Ukiona magoti yanamgonga ujue anajigonga.........

Rutashubanyuma hakika wasifika kwa kipaji
Kutoa yalo moyoni kuyaweka kwenye maandishi
Twashukuru kwa chako kipaji utenzi kukamilika
Moyo hauna subira ijapo kwa kiasi
 
Ruta ingekuwa wanadamu tumeumbwa kwa vioo ingekuwa rahisi sana kujua nini mawazo ya moyoni mwake. Lakini pia ingawa ni rahisi kwa binadam kubadilika na kuwa na usiri mkubwa inakupasa uwe na imani tu kwamba kama mm nawaza hivi juu ya mwenzangu basi nayeye anawaza the same. mengine ya sirini mwachie maulana anayejua kusoma siri za mioyoni mwa viumbe wake.

tena mwogope sana yule anayejigonga manake yupo anayefanya kwa maigizo tu, but if you are keen enough read a person from his redges
 
Moyo wa mtu ni kiza, tena ni kiza kinene
Mengine anaigiza,yana ladha ya senene.
kwa kina ukichunguza, yote yana rangi nane,
magoti yanahadaa

Siye wa zama zile, zama za kibaba na namba saba
twayajua mazongile,mapenzi hayana nasaba,
aso hili ana lile,magoti hayajui huba.
Anakuzuga
Rutashubanyuma acha, acha kucheza na mwili,
kuna vitu unaficha,mwili ni ndumila kuwili,
asikuzuge kwa kucha, cheza na macho mawili
Macho yana siri nyingi
BADILI TABIA funguka,sema kilicho moyoni,
macho yetu hupofuka, penzi likiwa akilini,
Magoti siyo kidaka.kichoracho ya moyoni
Amedanganywa

Ama wasemaje Kaunga,yupi asali ya moyo?,
yule anayejigonga,au mwenye hisia za choyo?
Mapenzi ni kuungaunga,siyo ndiyo siyo siyo
Usiyachunguze.

Naichukia mipasho, tangu mwanzo hadi mwisho,
Hata dada Kongosho,kama ni wake utambulisho
Nampa kisahihisho, nyayo hazina ganganisho
Hazigongani
 
Last edited by a moderator:
Ama wasemaje Kaunga,yupi asali ya moyo?,
yule anayejigonga,au mwenye hisia za choyo?
Mapenzi ni kuungaunga,siyo ndiyo siyo siyo
Usiyachunguze.

Eti nisiyachunguze?
Nilitumia yako kanuni, hapo nyuma kitambo.
Kuyaachia ya moyoni, bila tegea ulimbo.
Kutendwa sana jamani, hadi maumivu ya tumbo.
Sasa nimekuwa jumbo, wa machale mapenzini!

Rudia tena nisiyachunguze?
Moyo wampa mpenzi, ukitegemea mapenzi.
Waambulia majonzi, na kuishi katika njozi.
Sitasubiri fumanizi, nachunguza kwanza penzi.
Asante kwa utenzi, ingawa sikubaliani na pozi.

Kigarama wasemaje...nisiyachunguze!
Kanuni yangu ya sasa, nimpende akupendae
Sitajitia utasa, kung'ang'ania kwa nisonae
Kuchunguza kisasa, ndio mpango endelee
Wa furaha ukelele, pale kasoro unapokosa
 
Eti nisiyachunguze?Rudia tena nisiyachunguze?
wasemaje...nisiyachunguze!

Ndiyo usiyachunguze Kaunga usiyachunguze,
Na mapenzi siyo zeze,nyimbo zake uzicheze,
kwenye huba usiwekeze,utelezi njia zake
Usichunguze usiteleze

Mapenzi rangi rangile,wenye nayo mizukule,
Uyaonayo siyo yale,mtima ujifungile,
ikifika siku ile,hakutakuwa simile,
Uonacho ndiyo hicho.

Akisema nakupenda, hewala kwa muungwana,
ushahidi kakupenda, anajua maulana,
kuchunguza kakupenda, huko ni kutafutana
Usichunguze
 
Akisema nakupenda, hewala kwa muungwana,
ushahidi kakupenda, anajua maulana,
kuchunguza kakupenda, huko ni kutafutana
Usichunguze

Ninaomba unifahamishe, kaka yangu Kigarama,
Kwanini asinioneshe, mapenzi yake anayosema,
Au kwanini nimuonjeshe, ilhali ampenda Neema,
Na nisubiri kutemwa, ka bigG kwa karanga muonjeshe.

Kabla ya kumpa tunda, ni lazima kuchunguza,
Kama kweli anipenda, kwa nilivyoweka vigeza,
Na penzi kulilinda, anapotimiza vigeza,
Sitapenda kumpoteza, Mpenzi nilompenda.

Kuchunguza muhimu, kwa kila binadamu,
Hii tofauti muhimu, na viumbe waso wa Adamu,
Mapenzi yawe ya hamu, kama ndugu wa damu,
Nitampigia simu, kumswalisha swali gumu.

Aseme ka anipenda, na nimkwoti jibu lake,
Ili kesho akinitenda, nimkumbushe jibu lake,
Najua hatopenda, ila itamtesa dhamira yake,
Nachunguza pendo lake, ili afaidi langu tunda.
 
Last edited by a moderator:
Huba si kitu rahisi, Kaunga unielewe,
wala si jambo jepesi, kama unyoya wa mwewe,
Huba ni kama yabisi, mpendao muelewe,
Hakuna ajue anapendwa.

Kinywani kinachotoka, nani mwenye dhamana?
Anasema anachotaka, moyoni kimejazana?
wewe unachokishika,ni kile unachoona
Amini uambiwacho

Tangu zama za mababu, mapenzi siyo dhahabu
Mapenzi yana adhabu, tena haya adabu,
Yana ladha ya zabibu, mwishoni yana shurubu,
Amini uambiwacho

Kama mtu kakupenda, si angalie matendo,
Maneno yaweza pinda, moyoni ana upendo,
Matendo yakikushinda, ng'ang'ania kwenye pendo
Usiuache upendo

Atendendayo si anenayo, si kigezo cha kupenda,
anenayo ni ya moyo, atendandayo ni ya punda,
wewe angalia moyo, mapenzi utayashinda
usiyachunguze
 
Kigarama kaka yangu, nitakujibu baadaye
Ninao uzoefu wangu, ndani ya hili pendole
Naingia jikoni kwangu, nikapike ndizi nile
Mapenzi ni ulele?, ntamuuliza kaka KIKUNGU

NB
Ulele ni kinyamwezi maana yake ujinga si eti Sikonge?
 
Last edited by a moderator:
Kigarama kaka yangu, nitakujibu baadaye
Ninao uzoefu wangu, ndani ya hili pendole
Naingia jikoni kwangu, nikapike ndizi nile
Mapenzi ni ulele?, ntamuuliza kaka KIKUNGU

NB
Ulele ni kinyamwezi maana yake ujinga si eti Sikonge?

Mapishi uyapikayo, mola ajaze fanaka,
wale washibe walao, na wakombe wakitaka,
wewe si mwana mchoyo Kaunga ninatamka,
salheri!!
 
Last edited by a moderator:
Siyo rahisi kujua kilichoko ndani ya moyo wa mwanadamu
Mara nyingi kauli hupimika lakini kamwe siyo dira ya ukweli
Jicho laweza kurashiarashia nia lakini siyo kisemea moyo
Tabasamu laweza kukutikisa lakini lisitoboe la moyoni
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.

Kilichoko moyoni ni kificho japo chakuchungulia-chungulia!
Mtihani wako ni kutafakari moyoni kwake kuna nini lakini?
Lengo ni kuujua moyo wake ili uthibiti hila kama zipo
Mwanadamu asilia yake ni usiri na usibwatuke na siha...
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.

Moyo wa mwanadamu ni pasua kichwa na hata mmilikiwe kuzuzuliwa!
Anachodhani kipo moyoni leo, kesho kukikana yeye mwenyewe!
Moyo wa mwanadamu ni kizungumkuti kamwe usiuamini!
Kwani umekithiri hila na vitimbi, hivyo, kuwa tatanishi!
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.

Mwanadamu hapendi kuanguka hivyo magoti kuyalinda vyema.
Sasa magoti yanapoweweseka ujue umemshika pabaya.
Hana ujanja wa kujitunzia siri hapo kwani hata wewe shahidi.
Chunga magoti yake na wala siyo moyo wake kuujua undani wake.
Walakini magoti yanapomgonga-gonga ujue kweli anajigonga.

Magoti yakigongana mbele yako ujue hana ujanja tena kwako.....
Na ya kuwa umemtia kabali na kibanio hicho hatoki kamwe!
Kufurukuta kamwe hawezi na saa ya kumkokota imewadia..
Mpeleke kichinjioni ili ufaidi kitoweo kabla hajageuza somo!
Walakini magoti yanapomgonga-gonga ujue kweli anajigonga.

N.B Haya siyo mashairi bali ni tenzi za nyimbo...........kwa hiyo hakuna swala la vina kushahibihana n.k kama ummu kulthum anavyopendelea na wengineo.....sentensi ya mwisho ni kibwagizo tu au chorus/kiitikio n.k

nimegonga like na kamchina. . .upo juu!!
 
Ni kweli kabisa @Kaunga. Kuna ule wimbo "ulilele Ulilele nkima/ngosha/nyanda/nsumba - Masala kuduhu".
Kigarama kaka yangu, nitakujibu baadaye
Ninao uzoefu wangu, ndani ya hili pendole
Naingia jikoni kwangu, nikapike ndizi nile
Mapenzi ni ulele?, ntamuuliza kaka KIKUNGU

NB
Ulele ni kinyamwezi maana yake ujinga si eti Sikonge?
 
ummu kulthum is too lovely and a hot subject for now...................sijui kama anahusika na huu uzi wa leo mie nimeutapika tu kwa manufaa ya jf nzima.......................

ndetichia, si umeona rutashubanyuma anavyojitetea kama kuku mwenye mdondo?by the way kijana unanifurahishanga wewe,na mashairi yako yasiyo na vina keep it up!!!
 
Ruta, kauga and kigarama mmenifanya nisahau mengi niwaze zenu fikira ambazo najiuliza huwa mnawezaje kuyapata haya mashairi? binafsi sijui hata kutunga kawimbo ka kumbembeleza mtoto u can imagine jins ambavyo nawafeel kwa haya mashairi. keep it up
 
gfsonwin sifa zako namba wani, haya si ya kustaajabu
Elfu huanza na namba wani, vijana nao huwa babu,
roho yako usihini, kushindwa nyambua silabu,
utaweza

Eti Rutashubanyuma, unajua wakufeel
nenda usirudi nyuma, usiache jambo hili
tunga tungo zenye nyama, zenye lugha si dhalili,
unapendwa

Nawe Kaunga, wenzio wakutamani,
wanataka kujiunga, waje kwako chamani
tatizo lao kutunga, wajue wafanye nini?
waeleze
 
Honey, hata mimi naafikiri leo ni mara ya pili tu. So if l can try it hata weye waweza.
Ila Kigarama kanitoa no count, ngoja nitamuamkia alfajiri wakati kichwa kiko fresh!
 
Last edited by a moderator:
Kaunga bwana, umeniacha nacheka,
kumbe umeshindwa vina,muwala ukaibuka,
Hoja zako si za tina, wala hazina shubaka,
Gangamala
 
Last edited by a moderator:
Kaunga bwana, umeniacha nacheka,
kumbe umeshindwa vina,muwala ukaibuka,
Hoja zako si za tina, wala hazina shubaka,
Gangamala

Usijione mshindi, ni break tu nahitaji,
Kila kitu kwa kipindi, muulize hata Buji,
Alfajiri nitarudi, kuendeleza hii ligi,
Karibu kwa friji, poza koo kwa mtindi.
 
ummu kulthum is too lovely and a hot subject for now...................sijui kama anahusika na huu uzi wa leo mie nimeutapika tu kwa manufaa ya jf nzima.......................
ndetichia, si umeona rutashubanyuma anavyojitetea kama kuku mwenye mdondo?by the way kijana unanifurahishanga wewe,na mashairi yako yasiyo na vina keep it up!!!

Yaani ummu kulthum...wewe wacha fujo kabisa.........vina vya nini la muhimu si kuburudika na kulipata somo tu?
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin sifa zako namba wani, haya si ya kustaajabu
Elfu huanza na namba wani, vijana nao huwa babu,
roho yako usihini, kushindwa nyambua silabu,
utaweza

Eti Rutashubanyuma, unajua wakufeel
nenda usirudi nyuma, usiache jambo hili
tunga tungo zenye nyama, zenye lugha si dhalili,
unapendwa

Nawe Kaunga, wenzio wakutamani,
wanataka kujiunga, waje kwako chamani
tatizo lao kutunga, wajue wafanye nini?
waeleze

Kigarama leo nilitaka nipumzike lakini kwa hii mi saif sina namna itabidi nidondoke na tenzi nyingine......mie vina sina khabari nao kama naweza kufikisha ujumbe na kuburudihs wasomaji hapa JF...............that is enough for me..........
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom