Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi

Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi kubwa, huku ukitaka sherehe yako ianzie labda milioni 20, wakati wewe kianzio ulichonacho labda milioni 1; hizo zingine unategemea upate kwa watu, kwa njia ya kuchangisha, huo sio uungwana.

Kwa nini ujibebeshe mzigo usioweza, na matokeo yake ni kuwapa wachangiaji majukumu ambayo si ya lazima. Starehe upate wewe, kwa nini usumbue wengine?

Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi.
sawa kabisa, tuende sawa na hali ya uchumi.,,,,naunga mkono hoja
 
Tuna changishana hela then after one month majitu yame achana sasa hivi sichangi, kuna jamaa yangu mmoja nlitoa laki 2 ndoa haikudumu hata mwaka
 
Kutokana na ugumu au vipaumbele vya maisha, watu wengi wanajitahidi kupunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima. Sasa wewe kipato chako hakitoshelezi kufanya sherehe ya harusi kubwa, huku ukitaka sherehe yako ianzie labda milioni 20, wakati wewe kianzio ulichonacho labda milioni 1; hizo zingine unategemea upate kwa watu, kwa njia ya kuchangisha, huo sio uungwana.

Kwa nini ujibebeshe mzigo usioweza, na matokeo yake ni kuwapa wachangiaji majukumu ambayo si ya lazima. Starehe upate wewe, kwa nini usumbue wengine?

Ukiniona nipo kwenye ndoa na sijawahi kukupa kadi ya harusi kwa ajili ya mchango; usiniletee kadi yako ya mchango wa harusi.
Mimi sichangii mtu harusi hata siku moja, naona ni ujinga tu.....kuoa anaoa mtu mwingine halafu mimi nimchangie? Kama mtu hauko tayari kuoa si lazima ujilazimishe kuoa.
 
Hizi Issue za michango ya harusi nilishaachana nazo miaka kumi iliyopita kiasi kwamba hata hapa kazini wananijua kuwa sichangiaji hivyo hata kadi hawajishughulishi kunipa
 
Mambo ya maradhi hawachangii, ila mambo ya kurukaruka ukumbini wanataka michango
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom