Ukistaajabu ya tozo, tazama wafanyabiashara tunavyoumizwa na serikali

Tofauti ipo dmkali hawa wanalindwa na sheria wale dhamana za mahakamani...yaani mtu anatoka huko kwenye kikao eti cha Tozo ya bando akiamka bank akiamka sijui viingereza vya Railway Levy hawataishia hapo hawa...
Dawa yao siku ni kugoma mgomo mzito kama Sri lanka
 
Yaan utitiri wa kodi mpaka mtu unafikria au bora niajiriwe labda cku moja ntapata mwanya nami niwe kati yao? Mana if you cant fight them, then join them.
 
Dawa yao siku ni kugoma mgomo mzito kama Sri lanka
Yap kama itawezekana ni hatari sana aisee hii ya Bank sikuwahi kufikiri kama inaweza kuwepo lakini nilivyoona ishu ya mafuta walivyoichezea nikajua pana ujinga mwingi utaongezeka...mafuta yamepanda bei badala ya kufuta baadhi ya kodi wao wakashauri waweke ruzuku ya 100 Billion kipo wapi hali ni vile vile...
 
Kibongo bongo kufanya biashara bila kupiga kona kona,hutoboi kamwe.
 
Alafu Kuna mbuzi inasema toa risiti yaani sitoi nitafanya where necessary!! Nchi ya hovyo sana hii Kila mtu ashinde mechi zake.
 
Alafu Kuna mbuzi inasema toa risiti yaani sitoi nitafanya where necessary!! Nchi ya hovyo sana hii Kila mtu ashinde mechi zake.
Bidhaa moja inakodi 10 unatoaje risiti sasa! Haivutii hata kuwa mzalendo
 
Tozo ni mchango wa maendeleo, na kodi ni kwa mujibu wa sheria!
Inabidi tuwakumbusha watunga sheria wetu, hawa wengine tunawaonea bure maana ni watekelezaji wa sheria zilizotungwa na bunge
 
Tozo ni mchango wa maendeleo, na kodi ni kwa mujibu wa sheria!
Inabidi tuwakumbusha watunga sheria wetu, hawa wengine tunawaonea bure maana ni watekelezaji wa sheria zilizotungwa na bunge
Bunge la wananchi, lakini maslahi ni yetu hayasikilizwi
 
Kuna wakati unapata stress mpaka basi ila ndio hivo huwezi kuacha.
Mbaya zaidi ukute unafanya zile biashara ambazo mpaka ufanye lazima uwe na kibali ndio utajua hujui.
Na wasione sehemu kuna fursa ya kupata pesa watakuandama hao wala hawana huruma yaani wanapokezana au kuambiana huku wakijifanya wanakusaidia upate ahueni kumbe wanakutafuna.Hao hata biashara ya pipi hawajawahi fanya waujue uchungu na msoto wa biashara kazi kupenda vya bure na ndio mana wanakuwaga na mwisho mbaya.
Mtu yeyote anayefanya biashara anaelewa changamoto na lazima amuelewe mfanya biashara mwenzie ila hao ambao hawajui wala hawajawahi wakiona unafanya wanaona unapata sana kumbe masikini tunakaza roho.
Sometimes huwa natamani nipate ajira niwe na mimi nasubiria mwisho wa mwezi kuliko hizi heka heka.
 
Nasikia story ya Hamza chimbuko ilikuwa hivyo
 
Yote tisa wananchi hii mitandao pia inapiga sana hela wanakata mara 12 zaidi ya tozo. Serikali iingilie kati.
Makampuni ya kigeni yanajinufaisha sana.kupitia makato yao.....
 
Yote tisa wananchi hii mitandao pia inapiga sana hela wanakata mara 12 zaidi ya tozo. Serikali iingilie kati.
Makampuni ya kigeni yanajinufaisha sana.kupitia makato yao.....
Wala hakuna msikilizaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…