UKIMWI upo, tambueni thamani yenu

UKIMWI upo, tambueni thamani yenu

soma vizuri mkuu utaelewa baada ya miezi 7 ya kujifungua ndio mimi napewa taarifa hii wakati ambao mama anapaswa amuachishe mtoto kunyonya hivyo kwa hali yoyote angefanya kimya kimya lazima ningehoji kwanini iwe hivi.
Hakuna anaejisifia matatizo humu.
mkuu inaonekana alikuwa anajua na mjibu alishapewa kitambo,ila akahisi we lazima utahoji why mtt anyonyeshwi??
 
Nishasema ivi, raha ya dk 1 (when ejaculating) haiwezi nipotezea dira na mipango ya maisha ya miaka 70
utakuwa na kibamia, au sekunde 30 chali, kuamka mpaka jumatatu ijayo, hakuna aliekuwa mjanja kwa "k" hakuna cha osama, sadam, msomi ,una cheo, ww n daktar, hakuna mjanja kwa "k" ni tamuu ilee haikwepekiiii , mengne manusura ya m, mungu tuuu over!!
 
Mkuu nimepitia maelezo yako lakini ni kama mchumba wako huwenda anahili tatizo kitambo na hakutaka kukwambia maana mwanamke akishapata ujauzito mwanzoni kabisa kliniki anachekiwa ili kujua status yake kama anatatizo wanaanza utaratibu wa elimu na kumsaidia asipeleke maambukizi kwa mtoto,sasa kwanini akae kipindi chote hadi ajifungue na anyonyeshe kwa miezi 7 ndio aache kunyonyesha na kukwambia?


Kuhusu wewe kutopata maambukizi huwenda huyo binti alijijua kitambo hari yake na akawa katika mpangilio mzuri wa dawa,wanadai mtu akiwa katika mpangilio mzuri wa dawa kwa kipindi cha muda fulani mwanaume akija kumwingia peku hawezi pata tatizo,hebu fanya kuchunguza.
mkuu hospt wanawaambia wanyonyeshe kwa kipindi cha miezi sita kamili bila kumchanyia na kitu kingine chochote , baada ya hapo anaacha kunyonya mona kwa moja anaanza kutumia maziwa ya kopo
 
Mpenzi wangu wa sasa ndio wa kwanza ananisisitiza niende nae kupima. Ananipenda sana ila nafsi yangu inasita kweli kwenda pima.
Wiki hii napiga moyo konde naenda ila siendi nae, nitaenda kivyangu kwanza kisha majibu yakiwa mazuri nitamchukua nikapime nae sehemu nyingine.
Majibu yakiwa mazuri NAAPA nitaanza kwenda kanisani na nitamuoa huyu binti anayeonekana kunijali na nitatulia nae na pia nitaanza maisha mapya kwa kuachana na marafiki zangu wa sasa ambao kwa kweli sio wa kuwa nao. Nitabadili namba za simu na kuhama kabisa hata mkoa na kwenda anza "upya". Kuhama sio ishu, bado nitakapohamia nina mizizi hivyo haitakuwa ngumu. Kikubwa hili genge langu haliwezi fika huko. NIMEDHAMIRIA, MUNGU niongoze.
Duuh noma Sana aisee... Amua kweli mkuu
 
Asante sana Kwa kunipatia mwanga, kwasababu hata wakati ananipa taarifa hii alikuwa yupo simpo kama tunatania tu. hivyo hali yake aliifahamu kitambo na kosa langu ni mimi kutokwenda nae pamoja clinic wakati wa awali.
kosa kubwa sana tulifanyalo wanaume hilo.
 
Ila kuna watu wana maambukiz lakini wakipimwa hawana.
Hyo ipo kabisa,kuna jamaa kasha ua kibao lakini yeye kila akichek hana. Na akitambea na demu anaambukiza.
Hapo sijuagi ni kitu gani kwa kweli
mhh hamna kitu kama icho
 
Nilikuwa na tabia ya kuwabadilisha wanawake Mbalimbali kwaajili ya ngono, siku za weekend nikiwa free hadi watatu kwa siku, kama makahaba wanaojiuza wa kujipanga kujiuza nimetembea nao hawana idadi na barmaids kibao hawana idadi pia ( Kundi hili ni hatari zaidi) na wote hao sikutumia kinga nilifanya ngono zembe.

Ujanja wangu nikapatikana kwa binti wa miaka 18 tu akiwa mbichiiiii anawaka kama jua la saa sita, Nimekuwa nae hatimae akapata ujauzito na mpango wangu ulikua kumuoa kwasababu nilikolea haswaa, baada ya kujifungua ikapita miezi 7 akaniambia clinic ameambiwa amuachishe mtoto kunyonya kwasababu yeye ana Ukimwi. (Sijui ushujaa huu wa kuniambia alioutoa wapi)

Nikashangaa sana kwasababu nilikuwa nimetoka kupima sio muda nikiwa peke yangu... Hivyo nikaamua kumtaarifu mama yake juu ya taarifa hii kumbe wao wote huko kwao walikua wanafahamu habari hii ila mimi walikua wananificha na waliamini mimi ndio nimeleta ugonjwa kwa mtoto wao,

Baada ya mimi kulia na kupagawa sana nikaamua Kwenda kupima tukiwa wote mimi, mchumba wangu na mtoto pamoja na shahidi wa upande wa binti ambae ni mama yake mkubwa, vipimo vikawa mimi na mtoto ni wazima ila mchumba ni kweli hiv+.

Tokea hapo ndio niliitambua thamani yangu hapa duniani. hakika nimekoma tabia ya kuruka hovyo na wanawake bila tahadhari.

Enyi Madume menzangu mliopo kwenye ndoa kuweni na utaratibu wa kupima na wake zenu kwasababu lolote linaweza kutokea mtu ukajiokoa na maradhi haya.
Majibu ya mtu mmoja hayatoshi kuthibitisha afya yenu hasa tunavyowatumia wanawake kama vipimo vyetu wanapoenda clinic.

Tuwe makini bado tuna safari ndefu ya kuwafikisha watoto wetu katika ndoto zao.
Ni kweli hii inawezekana kabisa sisi watu wa afya kesi kama hizo tumekutana nazo sana ,,kuna mmoja alipona kwasababu alikuwa mlevi sana kwahiyo akawa ampandi Mkewe ndio pona pona yake
 
Duh! Kuna mambo mazito sana kwenye mahusiano
 
Back
Top Bottom