Ukiombwa pesa ya soda unatoa shilingi ngapi?

Ukiombwa pesa ya soda unatoa shilingi ngapi?

Attachments

  • index.jpg
    index.jpg
    9.3 KB · Views: 11
Juzi nilikua zangu nmekaa sehemu nakula rost ya kitimoto na Red Wine , wakati naendelea kula pale ghafla akatokea dada mmoja ambae ni jirani yangu lakini hatuna mazoea kivile, nikamsalimia akaitika, nikamkaribisha aje kula (Kama mnavyojua wabongo unamkaribisha tuu mtu kimazoea mda mwingine hatumaanishi)

Akavuta kiti akakaa, nashangaa anamuita muhudumu "Muuudumu niletee Glass na tishuuu! "nikashangaa sana, Wine yangu nilitaka ninywe mwenyewe sasa imepata muhuni tunaipiga mande!, nikasema sio tabu, Glass ikaletwa tukawa tunakunywa huku tunapiga story.

Kiukweli Dada aliniboa sana, ananiletea story nyingi, mara aniambie "hapa kuna vyumba ujuee"

Kiukweli mimi sipendi mtu aniongeleshe sana hua nasikia kama kichwa kinauma.

Nilimaliza kula, nikapiga glass moja ya mwisho, nikanawa, nikamuita muhudumu nikalipa bili, nikamuaga yule dada nikamuacha na chupa ya wine pale anywe.

Nashangaa naondoka ananishika mkono eti anataka nimuachie hata ya soda, nikasema sio shida, kwakua nilikua na chenchi nikampa 500 ya Coin akanywe hiyo soda, alitoa macho kama kapigwa shoti, kwa mawazo yake sijui alijua nitampa shingapi.

Mambo mengine bana.
Alikuwa anahitaji chakula, watoto waliokulia uswahilini huwa wako wazi namna hiyo hawazunguki zunguki kama ana shida, hasa kama ni ya chakula. Ila wewe nawe pia unaonekana ni mchoyo sana na amekuumiza sana hasa kwenye swala hili la malaji. Yeye alidhani kakuktana na mtu wanayefahamiana angalau atapata chochote, kaambuliwa 500 pamoja na kuja kutangazwa kwenye mtando wa jamii unaosomwa dunia nzima. Nampa pole sana huko aliko. Next time ukikutana na hali kama hii, jaribu kutumia hekima kidogo, hasa kutokutangaza kile ambacho umemfanyia mtu, kiwe kizuri au kibaya.
 
😂😂😂😂😂 wengine huomba “hela ya soda” lakini ukweli ni kwamba hajala hivyo anaomba pesa ili apate mlo. Mimi inategemea muombaje kaombaje, lakini kwa kujua muombaje anaweza kuwa anaomba pesa ya kula mara nyingi hutoa elfu 10.
Aseme, hela ya kula sio ya soda. Hivi unadhani Dr Hellen Bisimba atakuomba hela ya soda akimaanisha ujiongeze umpe ya kula???? Yule mama yuko straight forward, mabinti wanatakiwa kuwa straight forward.......sio kuleta ujinga hapa kama wanawake wa mererani ' eti naomba hela moja' akimaanisha 10,000/= puuzi kabsa.
 
Kila mtu ana style yake ya kuomba hivyo usilamizishe waombe vile utakavyo wewe. Mie nina uzoefu wa kusaidia watu mara nyingi tu na baadhi hufunguka kwa kukuombea dua chungu nzima huku wakisema hawajala siku 2 au zaidi japo waliomba hela ya soda.

Aseme, hela ya kula sio ya soda. Hivi unadhani Dr Hellen Bisimba atakuomba hela ya soda akimaanisha ujiongeze umpe ya kula???? Yule mama yuko straight forward, mabinti wanatakiwa kuwa straight forward.......sio kuleta ujinga hapa kama wanawake wa mererani ' eti naomba hela moja' akimaanisha 10,000/= puuzi kabsa.
 
1000 inatosha inayobaki atahifadhi na yeye wanasema keep chenji
 
Back
Top Bottom