Ukiona magoti yanamgonga ujue anajigonga.........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Siyo rahisi kujua kilichoko ndani ya moyo wa mwanadamu
Mara nyingi kauli hupimika lakini kamwe siyo dira ya ukweli
Jicho laweza kurashiarashia nia lakini siyo kisemea moyo
Tabasamu laweza kukutikisa lakini lisitoboe la moyoni
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.

Kilichoko moyoni ni kificho japo chakuchungulia-chungulia!
Mtihani wako ni kutafakari moyoni kwake kuna nini lakini?
Lengo ni kuujua moyo wake ili uthibiti hila kama zipo
Mwanadamu asilia yake ni usiri na usibwatuke na siha...

Moyo wa mwanadamu ni pasua kichwa na hata mmilikiwe kuzuzuliwa!
Anachodhani kipo moyoni leo, kesho kukikana yeye mwenyewe!
Moyo wa mwanadamu ni kizungumkuti kamwe usiuamini!
Kwani umekithiri hila na vitimbi, hivyo, kuwa tatanishi!

Mwanadamu hapendi kuanguka hivyo magoti kuyalinda vyema.
Sasa magoti yanapoweweseka ujue umemshika pabaya.
Hana ujanja wa kujitunzia siri hapo kwani hata wewe shahidi.
Chunga magoti yake na wala siyo moyo wake kuujua undani wake.
Walakini magoti yanapomgonga-gonga ujue kweli anajigonga.

Magoti yakigongana mbele yako ujue hana ujanja tena kwako.....
Na ya kuwa umemtia kabali na kibanio hicho hatoki kamwe!
Kufurukuta kamwe hawezi na saa ya kumkokota imewadia..
Mpeleke kichinjioni ili ufaidi kitoweo kabla hajageuza somo!
Walakini magoti yanapomgonga-gonga ujue kweli anajigonga.

N.B Haya siyo mashairi bali ni tenzi za nyimbo...........kwa hiyo hakuna swala la vina kushahibihana n.k kama ummu kulthum anavyopendelea na wengineo.....sentensi ya mwisho ni kibwagizo tu au chorus/kiitikio n.k

Siyo rahisi kujua kilichoko ndani ya moyo wa mwanadamu
Mara nyingi kauli hupimika lakini kamwe siyo dira ya ukweli
Jicho laweza kurashiarashia nia lakini siyo kisemea moyo
Tabasamu laweza kukutikisa lakini lisitoboe la moyoni
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.

Kilichoko moyoni ni kificho japo chakuchungulia-chungulia!
Mtihani wako ni kutafakari moyoni kwake kuna nini lakini?
Lengo ni kuujua moyo wake ili uthibiti hila kama zipo
Mwanadamu asilia yake ni usiri na usibwatuke na siha...
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.

Moyo wa mwanadamu ni pasua kichwa na hata mmilikiwe kuzuzuliwa!
Anachodhani kipo moyoni leo, kesho kukikana yeye mwenyewe!
Moyo wa mwanadamu ni kizungumkuti kamwe usiuamini!
Kwani umekithiri hila na vitimbi, hivyo, kuwa tatanishi!
Walakini magoti yanapomgonga-gonga jua kweli anajigonga.

Mwanadamu hapendi kuanguka hivyo magoti kuyalinda vyema.
Sasa magoti yanapoweweseka ujue umemshika pabaya.
Hana ujanja wa kujitunzia siri hapo kwani hata wewe shahidi.
Chunga magoti yake na wala siyo moyo wake kuujua undani wake.
Walakini magoti yanapomgonga-gonga ujue kweli anajigonga.

N.B Haya siyo mashairi bali ni tenzi za nyimbo...........kwa hiyo hakuna swala la vina kushahibihana n.k kama ummu kulthum anavyopendelea na wengineo.....sentensi ya mwisho ni kibwagizo tu au chorus/kiitikio n.k

Rutashubanyuma we mkare ya hiyo yote ni kwa sababu ya ummu kulthum
 
Last edited by a moderator:
ni kweli ndugu yangu moyo wa mwanadamu ni kizungumkuti leo waona hivi kesho umebadilika

chavka.......uko juu sana................sina la kuongezea zaidi ya kusema chunga magoti yake kama yanaweweseka......
 
Last edited by a moderator:
Sasa Rutashubanyuma, last week ulisema utampenda yule tu anayekupenda. Big question ni utajuaje kama anakupenda; kwani maneno, wala macho yake havielezie yaliyo moyoni.

Na hiyo ya kujigonga, haiwezi kutafsiriwa as kuwaka tamaa tu?
 
Kaunga uko juu sana....................ni kweli kujigonga kwaweza kuwa ni kuwaka tamaa au kupenda...........lakini unakuwa umeanza kupunguza maeneo yenye utata ambayo mhusika hawezi kuyapangilia vinginevyo...........................next week nitaongelea baada ya hatua hii what next.......................you almost took my next week love song away from my schedule partially because you keep on reading between my finer of the finest print........................I have to be careful next time............LOL
 
Ofcoz kujigonga kuko both sides, si kwamba wadada tu ndiyo hujigonga kwa wakaka.
Na ndivyo maumbile yanavyotupelekea,
kwani haiyumkini ukajigonga kwa mwenza wa gender ifananayo na yako.
"wayajua mahanjamu ya chuchu weyee ?"
 
mkuu kila naposoma post zako huwa naenjoy sana duuu!

Henge..........thanx a lot...........it is a pleasure to entertain others in a light touch, of course............
 
Last edited by a moderator:
Ofcoz kujigonga kuko both sides, si kwamba wadada tu ndiyo hujigonga kwa wakaka.
Na ndivyo maumbile yanavyotupelekea,
kwani haiyumkini ukajigonga kwa mwenza wa gender ifananayo na yako.
"wayajua mahanjamu ya chuchu weyee ?"

Judgement hapo kwenye nyekundu hebu tukumbushane.........kulikoni................
 
Last edited by a moderator:
RUTA ilike u.. yaan ww hdari sana,, unajua kupangilia mistari. NA watu wanasema MUOGOPE MWANAADAMU KWA AKILI YAKE USIOGOPE MANENO YAKE,, kama ushair wako kuwa hujui mtu kilichomo moyon mwake anawaza nn, hongera mkuu mm nmekukubali
 
Back
Top Bottom