aiseee posta na feri Kuna matapeli Sana, na ujanja wangu Kuna mdada alinipuna laki Saba
Kila Mara nilikuwa namuona maeneo ya posta hivyo tulianza kuzoeana, kumbe ni matapeli tu.
 
Daah hiyo namba 12 dada yangu kapigiwa simu juzi. Akasema hawa wameangalia mwaka nilioanza kazi wamepiga hesabu wakajua nastaafu mwaka huu au mwakani
 
mzee hio comment umeichukulia serious kias hichooo? Sikua na nia hioo...
Hata kama yupo serious vipi achana naye, mtu atawekaje 'ndita' usoni wakati tupo darasani, kisa eti mwalimu wa biology kakitaja kiungo cha uzazi wa jinsi yake na kila mwanafunzi kasikia?
Tusi kwenye kipindi siyo tusi ni somo.
 
Juzi tuu kuna jamaa kani call ooh sijui nna wazungu wanataka vinyago so nataka utusaidie wewe uwe ndio kama mwenyeji wetu hapo daslam na bla bla nyiingi mara nikupe namba ya boss wangu uongee nae,.lol nilicheka kwa nguvu maana daah basi tuu halafu jamaa nikimuona namkumbuka fresh kabisaa kaka smart nini ana muonekano ila ndio hivyo tena,.naona ndio mishe zake mjini hizo.
Sema nakuliwa pia uliliwa mbona Hilo usemi..
 
Utapeli ni art ya miaka dahari. Katika maisha zaidi ya 70% ya binadamu duniani wamewahi kukutana na dhahama ya kutapeliwa.

Dakika 5 mpk saa 1 baada ya kutapeliwa mtu huwa anachanganyikiwa. Dopamine yake huwa high na anajiona ni kilaza wa kiwango cha Airbus!

Wengi hufanya maamuzi ya kijinga baada ya kutapeliwa.

Tafadhari usifanye haya!
1. Usiende Kwa mganga wa kienyeji.
Hapa wengi huamua kwenda kuroga. Yaani eidha kurudisha Mali ilopotea au kumkomoa tapeli. Huku wengi huishia kutapeliwa Zaid. Mf kuna rafiki angu alitapeliwa about 6.7M akaenda Kwa sangoma akaishia kupigwa na mganga takribani 12M na hakupata chochote!

2. Kuna huu utapeli wa kupitia simu, issues za Mpesa, madawa, vifaa vya kilimo nk. Watapeliwa hustuka kuwa wameshalizwa baada ya kutuma pesa na mtumiwa hapatikani. Wengine huambulia kulia na kutupa simu. Usitupe simu, wala usipoteze muda kuloga au sijui kujihangaisha. Tulia, let life go. Chukulia kama umelipia tuisheni na Amua kutotapelewa tena.

3. Wanaotapeliwa Kwa kuuziwa Mali fake mf simu, dawa fake, madini feki, mamilioni ya pesa bank, Mali kale nk kupigwa magari nk, usitafute gari mfukoni. Epuka kutaka kujiua . Wewe sio wa Kwanza, wewe sio wa mwisho. Usipaniki. Tulia, tafuta wafariji, usikae peke yako.Kubali matokeo. Jipange kutokulizwa tena.

4. Utapeli wowote usikubali uuondoe utu wako. Bado maisha yanaendelea. Maisha ni ya thamani kuliko Mali yoyote. Mali inapatikana, uhai hauuzwi.

5. Halafu ndugu yangu, Kwa nini ukubali kuurudia utapeli? Acha tamaa ya kuwekeza Tsh 100,000 utengeneze Milion 100. Mali hupatikana kwa hard working.

6. Kuna wanaoamua kuwa matapeli baada ya kutapeliwa. Hapa sasa nikuambie ndugu, two blacks never make one white! Utaishia pabaya.

7. Jipe muda wa kujifunza njia mbalimbali za kutapeliwa na uziepuke. Hapa JF watu wamesimulia Sana walivyotapeliwa. Sasa wewe ukisoma unajifunza nini? Bado unaibiwa Kwa njia ya wizi ulosoma hapa?

8. Matapeli wa njia za madawa ya kichawi si wa kuamini. Kila utapeli ni suala la kucheza na akili yako tu! Yes, kuna Dawa za kitaalam za kupumbaza! Jiepushe na watu usiowajua. Asikushike wala kukukalibia kizembe. Ukigundua ni tapeli mbutue haraka!

9. Fahamu kuwa hakuna mtu asiye kujua atakayekupa utajiri. Kwa nini akutajirishe wewe mtu baki? From no where akuambie mtumie 2M akupe deal la 50M??? Unaamini hii trick ya tangu Zama za mawe za kati? Ndo pale unajikuta mtu kalamba 2M yako then unaachiwa mawe au magazeti kwenye brifkesi! Yaani aache kumpa utajiri mke wake au mdogo wake akutajirishe wewe wa Nanjilinji? Thubutuu!

10. Dawa ya tapeli ni kutompa muda. Kuna watu wanajifunza utapeli 10 good years. Sasa we umpe dk 10 zako si unalizwa?
Acha kushinda Instagram basi, pitia hata clips za Bongo Dar es salaam ujifunze wenzako wanaovyolizwa na we usilizwe!

11. Ukitapeliwa usiwe msiri au kutunga uongo mf eti umepoteza au sijui umevamiwa, no! Washirikishe wengine umelizwaje ili na wao wasilizwe! Sharing is caring! Ukikaa nalo moyoni litakutesa! Funguka!

12. Wastaafu: Ninyi huwa ni target kubwa ya matapeli, kuna timu kabisa kama kampuni ya kuwaibia. Huko kwenye hili jeshi la shetani kuna watu huvaa uhusika kama mashehe, mapadre, masista, wachungaji, usalama wa taifa, wanajeshi, Polisi, madaktari, wanasheria, mainjinia, mabwana misitu, mabwana mifugo na Kada zote uzijuazo ili tu kukuaminisha kuwa ni watu sahihi kumbe wapigaji, wakishamaliza kabisa Ile shilingi ya mwisho kwenye akaunti yako, hutawaona tena!

We ukipata pesheni tu, usimwamini mtu! Kula na familia yako usubiri kujirudishia faili Kwa Israel. Usifanye biashara ambayo hukuwahi kufanya, utapigwa tu na utakufa Kwa mistress Mzee wangu!

Sikio la kufa halisikii Dawa, dunia kila Siku ma-ndaza na mazwazwa au mburura wanazaliwa daily, kuna mtu dakika hii analizwa kiboya tena!!

Ndo maana US wanaruhusu kuwa na Gun! Hapa Bongo wakiruhusu tu nafuata AK 47 pale Mzinga natembea nayo 24/7, ukiniletea stories za sijui uniuzie rupia nipige 200M naku-shoot ya mdomo (cha ajabu kuna matapeli yenye pHD yanakuliza mpk bunduki yako)

Ene Wei, ukiuziwa sabuni ya mbuni kwenye housing ya iPhone usiitupe, kaogee!


Stuka!!!

Na kwakuongezea hapo, ukishagundua umetapeliwa usianze kulia kwa sauti kubwa, kupiga mayowe na kugalagala chini. Sanasana hapo utawapa faida watu wengine watakaokua wanakuangalia na kufa mbavu kwa vicheko.

Mwisho kabisa ukitapeliwa usipoteze muda wako KWENDA POLISI!
 
Hahahahahaha......
Nilitapeliwa 200k,nilipo gundua nimetapeliwa nilipatwa na hasira Kali alafu baadae nikaanza kumuonea wivu mtu alie nitapeli ( yaani kaingiza 200k mda mfupi tuu) nikaamua na mimi nitoe bank 100k na nikaitumia kwa kula bata ili ieleweke moja kuwa nimepoteza 300k....
 
matapeli yenye pHD yanakuliza mpk bunduki yako)
Hahhaaaaa!, ahsante kaka umesurrender mpaka kalashkanov yako! Kweli matapeli ni wababe
 
Usipoteze muda tafuta nyingine kaka.
Uko serious? Kuna mafala wamenitapeli 7m mwezi wa 5 huu sijawafanya kitu bado natafakari tu. Ila sijasamehe.
Kama uko serious mi napenda waokote makopo wote 3 mbwa wale.
 
Back
Top Bottom