Triple G
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 2,557
- 3,301
Daah aiseeh inatisha!! Mwenyezi Mungu atusaidie kwa kweliHakuna MTU aliyenifundisha madhara ya ukimwi kama mama yangu.Huwa haniambii maneno aliyosikia Bali mambo aliyoshuhudia
Walizaliwa 13 ila kati yao 9 wamekufa Kwa ukimwi.Kati ya wanne waliobaki tayari Wawili waathirika hivyo wanaishi Kwa matumaini
Huwa ananiambia ukoo wao unaisha Kwa ukimwi .Watoto wa Dada na kaka zake wanaishi Kwa matumaini.
Moja ya vitu ambavyo anauelewa mkubwa navyo basi namba moja ni ukimwi
Kauguza wote 9 waliofariki na anauguza Wawili sasa.
Nikiwa kitandani na mwanamke huwa nakumbuka maneno ya mama.
Niliwah pata demu mbichi ndio kamaliza form 4 kapo vizuri nikaenda nae kumgonga kavu kavu yani kwa american slang tunasema by the skin of my teeth .Tulipovua nguo nikakumbuka maneno ya mama.Nikamwambiaa vaa nguo tukapime ,akakubali.Tukazama Ukonga hospital ya masista tukakuta yeye muathirika ,ila hakuwahi kujua kuwa muathirika.
Now kila analonifundisha mama yangu nalifanyia kazi.
Asante mama.