Ukitapeliwa usifanye haya. Ni janga!

Ukitapeliwa usifanye haya. Ni janga!

Nilitapeliwa 200k,nilipo gundua nimetapeliwa nilipatwa na hasira Kali alafu baadae nikaanza kumuonea wivu mtu alie nitapeli ( yaani kaingiza 200k mda mfupi tuu) nikaamua na mimi nitoe bank 100k na nikaitumia kwa kula bata ili ieleweke moja kuwa nimepoteza 300k....
Nimecheka kama mazuri eti! Ha ha haaaa
 
Umenigusa sana mkuu,hasa hiyo point 1.Kuna tapeli lipo humu humu jf tena member maarufu na active limenipiga
Najua utapita hapa ila tambua kuwa "karma never loses an adress"
Na ukitapeliwa unakuwa wabaridiiiii.....pole dada!
 
Kutapeliwa kunaumiza sana, kunarudisha nyuma kimaendeleo kunanyong'onyesha,kunaumiza kunakatisha tamaa.hakuna kitu nakichukia kama kutapeliwa na nikishaisigi mtu ana element za utapeli nakaa naye mbali. The good thing about utapeli usitegemee kufanikiwa kimaisha utaishia kwenye utapeli na utaishia jela na hakuna tapeli yeyote awaye alimaliza safari yake kimaisha salama. Jasho la mtu haliliwi hyo ni principle, fanya kazi kwa uaminifu tafuta kwa njia halali usiwadhulimu wenzako ambao wanahangaika kijikwamua kimaisha na Mungu atakubariki pamoja na vizazi vyako vyote.
 
Somo zuri sana,
na 90% ukitapeliwa ujue imepita hiooo..
Wewe kajifungie ulie weeeee......

Watu tumetapeliwa 50M na korosho tumetulia zetu tuuu, wala hatumuendei kwa mganga...
Wewe si unajua utalima tena na kuvuna, potelea twende,

Ulizwe sasa mafao ya uzeeni,

Think twice na urudi tena,
 
We si unajua utalima tena na kuvuna,, potelea twende,,

Ulizwe sasa mafao ya uzeeni,,

Think twice na urudi tena,,
mzee hio comment umeichukulia serious kias hichooo? Sikua na nia hioo...
 
Tapeli usimpe muda kabisa..hata kama unamjua..hamna pesa rahisi

Watu wa Qnet walinitapeli 1m advance pyt..maninaa zao.,
Kuna jamaa kaanza kunitumia mi-link ya matapeli wa dizaini hii ya Qnet, nitakachomfanya atashangaa, ajiandae kunywa supu ya dha-kari yake soon!
 
Kuna jamaa kaanza kunitumia mi-link ya matapeli wa dizaini hii ya Qnet, nitakachomfanya atashangaa, ajiandae kunywa supu ya dha-kari yake soon!
Wala hamna haja ya kuwadhuru
Kikubwa usiwape nafasi ya kuongea nao
 
Utapeli unalipa mno, mtaji ni tamaa zetu.... watu wanapigwa kirahisi mno.
 
SOMO ZURI SANA HILI:
....utapeli ni art ya miaka dahari. Katika maisha zaidi ya 70% ya binadamu duniani wamewahi kukutana na dhahama ya kutapeliwa.

Dakika 5 mpk saa 1 baada ya kutapeliwa mtu huwa anachanganyikiwa. Dopamine yake huwa high na anajiona ni kilaza wa kiwango cha Airbus!

Wengi hufanya maamuzi ya kijinga baada ya kutapeliwa.

Tafadhari usifanye haya!
1. Usiende Kwa mganga wa kienyeji.
Hapa wengi huamua kwenda kuroga. Yaani eidha kurudisha Mali ilopotea au kumkomoa tapeli. Huku wengi huishia kutapeliwa Zaid. Mf kuna rafiki angu alitapeliwa about 6.7M akaenda Kwa sangoma akaishia kupigwa na mganga takribani 12M na hakupata chochote!

2. Kuna huu utapeli wa kupitia simu, issues za Mpesa, madawa, vifaa vya kilimo nk. Watapeliwa hustuka kuwa wameshalizwa baada ya kutuma pesa na mtumiwa hapatikani. Wengine huambulia kulia na kutupa simu. Usitupe simu, wala usipoteze muda kuloga au sijui kujihangaisha. Tulia, let life go. Chukulia kama umelipia tuisheni na Amua kutotapelewa tena.

3. Wanaotapeliwa Kwa kuuziwa Mali fake mf simu, dawa fake, madini feki, mamilioni ya pesa bank, Mali kale nk kupigwa magari nk, usitafute gari mfukoni. Epuka kutaka kujiua . Wewe sio wa Kwanza, wewe sio wa mwisho. Usipaniki. Tulia, tafuta wafariji, usikae peke yako.Kubali matokeo. Jipange kutokulizwa tena.

4. Utapeli wowote usikubali uuondoe utu wako. Bado maisha yanaendelea. Maisha ni ya thamani kuliko Mali yoyote. Mali inapatikana, uhai hauuzwi.

5. Halafu ndugu yangu, Kwa nini ukubali kuurudia utapeli? Acha tamaa ya kuwekeza Tsh 100,000 utengeneze Milion 100. Mali hupatikana kwa hard working.

6. Kuna wanaoamua kuwa matapeli baada ya kutapeliwa. Hapa sasa nikuambie ndugu, two blacks never make one white! Utaishia pabaya.

7. Jipe muda wa kujifunza njia mbalimbali za kutapeliwa na uziepuke. Hapa JF watu wamesimulia Sana walivyotapeliwa. Sasa wewe ukisoma unajifunza nini? Bado unaibiwa Kwa njia ya wizi ulosoma hapa?

8. Matapeli wa njia za madawa ya kichawi si wa kuamini. Kila utapeli ni suala la kucheza na akili yako tu! Yes, kuna Dawa za kitaalam za kupumbaza! Jiepushe na watu usiowajua. Asikushike wala kukukalibia kizembe. Ukigundua ni tapeli mbutue haraka!

9. Fahamu kuwa HAKUNA MTU ASIYEKUJUA atakayekupa utajiri. Kwa nini akutajirishe wewe mtu baki? From no where akuambie mtumie 2M akupe deal la 50M??? Unaamini hii trick ya tangu Zama za mawe za kati? Ndo pale unajikuta mtu kalamba 2M yako then unaachiwa mawe au magazeti kwenye brifkesi! Yaani aache kumpa utajiri mke wake au mdogo wake akutajirishe wewe wa Nanjilinji? Thubutuu!

10. Dawa ya tapeli ni kutompa muda. Kuna watu wanajifunza utapeli 10 good years. Sasa we umpe dk 10 zako si unalizwa?
Acha kushinda Instagram basi, pitia hata clips za Bongo Dar es salaam ujifunze wenzako wanaovyolizwa na we usilizwe!

11. Ukitapeliwa usiwe msiri au kutunga uongo mf eti umepoteza au sijui umevamiwa, no! Washirikishe wengine umelizwaje ili na wao wasilizwe! Sharing is caring! Ukikaa nalo moyoni litakutesa! Funguka!

12. Wastaafu: Ninyi huwa ni target kubwa ya matapeli, kuna timu kabisa kama kampuni ya kuwaibia. Huko kwenye hili jeshi la shetani kuna watu huvaa uhusika kama mashehe, mapadre, masista, wachungaji, usalama wa taifa, wanajeshi, Polisi, madaktari, wanasheria, mainjinia, mabwana misitu, mabwana mifugo na Kada zote uzijuazo ili tu kukuaminisha kuwa ni watu sahihi kumbe wapigaji, wakishamaliza kabisa Ile shilingi ya mwisho kwenye akaunti yako, hutawaona tena!

We ukipata pesheni tu, usimwamini mtu! Kula na familia yako usubiri kujirudishia faili Kwa Israel. Usifanye biashara ambayo hukuwahi kufanya, utapigwa tu na utakufa Kwa mistress Mzee wangu!

Sikio la kufa halisikii Dawa, dunia kila Siku ma-ndaza na mazwazwa au mburura wanazaliwa daily, kuna mtu dakika hii analizwa kiboya tena!!

Ndo maana US wanaruhusu kuwa na Gun! Hapa Bongo wakiruhusu tu nafuata AK 47 pale Mzinga natembea nayo 24/7, ukiniletea stories za sijui uniuzie rupia nipige 200M naku-shoot ya mdomo (cha ajabu kuna matapeli yenye pHD yanakuliza mpk bunduki yako)

Ene Wei, ukiuziwa sabuni ya mbuni kwenye housing ya iPhone usiitupe, kaogee!


Stuka!!!
 
Back
Top Bottom