Ukimya wa Katiba ya JMT Kuhusu Kifo cha Mgombea Urais

Mkuu Matuja uko vizuri, ila hapo kwenye para ya 4, vipi kama chama kina uhakika kuwa aliyeapa kuchukuwa nafasi ya marehemu aliyefariki kwenye kampeni hauziki kwa wapiga kura alafu wakaitisha vikao hivyo kumtokosa ugombea wa urais wakati ameishaonja tamu ya urais alafu akawaza kuwa si mimi ndiyo ninaamuru majeshi? Si mimi ndiyo nina mamlaka ya kuahirisha/kufuta uchaguzi? Kwanini nikubali kuachia urais na kurudi kugombea kama running mate alafu nije nirudi Ikulu ambayo tayari nimeishakuwa rais lakini nirudi humo kama Makamu wa Rais? What is chama after all? Si ni wawahi viongozi wa chama kwa kufuta uchaguzi wote alafu naunda chama changu nakisajili na ndipo niitishe uchaguzi mkuu baada ya muda hukooo?

Mkuu Matuja, tupe maarifa.
Mkuu Douglas, ngoja tubaki ni assumptions za sasa; hizo zingine waswahili wanasema ingakuwa ngumu "kumesa".
Wakubwa wa chama au wale wanaofahamu vema falsafa za utamaduni wao wanaweza kutupa dondoo nini kinaweza kufanyika
 
MIMI NINAVYOELEWA INAPOTOKEA RAIS ALIYEPO MADARAKANI AKIFA AKIWA KWENYE KAMPENI NI KWAMBA KWANZA TUELEWE KUWA RAIS KUWA KWENYE KAMPENI MAANA YAKE MUDA WAKE WA KUKAA MADARAKANI UMEISHA HIVYO IKITOKEA KIFO NI KWAMBA TUME YA UCHAGUZI ITASITISHA KAMPENI KWA WAGOMBEA URAIS TU (MAANA YAKE KAMPENI ZINGINE YA UBUNGE NA UDIWANI ZITAENDELEA) NA CHAMA HUSIKA ITAPEWA NAFASI YA KUTAFUTA MGOMBEA MWINGINE NA ASKISHAPATIKANA KAMPENI ZITAENDELEA KAMA KAWAIDA. kama kuna mwenye uelewa zaidi wa hayo mambo anaweza kutusaidia
Uelewa wako ni mzuri na inawezekana ndiyo utaratibu uliopo kwenye ground. Mfupa mgumu ni huu:-
Ikiwa Makamu Rais ambaye ni Mgombea mwenza atachukuwa kiti cha Rais, lakini akawa hauziki kwa wapiga kura (hawezi kuleta ushindi) kwa maana kwamba chama kinamtaka asigombee Urais, je, atakubali ugombea mwenza ili aje awe Makamu cheo cha zamani kabla hajarithi kiti cha Rais? Yaani alikuwa Makamu Rais, akapanda akawa Rais (kupitia kifo cha Rais) alafu arudi kuwa Mgombea mwenza ili aje arudie cheo cha zamani cha Umakamu, ni rahisi hii? Na kama siyo rahisi Katiba inatoa ufumbuzi upi? Kama Katiba iko kimya je, hawezi kutumia ukimya huo kufuta uchaguzi, kupiga marufuku shughuli za kisiasa kwa kiwango kikubwa? Akaunda chama chake alafu akiishaweka mizizi anaitisha uchaguzi?
 
Kanda yote ya ziwa ina wapiga kura kama 25% tu. Hiyo asilimia inamwongezea tu kura mgombea lakini haina uwezo wa kuamua mshindi.

Sijui kwa nini wakati wa Magufuli watu walidanganywa na kuaminishwa kuwa kanda ya Ziwa pekee inaweza kuamua juu ya kura za Rais. Ujinga ni mzigo.
Tatizo limeanzia hapo uliposema kama.
kama hunauhakika usipinge jiridhdishe kwanza afu uje na data halisi.
 
Mada Fikirishi

Katiba yetu inaongelea kifo cha Rais akiwa madarakani lakini haiongelei Mgombea Urais ambaye tayari ni Rais akifa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu. Natoa mfano ili uelewe kwa urahisi kwamba JPM angekufa akiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu Katiba haisemi kitu gani kifanyike zaidi tu ya kusema nafasi ya Rais itachukuliwa na Makamu wa Rais. Sasa yafuatayo hayana majibu ya Katiba:-

1. Je, kama Mgeombea Urais akifa kwenye kampeni za uchaguzi nafasi yake itajazwaje?

2. Je, Makamu wa Rais anayerithi kiti cha Rais ndiye atakuwa Mgombea nafasi ya Urais?

3. Je, atateuliwa mwingine na chama kujaza nafasi ya Mgombea Urais? Au atajaza nafasi ya Makamu wa Rais kwa kuwa Makamu wa Rais aliyekuwepo tayari amerithi kiti cha Rais na kuwa Rais?

4. Kama Makamu anayerithi kiti cha Rais siyo strong kushinda uchaguzi yaani siyo kipenzi cha wapiga kura wengi na kwamba akipewa kurithi pia nafasi ya Mgombea Urais aliyekufa kwenye kampeni huenda chama kikapoteza ushindi je, hapa chama au serikali iliyoko madarakani itamshusha Rais huyu (ambaye alikuwa Makamu zamani) toka kwenye kiti cha Rais ili arudi aendelee kugombea nafasi yake ile ile ya awali ya Makamu wa Rais aliyokuwa akigombea kabla Mgombea Urais (ambaye alikuwa Rais) kufa wakati wa kampeni za uchaguzi?

5. Je, hiyo siyo demotion/kushushwa cheo kwa Rais?

6. Je, Katiba inatoa maelekezo yoyote kuhusu demotion ya Rais toka kuwa Rais na kurudi kuwa Makamu wa Rais?

7. Japokuwa iko wenye Katiba kuhusu kifo cha Rais akiwa madarakani lakini kama taifa hatukujiandaa na kifo cha Rais akiwa madarakani, ni vivyo hivyo kumbe kwamba hata sasa kama taifa hatujajiandaa na kifo cha Rais ambaye ni Mgombea nafasi ya Urais; kwenye kampeni za uchaguzi mkuu. Kipi kifanyike? Au tuige Katiba ya Urusi ambayo Rais anaweza kuondoka Ikulu na akawa Waziri Mkuu na kurudi kuwa tena Rais Ikulu?
Inawezekana ukawa umezaliwa miaka ya hivi karibuni. Uchaguzi wa 2005 uliahirishwa siku moja kabla ya siku ya uchaguzi baada ya mgombea mwenza wa CHADEMA kufariki. hivyo katiba yetu iko wazi kwenye hilo
 
Vipi? kuna mwingine tena anafuatia maana hoja hii leo imejadiliwa saana.
 
Mkuu, nadhani wenye mawazo kama hayo wanapoteza muda tu, utakumbuka siku moja nilipost hapa kuwa kura na katiba mpya hazimpeleki Rais Ikulu, rais anapelekwa Ikulu na dola. Kura na katiba mpya zinapeleka tu Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa SM. Yaani ni ngumu sana ukatoka Ubelgiji ukaja kugombea Urais alafu utegemee masanduku ya kura na katiba mpya vikuingize Ikulu. EL alikuwa tishio lakini bado masanduku ya kura hayakumpa Ikulu, ni vivyo hivyo kwa wengine waliojaribu kinyang'anyiro. Siko kwenye ushabiki wa kiitikiadi na mrengo na wala sina nia mbaya na mtu awaye yote ila tu naongelea Empiricism (uhalisia).

Empirical Facts:-
Kanda ya Ziwa ina Majimbo 42 tu dhidi ya Majimbo 222 ya Kanda zingine za nchi. Hivyo hata Kanda ya Ziwa ikifanya fitina bado koramu ya Majimbo 222 ipo kwenye Kanda zingine.

Tz ina Majimbo 264 (Bara 214 na Znz 50).

NB.
Siasa za fitina za Kikanda ziko nchi jirani, hapa Tz hazina washabiki kwasababu Watz hawako tayari kujinasib kwa Ukanda maana wanajuwa madhara yake.
Ilo ulilotaja hapo juu linawezeshwa na ubovu wa katiba iliyopo sasa.Hizo unazoziita dola na jamii yake vinakua hivyo vilivyo kwasababu kuna katiba inampa mtu mmoja mamlaka yakuteua hao wote.Kwahiyo kamwe usidharau katiba kama hujui imempa nguvu rais aliyepo madarakani nguvu kiasi gani.
 
Ilo ulilotaja hapo juu linawezeshwa na ubovu wa katiba iliyopo sasa.Hizo unazoziita dola na jamii yake vinakua hivyo vilivyo kwasababu kuna katiba inampa mtu mmoja mamlaka yakuteua hao wote.Kwahiyo kamwe usidharau katiba kama hujui imempa nguvu rais aliyepo madarakani nguvu kiasi gani.
Mkuu mbona hiyo inaeleweka wazi tu kwa kila mtu, ndiyo maana nikasisitiza kwamba kwa nguvu alizonazo "who can dare him/her" hata kama wewe ni Kanda ya Ziwa? Mfano, Uhuru Kenyatta alisuswa Jimbo lote la Nyanza kwenye rerun ya Oktoba 26, 2017 ambayo hasimu wake Raila aliwahamasisha watu wa Nyanza kususia rerun kwa sababu IEBC haijatekeleza makubaliano ya mabadiliko lakini pamoja na Nyanza kususa haikumzuia Uhuru kuwa rais. Pamoja na Raila kujiapisha bado haikumzuia Uhuru kuwa rais na leo Raila amekubali nguvu ya taasisi hiyo akajirudi kuungana naye Uhuru. Kwanini? kwa sababu taasisi hiyo ya rais inampa nguvu kubwa ya turufu juu ya watu na taasisi zote. Hivyo dhana kwamba Kanda ya Ziwa inaweza kuikwamisha nchi ni dhana ambayo siyo Empirical.
 
MIMI NINAVYOELEWA INAPOTOKEA RAIS ALIYEPO MADARAKANI AKIFA AKIWA KWENYE KAMPENI NI KWAMBA KWANZA TUELEWE KUWA RAIS KUWA KWENYE KAMPENI MAANA YAKE MUDA WAKE WA KUKAA MADARAKANI UMEISHA HIVYO IKITOKEA KIFO NI KWAMBA TUME YA UCHAGUZI ITASITISHA KAMPENI KWA WAGOMBEA URAIS TU (MAANA YAKE KAMPENI ZINGINE YA UBUNGE NA UDIWANI ZITAENDELEA) NA CHAMA HUSIKA ITAPEWA NAFASI YA KUTAFUTA MGOMBEA MWINGINE NA ASKISHAPATIKANA KAMPENI ZITAENDELEA KAMA KAWAIDA. kama kuna mwenye uelewa zaidi wa hayo mambo anaweza kutusaidia
Mkuu, muda wa Rais hauishi kwa kuwa Rais yupo kwenye kampeni. Ndio maana hata wakati wa kampeni sio Tanzania tu, duniani kote, seating president anaendelea kuwa na huduma zote na mamlaka yote kama Rais, mpaka pale Rais mpya anapochaguliwa na kuapishwa.

Kikatiba Rais huwa anakoma kuwa Rais baada ya Rais mwingine kuapishwa au kama ambayo kifo kitaweza kutokea akiwa kwenye kampeni. Ni vema tuwe na uwelewa wa pamoja kwenye hili.
 
Back
Top Bottom