Ukitaka ukosane na rafiki omba akukopeshe fedha..
Siku mbili tatu zilizopita nilipata changamoto kidogo za kiuchumi,kutokana na mambo ya ujenzi....wajuzi wanasema zege hali lali,nikajishauri nikaona ngoja niombe fedha ya dharura kwa marafiki zangu.Majadiliano yakawa hivi:-
Mimi: mambo vipi mkuu?naomba unisaidie kiasi fulani cha dharura by alhamisi nitakurudishia hata kwa riba.
Rafiki 1: Sawa haina shida kaka nitakucheki baadaye
Baada ya hapo kimya,ukimpigia simu hapokei
Rafiki 2: Ok nitakupatia kesho
Kesho inafika kimya,ukimpigia simu hapokei
Rafiki 3: Siko vizuri kiuchumi,biashara zimesimama kaka
Bora huyu alikuwa muwazi na nilimuelewa
Rafiki 4 : Siko vizuri kaka,nitakupatia nusu yake
Mimi: Nashukuru nilikuwa naitaji full
Kutokana na hali hiyo,nilichoweza kujifunza ili usikosane na rafiki yako inabidi mahusiano yenu yasihusu mambo ya fedha.