Mimi naona,mtu kama hujaridhika na malipo ya sehemu unayofanyia kazi, ni bora ukacheki issue zingine kuliko kupoteza muda wako au kuharibu kazi za watu coz mpaka unaanza hiyo kazi lazima utakua umesign contract au umekubaliana na muajiri wako,
Kufanya kazi kivivu hakuwezi kubadili chochote kisa unalipwa kidogo bali kinaweza kukusababishia hata hicho kidogo ukakikosa,
Mtu mvivu hata umlipe mshahara anaoutaka,atabadilika kwa muda tu ila ile hali yake ya uvivu na kutokuwajibika itarudi pale pale,uwajibikaji na kujituma ni tabia.
Piga kazi,timiza majukumu yako ipasavyo, Mungu atakuona tu na malipo yako utayapata tu,kama sio hapo ofisini kwako basi Mungu atakupa kazi bora zaidi hata sehemu nyingine, juhudi na kujituma hua haziendi bure,piga kazi huku ukimtegemea Mungu, hawezi kukutupa,jasho la mtu haliendi bure, jijengee tabia ya kujituma na uwajibikaji ni jambo zuri hata kama utaamua kufanya kazi zako binafsi.