UKIMWI upo, tambueni thamani yenu

UKIMWI upo, tambueni thamani yenu

Mkuu nimepitia maelezo yako lakini ni kama mchumba wako huwenda anahili tatizo kitambo na hakutaka kukwambia maana mwanamke akishapata ujauzito mwanzoni kabisa kliniki anachekiwa ili kujua status yake kama anatatizo wanaanza utaratibu wa elimu na kumsaidia asipeleke maambukizi kwa mtoto,sasa kwanini akae kipindi chote hadi ajifungue na anyonyeshe kwa miezi 7 ndio aache kunyonyesha na kukwambia?


Kuhusu wewe kutopata maambukizi huwenda huyo binti alijijua kitambo hari yake na akawa katika mpangilio mzuri wa dawa,wanadai mtu akiwa katika mpangilio mzuri wa dawa kwa kipindi cha muda fulani mwanaume akija kumwingia peku hawezi pata tatizo,hebu fanya kuchunguza.
 
Nilikuwa na tabia ya kuwabadilisha wanawake Mbalimbali kwaajili ya ngono, siku za weekend nikiwa free hadi watatu kwa siku, kama makahaba wanaojiuza wa kujipanga kujiuza nimetembea nao hawana idadi na barmaids kibao hawana idadi pia ( Kundi hili ni hatari zaidi) na wote hao sikutumia kinga nilifanya ngono zembe.

Ujanja wangu nikapatikana kwa binti wa miaka 18 tu akiwa mbichiiiii anawaka kama jua la saa sita, Nimekuwa nae hatimae akapata ujauzito na mpango wangu ulikua kumuoa kwasababu nilikolea haswaa, baada ya kujifungua ikapita miezi 7 akaniambia clinic ameambiwa amuachishe mtoto kunyonya kwasababu yeye ana Ukimwi. (Sijui ushujaa huu wa kuniambia alioutoa wapi)

Nikashangaa sana kwasababu nilikuwa nimetoka kupima sio muda nikiwa peke yangu... Hivyo nikaamua kumtaarifu mama yake juu ya taarifa hii kumbe wao wote huko kwao walikua wanafahamu habari hii ila mimi walikua wananificha na waliamini mimi ndio nimeleta ugonjwa kwa mtoto wao,

Baada ya mimi kulia na kupagawa sana nikaamua Kwenda kupima tukiwa wote mimi, mchumba wangu na mtoto pamoja na shahidi wa upande wa binti ambae ni mama yake mkubwa, vipimo vikawa mimi na mtoto ni wazima ila mchumba ni kweli hiv+.

Tokea hapo ndio niliitambua thamani yangu hapa duniani. hakika nimekoma tabia ya kuruka hovyo na wanawake bila tahadhari.

Enyi Madume menzangu mliopo kwenye ndoa kuweni na utaratibu wa kupima na wake zenu kwasababu lolote linaweza kutokea mtu ukajiokoa na maradhi haya.
Majibu ya mtu mmoja hayatoshi kuthibitisha afya yenu hasa tunavyowatumia wanawake kama vipimo vyetu wanapoenda clinic.

Tuwe makini bado tuna safari ndefu ya kuwafikisha watoto wetu katika ndoto zao.
Leo mara ya 4 napima naambiwa sina itakuwa sina kweli
IMG_20181014_131459.jpg
 
Unahakika hao wote uliokula hawakua na ugonjwa?

Wewe umenusulikaje?

Hoja za Decemption hizi
Kwa idadi ya niliowakula ni kubwa na makundi hatarishi hivyo naamini hawakosekani walio na Hiv+. Hebu fikilia mtu katwangwa risasi 30 nk na yupo hai na yule wa risasi moja amezikwa na tumemsahau. Hizi ni neema za Mungu pekee
 
Unaogopa ukimwi,,njoo hapa ocean road uone watu walivyotafunwa na saratani za koo na kadhalika,, ni hatari kabisa mkuu,, kuna maradhi kumbe afadhali ya huo ukimwi
Hakika mkuu hilo halipingiki, japo kuwepo kwa saratani kusitufanye tusahau kuna magonjwa ya kuambukizwa kama VVU na INI. unapokua hai ukipata nafasi ya kusemea chochote kwa manufaa ya jamii bora useme.
 
Mkeo kakutwa na hivyo vitu kwa sababu ya hofu ya muda mrefu kinga yake ilishaathirika ila asingeambiwa hivyo mpaka sasa angekuwa poa na mgeenda wote mkawa poa,kuna siasa nyingi sana juu ya hili suala
Mkuu ukweli sijajua kwanini sijapata naamini ni mipango ya Mungu pekee alikuwa na malengo yake, kwasababu kuna wakati nilikuwa napata hadi michubuko na nilikuwa rafu sana kwenye hilo.
labda kibaiolojia kuna sababu za msingj zaidi
 
Asante sana Kwa kunipatia mwanga, kwasababu hata wakati ananipa taarifa hii alikuwa yupo simpo kama tunatania tu. hivyo hali yake aliifahamu kitambo na kosa langu ni mimi kutokwenda nae pamoja clinic wakati wa awali.
Mkuu nimepitia maelezo yako lakini ni kama mchumba wako huwenda anahili tatizo kitambo na hakutaka kukwambia maana mwanamke akishapata ujauzito mwanzoni kabisa kliniki anachekiwa ili kujua status yake kama anatatizo wanaanza utaratibu wa elimu na kumsaidia asipeleke maambukizi kwa mtoto,sasa kwanini akae kipindi chote hadi ajifungue na anyonyeshe kwa miezi 7 ndio aache kunyonyesha na kukwambia?


Kuhusu wewe kutopata maambukizi huwenda huyo binti alijijua kitambo hari yake na akawa katika mpangilio mzuri wa dawa,wanadai mtu akiwa katika mpangilio mzuri wa dawa kwa kipindi cha muda fulani mwanaume akija kumwingia peku hawezi pata tatizo,hebu fanya kuchunguza.
 
Back
Top Bottom