Ukimya wa CCM na Lusinde

Hawawezi toa tamko they thought Arumeru was 'Campo Vaccino':nono:
 
Hivi sirikali imeishatoa tamko lolote kuhusiana na polisi na UVCCM kuhusika na kupiga na kushambuliwa kwa wabunge wa Chadema mwanza?
 
Suala la Lusinde limerudishwa kwenye kamati ya maadili ya chama!
 
Yule lusinde alikuwa anawapa burudani wasikilizaji wake ambao hawajalamika. Achana na kibabaji bana tena anasema akili chafu kwake yeye ni za kuzaliwa
 
mi naona asamehewe tuu kwani si unajua mfa maji, alikuwa hana la kusema yy sera zake zilikuwa hizo.kama bado ananguvu ajitahidi kuweka mambo sawa 2015 la sivyo itabidi apokwe jimbo lake kwa kubebwa na CDM
 
Samahanini wanajamvi kwa kuwarudisha nyuma.

Hii hasa ni kwa wale wana CCM ambao ndio wenye uwezo wa kumshawishi au kumlazimisha mbunge wao Lusinde ajiuzulu wazifa wake.

Nimekua nikifuatilia huku kwenye mtandao wa great thinkers na magazeti kuona kama kuna kiongozi yeyote wa juu CCM ambaye ameonyeshwa kuchukizwa na matusi yaliyokua yakiporomoshwa na Lusinde lakini sijafanikiwa kupata hata kauli moja. Sasa sielewi kama viongozi hawa wameridhika na matusi hayo au ni vipi!
Kwangu mimi hili sio jambo dogo na lina impact kubwa sana kwa maendeleo ya CCM kwani clip au video zilizorekodiwa kuonyesha Lusinde akitukana zitaishi milele na zitatumika kuonye ubaya wa CCM na ukosefu wa maadili kwenye chama hiki.
Natoa wito kwa wanachama wa CCM kupiga kura kumshinikiza Lusinde ajiuzulu wadhifa wake kama mbunge. Wana CCM humu JF wanaweza kuwa mfano wa kuchukizwa na swala hili na pia kuwashawishi wabunge wa CCM wamshinikize mbunge mwenzao ajiengue kwa ajili ya maslahi ya chama.
Vinginevyo, CCM wajiandae kwa hali ngumu zaidi kwani msione kukaa kimya kwa CHADEMA inamaanisha wameridhiswa na matusi yale yaliyoporomoshwa na huyu bwana.
Haiingiia akilini kuona wazee wenye busara waliopo CCM wote wamekaa kimya na hakuna aliyesimama kiume na kusema kwamba Lusinde alikosea kutoa matusi yale.

Nape, embu jaribu kujitoa muhanga kumweleza ukweli kijana mwenzio na wenzako watafuata.
 
Hivi CCM wameshatoa tamko lolote kuhusiana na mbunge wao Livingston Lusinde kuporomosha mitusi kule Arumeru?

Sina hakika kama watasema lolote ... kumbukumbu yangu inaonyesha kwamba CC ilikutana kabla ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki na nina hakika kwamba apart from kujadili majina ya wagombea wa Ubunge wa EAC kupitia CCM, lazima CC ilipokea taarifa ya tathimini ya Kampeni za huko Arumeru. Wakati CC inakutana tayari Lusinde alishaporomosha matusi na tayari yalishazua mjadala kwenye mitandao ya kijamii.

Tatizo la CCM huwa wanafikiri kwamba wanachukiwa na mitandao ya kijamii na kwamba wapiga kura wana feelings tofauti na zile tulizo nazo hapa. Kwa hiyo inawezekana wali-ignore na hasa ukizingatia kwamba Lusinde alipokuwa akiporomosha matusi alikuwa akishangiliwa sana na kumbe wapo kibao ambao walikuwa wanakwazika lakini hawaonyeshi kukerwa kwao.

Kwa kiasi kikubwa Lusinde, Mkapa na Wasira wamewasaidia sana CHADEMA kushinda, hasa LUSINDE. Next time CCM itapeleka watu wenye akili kwenye kampeni na sio watukanaji kama Lusinde au waropokaji kama Mkapa na Wasira.
 
Na Mkapa pia aliongea pumba, na Yule Babu Wassira naye aliongea pumba,,, nani amfunge paka Kengele?
 
NN

Inasikitisha kuona hadi sasa, hakuna kiongozi yeyote wa CCM aliyekana matusi ya Lusinde

it is really disappointing
 
NN

Inasikitisha kuona hadi sasa, hakuna kiongozi yeyote wa CCM aliyekana matusi ya Lusinde

it is really disappointing

But you know what, I think it's a good thing. Mimi binafsi sitaki kabisa aadhibiwe.
 
Back
Top Bottom