Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi

Halafu cha ajabu unakuta ndugu wanachangia harusi ya siku moja 20m halafu baada ya miaka miwili ndoa inavunjika! Ila kumchangia ndugu mmoja hiyo 20m akasome elimu ya chuo kwa miaka mitatu ambayo itakuja kumsaidia maishani nahi!
Au hata mtaji wa biashara, au kuchangia matibabu. Akili za hovyo hovyo tu.
 
Au hata mtaji wa biashara, au kuchangia matibabu. Akili za hovyo hovyo tu.
Teh watakuambia huyo ndugu tukimchangia akasome au akafanye biashara baadaye akifanikiwa atatusahau! Unabaki unajiuliza kwamba wakichangia harusi ndiyo watafaidika ama!
 
Vipi kama anayeoa ni ndugu yako wa damu? Kama uwezo wa kuchangia huna sio lazima. Maisha ndio hayahaya. Jamii ndio itakuzika.
 
Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi kubwa, huku ukitaka sherehe yako ianzie labda milioni 20, wakati wewe kianzio ulichonacho labda milioni 1; hizo zingine unategemea upate kwa watu, kwa njia ya kuchangisha, huo sio uungwana.

Kwa nini ujibebeshe mzigo usioweza, na matokeo yake ni kuwapa wachangiaji majukumu ambayo si ya lazima. Starehe upate wewe, kwa nini usumbue wengine?

Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi.
Sawa
 
Harusi huitaji washenga,wafungishwa ndoa , mchungaji,wazazi pande mbili ma marafiki kadhaa kama nne.
Wakushangilia.

Ila kuna mtu alifunga ndoa kirahisi tu alikuja wakati wanakwaya wanapractise na akawaomba wawe mashaidi, mchungaji alikuwa kwenye kwa ya hiyo akaja akawauliza mmekubalina ndio wote wawili ndio basi wakafungishwa ndoa na kila kitu kilifanywa na wanakwaya vigelegele na ushuhuda. Basi ikawa ndio mwisho.

Ila mimi lazima aisee tarumbeta na msafara hata wamagari mawili tu matatu ila sendoff sifanyi huo muda sina .
 
Nimeanza kutunza hela kwaajili ya tukio langu sitasumbua mtu, mana asikwambie mtu hakuna kitu kigumu kama kuwakumbusha kumbusha watu michango, kama mimi kupiga piga simu ndo siwezagi kabisa.
 
Nimeanza kutunza hela kwaajili ya tukio langu sitasumbua mtu,mana asikwambie mtu hakuna kitu kigumu kama kuwakumbusha kumbusha watu michango,kama mimi kupiga piga simu ndo siwezagi kabisa.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Wengine hawaelewi; kuna wakulungwa wamenipa kadi hapa, nipo nazitazama tu huku napiga bia yangu taratiibu
 
Me mwenyewe nina kadi mbili..huyo mmoja ndo kanichosha elfu 50 single alafu double 80.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app
Mi huwa nachangia mambo ya msingi tu, haya ya sherehe nilishaachana nayo, ingawa wakati mwingine unawakwaza wengine; lakini mi kipaumbele huwa ni kuchangia kwenye afya ya mtu
 
Wasiwasi wangu sijui kama wamekuelewa ila the title itself is self explanatory. Watu waelewe ujumbe huu ni muhimu na ndio ukweli. Kule kwetu kuna msemo kuwa kuku huwa anadonoa punje anayoweza kumeza.
 
Unakuta mtu hadi pete ya ndoa ananunua kwa michango ya watu. Sasa unakuta watu wanatoa kwa manung'uniko weee....unadhani hiyo ndoa itatoboa hata mwaka?? Mimi siwezi kuchangisha senti ya mtu aisee. Bora nisifanye sherehe kabisa.
 
Back
Top Bottom