Ukitapeliwa usifanye haya. Ni janga!

Ukitapeliwa usifanye haya. Ni janga!

Kuna waliotapeliwa kupewa laptop wametulia tu tena wanataka kuanzisha shirikisho la kumuunga mkono tapeli
Somo zuri sana,
na 90% ukitapeliwa ujue imepita hiooo..
Wewe kajifungie ulie weeeee......

Watu tumetapeliwa 50M na korosho tumetulia zetu tuuu, wala hatumuendei kwa mganga...
 
Maisha lazima yaendelee, wajinga hawaishi na binadamu huwezi jua yote
 
Kuna utapeli wa kuumiza watu kimapenzi pia nkuu wa nkoa anaufuatilia
 
Uko serious? Kuna mafala wamenitapeli 7m mwezi wa 5 huu sijawafanya kitu bado natafakari tu. Ila sijasamehe.
Kama uko serious mi napenda waokote makopo wote 3 mbwa wale.
Naona mmelike tu. Mil 7 yangu imenirudisha sana nyuma. Natafuta mchawi wa kufanya hiyo kazi.
 
Nilitapeliwa simu way back 2006 huko, aisee niliitafuta kuanzia kichwani hadi kwenye socksi huku nikizunguka zunguka huku na kule kama mwehu
 
Miaka ya nyuma nikiwa bado bwana mdogo ndio naanza maisha nilijikuta naiuza pikipiki yangu (niliyoipata kwa urithi na sikuwa na uwezo wa kuinunua) kwa Ml 1.2 na zote kumpatia tapeli wa mambo ya rupia! Nilifadhaika sana na kuingia unyonge haswa kwa kuwa ilikuwa ndio kitu pekee ninachokitegemea na cha thamani nilichonacho, maneno ya malawama ya mama mzazi na mke wangu yalizidi kuniumiza moyo haswa kwa kuwa walinikanya hapo kabla lakini sikuwaelewa.

Nilijikaza kiume nikajipa moyo na kuanza upya kwani hadi kazi nilishaacha nikajikuta nipo vijijini takribani miezi miwili nikiwawinda wabaya wangu na nikaambulia patupu, nilianza moja na kujipanga nikiwa na ghadhabu za maisha hatimae kazi zikakaa sawa nikanunua kwa jasho langu machine kubwa na yenye thamani kuliko ile na pia kufikia malengo kadhaa ya kimaisha kwani tukio lile kila nilipolikumbuka lilinifanya niamini zaidi kazi za mikono yangu ndio zitakazo nisogeza niongeze bidii kwani hakuna njia ya mkato.

Baadae nikahamia kwenye magari na hapo akatokea mtu ambae nilimuamini sana na kumtumia pesa mara nyingi na kunitumia spare na muda mwengine kuniletea yeye mwenyewe ila ghafla akaja kunitapeli laki nne za gear box na kubadilisha line! Maisha yana mambo mengi na mengine huja kama funzo na kukukomaza ki fikra hivyo huyu nae nilimuombea Mungu tu....baada ya miezi kadhaa nikapita mahali nikasikia vurugu kuna mtu anapigwa kufika ni yule jamaa kamtapeli mtu karibu ml 3 za mazao!!

Matukio hayo japo yalikuwa ni mabaya na kwa ambae hayajamkuta huona ni ya kizembe ila kwangu niliyageuza kuwa chachu ya mafanikio na leo hii ukisogea karibu tu nimeshakusoma ubongo wako kabla hujatoa kauli [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kutapeliwa maaana yake ni kuwa
Una Dalili ya Wizi au Tamaa
Haiwezekani utake iphone 7 kwa laki 1 kama sio ya wizi au unapigwa
 
Kuna Mama alinitapeli Tani 2 ya mchele pale Ubungo kiukweli sikumsamehe Sasa hivi anaokota makopo pale Ubungo
 
Back
Top Bottom