Sijielewi elewi; kimsingi sijawahi kukaa na pesa zaidi ya wiki moja, nakuwa nimeshaivuruga yote

gidume

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
662
1,000
Wakuu kwema?

Sijielewi elewi, kimsingi sijawahig kukaa na pesa zaidi ya week moja, nakua nimeshaivuruga yote hata iwe kiasi gani.

Kisa kilichonifanya nije na hii mada.

Majuzi kama mwezi mmoja umepita baada ya shughuli zangu zote kugoma nikasema sbr niuze ka ofisi changu..na kweli nikafanikiwa kupata mteja tukafanya biashara kwa sababu najijua mimi pesa yangu huwaga haidumu mifukoni kwangu nikasema sbr nianze kuiallocate sehemu tofauti ili adi iishe atleast niwe na kitu cha kusema nimefanya na kikainua kitu kingine.

Nilitaka niiamshe ofisi nyingine ambayo nilikua naona itanipa matumaini ambayo pia niliifunga kutokana na ukosefu wa ukwasi hivyo nikawa nayo nataka niiuze hivyo ikawahi hii kutoka. Nikawa nna kama mil 6 kwa bei ya kuiuza, ghafla akaja mteja akapanda dau kwenye gari yangu nnayotumia mil 15 nikasema nisiache pesa sbr niuze, jumla nikawa na mil 21,000,000 kwenye account.

Nilivyoona vile nikajiapiza sitokaa na njaa tena maishani mwangu labda niwe sio mimi na familia yangu sasa itaanza kula matunda ya uwekezaji mdogo niliopitia changamoto kujikusanya miaka mitatu au minne iliopita.kwa sasa nna miaka 32 tu.

Ghafla baada ya kupata ile pesa nikaona gari nzuri kweli inatangazwa kwenye mtandao inauzwa mil 17... nikaipandia basi kuifata nikanegotiate kwa mil 16 wakakubali nikawalipa nikarudi kuendelea na maisha yangu.

Zikabaki kama tsh mil 4,500,000 ukitoa mambo mengine ya matumizi na vitu vingine.

Nilivyorudi nikaanza kuhudumia ofisi ile nyingine nikalipa kodi za ofisi zangu na kufanya mambo mengine.

Kuna siku nikatoka weekend na warembo kujipongeza nikatumia kama laki mbili na shopping kiasi kwa mambo ya ndani..ya vitu visivyo vyakula.

Nakumbuka hela ya mwisho imeisha naitumia nategemea kuna deal linatick bahati mbaya lile deal halijatick.

Sasa nimerudi upyaaa kwenye umaskini yani adi sasa kwenye account inasoma tsh 12,000/=na leo nalumangia ugali na soda ya juzi nilioacha kwenye fridge.

Sasa najiuliza hili ni janga langu au wengine mnatumia njia gani kuhifadhi pesa zenu msizitumie hovyo.

Naendesha gari ya gharama mtaani najulikana nna pesa kumbe nalala na njaa.

Nimewaza niiuze tena hii gari..je haitatokea nikiuza nizitafune hizo pesa kimazingara kama nilivyozifanya hizi mil 5? Maana hazijamaliza ata siku tano zimeisha adi to 12,000/= balance ambayo huwezi ukatoa .

Kitu kibaya zaidi napenda sana kuishi kibabe, yani kutumia vitu expensive kama magari ndo ugonjwa wangu kulingana na nilivyojiwekeza. Mind you kwa sasa sina kipato cha namna yoyote zaidi nilitegemea niinue hiyo ofisi lakini nashangaa ata kukamilika haijakamilika na pesa zimeniishia.

Kazi nilishaacha sababu ya figisu na manyanyaso ya boss, nikasema kwa jinsi nimejiwekeza sbr nijaribu kujisimamia lakini nimekuja kugundua sina hicho kipaji.

Tushauriane jinsi ya kusave pesa maana naona umaskini unaniita..nimeuza vitu vingi sana..kuweka bond ndo usiseme vingine nimeshindwa kuvitoa na mingineyo.

Namuonea huruma mtoto wangu bado mdogo ana miaka mitano lakini na yeye anapenda sana quality life nisije nikamkosesha huko mbeleni kuishi maisha atayopenda.

Au kuna chuma ulete apa kati maana naogopa ata kuhighlight matumizi. Nafsi haitaki kuyapitia ili nione nilitumiaje.

Mbona hatari

Nawasilisha...
 

BMWsimba

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
329
500
kikubwa angalia usipate depression, maana mda sio mrefu hao unaowavimbia hutosubutu kuonana nao tena, maana utakuwa umefulia na itakuwa zamu yao kukuzomoe, hata kama hawatakuwa wanakuzomoe utahisi unazomewa.
 
  • Thanks
Reactions: Luv

gidume

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
662
1,000
kikubwa angalia usipate depression, maana mda sio mrefu hao unaowavimbia hutosubutu kuonana nao tena, maana utakuwa umefulia na itakuwa zamu yao kukuzomoe, hata kama hawatakuwa wanakuzomoe utahisi unazomewa

Rejea kwenye aya inayoanzia nimewaza niiuze hii gari alaf unipe jibu la kigentleman.
 

Tarakwa

JF-Expert Member
Apr 19, 2017
718
1,000
Unaonekana umelelewa kwenye maisha ya mboga saba. Sasa umefikia umri wa kujitegemea. Umeona Pesa ilivyo ngumu?!
 

gidume

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
662
1,000
Unaonekana umelelewa kwenye maisha ya mboga saba. Sasa umefikia umri wa kujitegemea. Umeona Pesa ilivyo ngumu?!

Hata hivi nilivyokua nayo sikupewa mkuu nimetoa jasho, nimesota sana kuvipata, nimekopa na nimerejesha. Lakini hii force ya kuisha inanizidi umri.
 

oldwine

Senior Member
Dec 30, 2020
118
250
Unavosema kwa sasa una miaka 32 tu una maanisha kuwa unajiona mtoto bado au?

Na hapo una mtoto wa miaka mitano?

Anyways, kiushari wangu hiyo spending smtimes inatokea. Na afterwards unajilaumu kweli. Maana yake ni kwamba una consciense na hii ni akili. Maana yake ukizingatia next time hautaspend vibaya.

Kikubwa zaidi naona walau sehemu kubwa ya pesa 17M unajua umeiweka wapi. Na unaweza kuirecover ukitaka hata kesho kwa kuuza gari. Ni wewe tu.

Muhimu hata ukiiuza gari ujue hiyo pesa unaiweka wapi? Au utatumbua then utakuja na thread ingine tena kuwa una "chuma ulete?"
 

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
16,108
2,000
Matumizi rough ya pesa bila sababu ya msingi ndio chanzo kikuu cha kuishiwa.

Chuma ulete gani hiyo ambayo unaelewa kila cent ya pesa namna ilivyotumika?

Huwezi ukafanya machache halafuu ukawa na ndoto ya kuishi kama mengi.
 

gidume

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
662
1,000
Bora umenipa moyo. Sbr nipange mipango, atleast nipate sasa kagari cha mil 8 adi 9 mengine niweke kwenye account ambayo sio rahisi kuizoa..ikipepea ntakuja na mada ya chuma ulete
 

gidume

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
662
1,000
Matumizi rough ya pesa bila sababu ya msingi ndio chanzo kikuu cha kuishiwa

Chuma ulete gani hiyo ambayo unaelewa kila cent ya pesa namna ilivyotumika?

Huwezi ukafanya machache halafuu ukawa na ndoto ya kuishi kama mengi

Natumia rough kwa kualocate sehemu za msingi sbb naelewa nikikaa na pesa naweza tumia kwenye vitu ambavyo sitaki kutumia..
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,866
2,000
Pesa utumie mwenyewe, mchawi umtafute mwingine!??? Tanzania kweli kuna watu na viatu! Ushauri wa bure, angalia komenti ya Mr Slim hapo juu :)

NB: Ukweli, sidhani unahitaji ushauri, bali kupongezwa kwa kuitumia hela ili IKUZOEE halafu baadaye ulimwengu UKUZODOE!
 

Zabron Hamis

Verified Member
Dec 19, 2016
3,490
2,000
Kwa mtazamo wako utaona haina ulazima ila kwa status yangu mimi niliona inanifaa sbb nilikua nna excess ya mil 5 nzima..
Hakuna status bali ujinga tu. Haya hiyo status imekusaidia nini mpaka sasa.

Unapenda kuishi maisha ya watu wengine na sio maisha yako. Haya shauriwa na hiyo status yako sasa. Wakati mwingine mnawasingizia wachawi bure.
 

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
2,012
2,000
Uza tafuta gari ya kawaida ya m7.ilobaki kalime mvua zinakuja machi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom