Ukimya wa CCM na Lusinde

Kibajaji - duu kweli tz tunasafari ndefu, hivi huyo aliyemtaburisha kibajaji ni nani?
 
Sahau. Kwenye matuzi yake alianza hivi: "CCM Oyeeee." Wasikilizaji wakaitikia "Oyeeeeeeeeeeeee." Kabla ya kumwaga matuzi akasema "Mheshimiwa Mwenyekiti wa chama, Waheshimiwa viongozi wenzangu na Wanachama wenzangu." Kama alikuja kivyake pale pale (hakutumwa) kwa nini ali-wamention hawa? Na kama walimtuma wanaweza kweli kumchukulia hatua?
 
Hivi CCM wameshatoa tamko lolote kuhusiana na mbunge wao Livingston Lusinde kuporomosha mitusi kule Arumeru?

Nyepesi nyepesi zinasema ati alikuwa na baraka zote za chama chake. Ingawa tunasubiri kauli ya Polisi na NEC kuhusu uvunjifu wa sheria (kutukana hadharani) na kanuni za uchaguzi (kutumia lugha zisizokubalika katika jamii ya kistaarabu. I wonder ingekuwaje endapo mbunge wa CHADEMA angetumia maneno hayo hayo dhidi ya viongozi wa CCM!?
 
Last edited by a moderator:
Sahau. Kwenye matuzi yake alianza hivi: "CCM Oyeeee." Wasikilizaji wakaitikia "Oyeeeeeeeeeeeee." Kabla ya kumwaga matuzi akasema "Mheshimiwa Mwenyekiti wa chama, Waheshimiwa viongozi wenzangu na Wanachama wenzangu." Kama alikuja kivyake pale pale (hakutumwa) kwa nini ali-wamention hawa? Na kama walimtuma wanaweza kweli kumchukulia hatua?

Mimi nimeanza kuhisi kuwa alikuwa na baraka zote za chama na ndiye alikuwa 'designated bomb thrower'....
 
Lakini Bob, huoni kwamba huyu jamaa ndo anaweza kuizamisha meli ya CCM 2015? Au wewe bado unataka CCM iendelee tu kutawala?

Nyani Ngabu, matusi ya huyu jamaa yalivuka mipaka. Ni lazima ashikishwe adabu .... ngoja tusubiri kama chama chake kitatoa kauli yoyote.
 
jamani mwacheni lusinde huo ndo mtaji mkuu wa CDM tatumia matusi yake kuwashtaki ccm kwa wananchi.
 
Mimi nimeanza kuhisi kuwa alikuwa na baraka zote za chama na ndiye alikuwa 'designated bomb thrower'....

Labda turudi nyuma kidogo. Heri huyu aliyetukana. Vipi yule aliyekuwa kwenye mkutano Igunga na bastola amechukuliwa hatua gani hadi sasa?

​
rage.jpg
 
Hawawezi kutoa tamko lolote kwa sababu matusi ndiyo sera yao; hivi wewe hujawahi kumsikia Mkapa akiporomosha matusi? Tofauti ni kuwa Lusinde anajua matusi mengi kuliko Mkapa, yaani anajua kutangaza sera za CCM vizuri kuliko Mkapa. Je unakumbuka mzee Makamba naye alivyokuwa akitoa matusi makavu makavu? je unamkumbuka Ditopile alivyokuwa nay akitoa matusi ya wazi wazi? Je CCM iliwafanya nini? Utamshangaa Lusinde hapo tu, lakini yeye ataendelea kudunda ndani ya CCM kwa vile ndiye mtendaji mzuri.
 
Ccm wanazaa pacha watatu kila wakati, this time pacha watatu wa matusi Lusinde, Mkapa na Wasira.
 
Hawawezi kutoa tamko lolote kwa sababu matusi ndiyo sera yao; hivi wewe hujawahi kumsikia Mkapa akiporomosha matusi? Tofauti ni kuwa Lusinde anajua matusi mengi kuliko Mkapa, yaani anajua kutangaza sera za CCM vizuri kuliko Mkapa. Je unakumbuka mzee Makamba naye alivyokuwa akitoa matusi makavu makavu? je unamkumbuka Ditopile alivyokuwa nay akitoa matusi ya wazi wazi? Je CCM iliwafanya nini? Utamshangaa Lusinde hapo tu, lakini yeye ataendelea kudunda ndani ya CCM kwa vile ndiye mtendaji mzuri.

Hata huyu huyu Nape alishawahi kutaka wafuasi wa Chadema wapigwe huko Mwanza, huku akiwaita "Manyani wa CHADEMA" lakini hakuchuliwa hatua zozote: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/183485-nape-kushtakiwa-kwa-jk-kwa-matusi-mwanza-2.html
 
Lakini ni kweli wa upande wa pili walimwita jamaa ni shoga? maana kama ni kweli wote hawana tofauti na kama si kweli huyu bajaji ilitakiwa hata uunge avuliwe.
 
Wapenzi wengine visimu vyetu havina uwezo kufungua yotube tusikie. Mwenye uwezo aandike hayo matusi wote tujue. Ili tusaidiane kumhukumu.
 
At Least Kibajaj amenikumbusha kampeni za akina Madevu na Komandoo miaka ya tisini

Komandoo Salmin Amour au Komandoo Hamza Kalala? Kama Ni Salmin naona ashakuwa mgambo...hana lake tena kwisha habari yake. Ndo faida ya siasa za kibabe.
 
Wapenzi wengine visimu vyetu havina uwezo kufungua yotube tusikie. Mwenye uwezo aandike hayo matusi wote tujue. Ili tusaidiane kumhukumu.

mkuu matusi hayaandikiki. Jaribu ku-connect dots. Au tumia computer
 
Ndugu yangu ni CCM ipi unayoizungumzia? Hii ya sasa? Labda Mwl .Nyerere afufuke ndipo watu wafunguke macho na kuanza kuona ubaya wanayoyafanya na kuyazungumza. Short of that, forget about it!!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom