Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,805
- 43,230
miaka ya 1990 hivi, baada ya kumaliza manunuzi yangu mitaa ya Kariakoo nikawa nakatiza mitaa kuelekea kituo cha Kongo nichukue daladala kurudi nyumbani. Katikati ya hiyo mitaa nikakutana na machinga ameshika blausi mkononi akaniambia elfu nne, kiukweli blausi niliipenda maana fasheni yake ndio ilikuwa imeingia ila mkononi nilibakiwa na shilingi elf 2 na mia tano tuu. Nikaanza kuondoka nikijua siwezi inunua, akaniambia kwani una shilingi ngapi, nikamwambia elf 2 akasema lete nikuuzie. Haraka nikampa hela na kujua kuna kufungiwa kanyaboya nikamwambia usinifungie naondoka nayo mkononi ile nageuka nashikwa bega na kijana mwingine, sista hiyo blausi umeuziwa shilingi ngapi nikamwambia kwani vipi akasema hiyo hela haitoshi ongeza hela au rudisha balusi urudishiwe pesa yako. Nikasema isiwe tabu nipeni elfu 2 yangu niondoke. Kama Mungu ile napewa elfu 2 nikaiangalia kwa macho kumbe nashikishwa kikaratasi cha majaladio yale ya khaki.
Nikapata ujasiri ghafla wa kumshika shati yule jamaa nipe hela yangu nakuitia mwizi sasa hivi, akamwambia jamaa mwingine lete hiyo hela na matusi juu kuwa ulifikiri utapata nguo nzuri kwa bei rahisi hivyo. Niliishika hela yangu mkononi huku naondoka haraka kuelekea kituoni na kila dakika naiangalia ni ela kweli au itageuka kuwa karatasi looh.
Nilipenya tundu la sindano.