Samahanini wanajamvi kwa kuwarudisha nyuma.
Hii hasa ni kwa wale wana CCM ambao ndio wenye uwezo wa kumshawishi au kumlazimisha mbunge wao Lusinde ajiuzulu wazifa wake.
Nimekua nikifuatilia huku kwenye mtandao wa great thinkers na magazeti kuona kama kuna kiongozi yeyote wa juu CCM ambaye ameonyeshwa kuchukizwa na matusi yaliyokua yakiporomoshwa na Lusinde lakini sijafanikiwa kupata hata kauli moja. Sasa sielewi kama viongozi hawa wameridhika na matusi hayo au ni vipi!
Kwangu mimi hili sio jambo dogo na lina impact kubwa sana kwa maendeleo ya CCM kwani clip au video zilizorekodiwa kuonyesha Lusinde akitukana zitaishi milele na zitatumika kuonye ubaya wa CCM na ukosefu wa maadili kwenye chama hiki.
Natoa wito kwa wanachama wa CCM kupiga kura kumshinikiza Lusinde ajiuzulu wadhifa wake kama mbunge. Wana CCM humu JF wanaweza kuwa mfano wa kuchukizwa na swala hili na pia kuwashawishi wabunge wa CCM wamshinikize mbunge mwenzao ajiengue kwa ajili ya maslahi ya chama.
Vinginevyo, CCM wajiandae kwa hali ngumu zaidi kwani msione kukaa kimya kwa CHADEMA inamaanisha wameridhiswa na matusi yale yaliyoporomoshwa na huyu bwana.
Haiingiia akilini kuona wazee wenye busara waliopo CCM wote wamekaa kimya na hakuna aliyesimama kiume na kusema kwamba Lusinde alikosea kutoa matusi yale.
Nape, embu jaribu kujitoa muhanga kumweleza ukweli kijana mwenzio na wenzako watafuata.