Mtoto una vijineno weye, kama kurumbizi!
Zinduna na Heart
mwanivutia maneno hadi na picha
nilitaka kukacha lkn sasa nimefika
Mtu chake mtu chake,usitake nikukate mtama
Mie sio wa chakechake,ni wa hapa hapa daresalaama
Kama unatafuta mke,sisi tuache kwa wako usalama
Tumkaribishe zinduna,kwa matarumbeta na vicheko
nawe karibu hukuKaribu tena
Hahahaaa... ndio maana sitaki kabisa kuonana/kujuana na members wa JF huko mtaani. Vijembe njenjeChokest kabisa mu poketi
Hahahaaa... ndio maana sitaki kabisa kuonana/kujuana na members wa JF huko mtaani. Vijembe njenje
Jamani Heart..wala usihofu
nimekuona wewe...ila kwa zinduna mm kipofu
natoka kivu..mpk bandari ya salama
Sio kwamba nalia,nina machozi ya furaha
Kama zinduna karidhia,basi mchukue kwa raha
Mimi hilo nimefurahia,sisikii kinyongo wala karaha
Tumkaribishe zinduna,kwa matarumbeta na vicheko
Karibu zinduna.Kimya changu, hakika kinamshindo,
Msijedhani nikimya, milele hata dahali,
Kuwa kwangu kimya, ni sawa na ada ya mja,
Ukimya wangu
Ada ya mja hunena, walisema wahenga,
Kwa muungwan ni vitendo, walimalizia malenga,
Kukaa kwangu kimya, hakika ni uungwana,
Ukimya wangu
Teh teh teh....
Kipi kikuchekeshechacho......?? (I hope i'm right)
Katangaze mshindi kwenye mkesha wa jana!
Jana Da'Moyo alifunika mbaya!
wala bado hajaridhia..ndio kwanza namlilia
dua yako iwe ya heri..kilio changu kusikia
zinduna uko wapi..au ndio umenunaa