Ukimuacha Nyerere, makosa ya Marais wetu ni ya makusudi kwa manufaa ya familia zao

Yaani ndo nchi zetu za Afrika tulivyo..
..., mambo yaleyale na afadhali hata nchi kama SA wanajaribu kwa katiba yao na kuheshimu sheria zao, na jana tu tumeona yaliyofanyika kwa Jacob Zuma.... bado naona tuna safari ni ndefu...kazi iendelee.
Tanzania Marais hawawajibiki wakiwa madarakani kwakua wakimaliza muda wao haijalishi walichokifanya Bado wanabakia na heshima zao ,

Hakuna wa kuwawajibisha.
 
Jambo ambalo watu wengi hawajui ni kwamba, matatizo karibu yote ya nchi hii msingi wake uliwekwa na Nyerere. Huo ndiyo ukweli mchungu.
 
Laiti ungejua kampuni iliyojenga Chato airport, Uboreshaji wa Dodoma na aliyepewa tenda ya kusupply malori kule Nyerere HEP huyo Meko usingemtoa kwenye list kabisa aisee.

Fanya research zaidi. Ulizia yule dogo bonge aliyekuwa kwenye Landcruiser nyeusi mbele ya msafara wa mazishi ana cheo gani kwenye kampuni ya dingi yake? Anasimamia tenda ngapi? Walizipataje?

Ukipata majibu njoo uedit Uzi wako.
Nyerere alivyokuwa ana ongoza south south commission, alisema tatizo la south yaani "Africa" mtoto wa kiongozi

1. Anapewa mradi kwa upendeleo
2. Atalipwa pesa na kazi hatofanya hivyo huo mradi yatakuwa na tija kwa uchumi wa Nchi, lakini Asia kosa litakuwa moja tu namba moja kwamba kazi itatolewa kwa upendeleo, lakini kazi itafanyika hivyo kuwa na tija kiuchumi.

Nafikiri utakuwa umeelewa
 
Tanzania Marais hawawajibiki wakiwa madarakani kwakua wakimaliza muda wao haijalishi walichokifanya Bado wanabakia na heshima zao ,

Hakuna wa kuwawajibisha.
Hapo ndo pa kubadilisha. Haiwezekani binadamu huyuhuyu aliyezaliwa kutoka kwa Adam na Eva asiwe anategemewa kufanya makosa akiwa na nguvu kubwa kiasi hicho
 
Nyerere alivyokuwa ana ongoza south south commission, alisema tatizo la south yaani "Africa" mtoto wa kiongozi

1. Anapewa mradi kwa upendeleo
2. Atalipwa pesa na kazi hatofanya hivyo huo mradi yatakuwa na tija kwa uchumi wa Nchi, lakini Asia kosa litakuwa moja tu namba moja kwamba kazi itatolewa kwa upendeleo, lakini kazi itafanyika hivyo kuwa na tija kiuchumi.

Nafikiri utakuwa umeelewa
This is not Asia bahati mbaya unless unataka kumaanisha kwamba alipewa kwa upendeleo na amefanya cha maana kitu ambacho sitakubaliana nawe and am not even ready to embark myself kwenye University work of arguments.
 
Haya yote ni matatizo ya katiba mbovu.
Katiba mpya inahitajika wakati huu kuliko wakati mwingine wowote.
Watu hawa tumewadekeza sana na wanazidi kuwa wezi na mafisadi siku hadi siku.

Mwinyi alikuwa na matatizo ya kuuza Loliondo bila aibu na maeneo ya wazi Dar yakachukuliwa. Mkapa akauza viwanda hovyo hovyo na kujiuzia yeye mwenyewe pia, akagawa Tanesco kwa Netgroup solutions ya SA, akagawa ATC kwa SA, migodi ikapewa watu, tukasikia ana hotel SA. Kikwete akaja kutia fola na IPTL, escrow aliyoonesha ushenzi eti siyo pesa za serikali, twiga wakauzwa uarabuni, TRC ikauzwa kwa wahindi, rada na chenji yake ikapotea, ukodishaji wa ndege, Bandari ya bagamoyo, n.k.

Magufuli haijaeleweka sana ni nini alichojineemesha. wengi wanasema Chato Chato lakini ujenzi wa chato kwa upendeleo, iwe airport, iwe hospitali, iwe Burigi N.P, vyote hivi ni vya serikali na wananchi na vimebaki tunaviona. Hawa wengine walijineemesha wao binafsi.

Sasa amekuja Samia ameanza kunadi Bagamoyo kwa nguvu zote, anawaachia mafisadi kama akina Singh kwa bei ya chini kuliko pesa walizo pora. Mwaka haujaisha lakini ni ishara kwamba yajayo yanafurahisha. Sidhani kama muda wa siku 100 ulimtosha kufahamu undani wa mradi na niya njema au mbaya juu ya mradi huu. Naweza kuhisi kwa 70% kwamba ameambiwa na wanaofahamu mradi ili aendelee, wafaidi. Wananchi anawapoza kwa kuwaambia analeta uhuru na demokrasia. Huu ni mtindo wa Mobutu alivyowaachia wakongo kucheza ndombolo yeye akipora.
 
Tujipime if it's not true.
 
Attachments

  • Botha's speech1.pdf
    71.2 KB · Views: 5
Nyerere alijenga umoja tangu mapema kabisa. Alichofanya kilikuwa ni msingi wa utaifa wetu tukumbuke kuwa yapo mataifa ambayo hayakuanza na umoja walianza na mawazo ya kikabila na kikanda, wakavurugikiwa mapema sana.

Kiuchumi hakuwa na chaguo ilibidi awe bepari au awe mjamaa. Alifanya kazi akiwa na mazingira magumu kulinganisha na wengine waliofuatia.

Hawa waliokuja kuanzisha mitandao ndio walivuruga kila kitu, wakaleta siasa za majungu na upambe wa kujikomba.
 
Tanzania Marais hawawajibiki wakiwa madarakani kwakua wakimaliza muda wao haijalishi walichokifanya Bado wanabakia na heshima zao ,

Hakuna wa kuwawajibisha.
Ni shamba la bibi wanajichotea wao na familia zao tu huku wananchi wa kawaida wakihimizwa kuwa wazalendo na kuipenda nchi yao.
 
This is not Asia bahati mbaya unless unataka kumaanisha kwamba alipewa kwa upendeleo na amefanya cha maana kitu ambacho sitakubaliana nawe and am not even ready to embark myself kwenye University work of arguments.
So Nyerere was embarking on "university argument " akili za kuambiwa changia na zako keep it Up and keep your points to yourself if you are closed minded person.

And second point you say this is not Asia, well and good, then you should note also this is not "Europe" hence one will be wondering what is your point at all. "A kindergarten point of view" or a recent graduate who is fixed to a certain village life or what he have heard
 
Watu hawa tumewadekeza sana na wanazidi kuwa wezi na mafisadi siku hadi siku.

Mwinyi alikuwa na matatizo ya kuuza Loliondo bila aibu na maeneo ya wazi Dar yakachukuliwa. Mkapa akauza viwanda hovyo hovyo na kujiuzia yeye mwenyewe pia, akagawa Tanesco kwa Netgroup solutions ya SA, akagawa ATC kwa SA, migodi ikapewa watu, tukasikia ana hotel SA. Kikwete akaja kutia fola na IPTL, escrow aliyoonesha ushenzi eti siyo pesa za serikali, twiga wakauzwa uarabuni, TRC ikauzwa kwa wahindi, rada na chenji yake ikapotea, ukodishaji wa ndege, Bandari ya bagamoyo, n.k.

Magufuli haijaeleweka sana ni nini alichojineemesha. wengi wanasema Chato Chato lakini ujenzi wa chato kwa upendeleo, iwe airport, iwe hospitali, iwe Burigi N.P, vyote hivi ni vya serikali na wananchi na vimebaki tunaviona. Hawa wengine walijineemesha wao binafsi.

Sasa amekuja Samia ameanza kunadi Bagamoyo kwa nguvu zote, anawaachia mafisadi kama akina Singh kwa bei ya chini kuliko pesa walizo pora. Mwaka haujaisha lakini ni ishara kwamba yajayo yanafurahisha. Sidhani kama muda wa siku 100 ulimtosha kufahamu undani wa mradi na niya njema au mbaya juu ya mradi huu. Naweza kuhisi kwa 70% kwamba ameambiwa na wanaofahamu mradi ili aendelee, wafaidi. Wananchi anawapoza kwa kuwaambia analeta uhuru na demokrasia. Huu ni mtindo wa Mobutu alivyowaachia wakongo kucheza ndombolo yeye akipora.
Mtu wa Chato huwezi kosoa mzaliwa wa Chato mwenzio kwa sababu wewe ni mojawapo ya kizazi cha nyoka mwenye sumu,katika vitu vya ovyo kabisa ni kutaka kuijenga Chato kuwa Dar wakati wananchi wakiteseka miaka mitano na robo bila ajira,mishahara kuongezewa,madaraja kazini kupandishwa,mzunguko wa pesa nchini ukiwa hafifu,uhuru wa kweli kwa Watanzania walio wengi kzorota na mateso ya kila aina,Bora hao uliowataja Watanzania walikula mema ya nchi yao kwa ujumla wao kuliko huyo unayesema alijenga Chato na kuiachia nchi umaskini wa kutupwa.
 
Nyerere hakua mzalendo kama wengi tunavyo mpamba alitambua kbs ratiba aliyo i copy nchi za koloni ni mwiba na inatoa mwanya kwa viongozi wa africa kufanya utopolo alishindwa nn kuturithisha katiba yenye kubeba maono ya tanzania tunayoitamani
 
Nyerere alifeli kwenye Mambo haya kwa mtazamo wangu .

1.Katiba Bora na Safi .

2.uchumi imara na madhubuti.

Ila alijitahidi kwenye mengi.Ndio maana anaimbwa Hadi Leo

Hawa wengine watasaulika tu maana wanajiende tu
 
Sasa kujipa tenda kuna ubaya gani kama kampuni ipo na imetimiza vigezo? Kwamba wewe usiajiriwe ofisi aliyepo baba yako kama afisa muajiri ikiwa umeomba nafasi na sifa unazo! Hebu acheni chuki za kishamba jamani
Na utakuta alitoa fursa za ajira labda iwe waajiriwa wote ni wanafamilia jambo lisilowezekana.
 
Dah! Ni hawa hawa wanajengewa nyumba za kustaafu. Hapo ni baada ya kutuibia!

Kama Samia ana akili ya wizi basi ametia fola na yeye maana ndani ya siku 100 anawazia miradi yenye kuleta ugomvi kiasi hiki? Hii imenikumbusha makara ilionesha wezi wa Indonesia na Malaysia wanavyosaidia nchi zao kwa mali walizoiba. Mtoto wa Suharto akajenga kiwanda cha kuunda magari nchini. Mi naomba tumruhusu kuiba lakini ajenge reli yake nchini Zanzibar ili iwasaidie usafiri.
Wizi hauna manufaa hiko kiwanda cha magari hakishindani ya hyundani ya Korea wakati wote walikua sawa
 
Nyerere alitambua hii Katiba iliyopo inaweza kumfanya kiongozi awe dikteta, lakini sio yeye wala wasaidizi wake kina Kawawa na wengine walioona umuhimu wa kuibadilisha, na wakati huo upinzani ungeweza kuwa mdogo kwasababu ungetoka ndani ya chama, na zaidi wasomi wa kuibadilisha kina jaji Warioba walikuwepo.

Lakini baada ya vyama vingi kuanzishwa, na madudu yanayofanywa na viongozi wa CCM na serikali yao, kuipata Katiba Mpya ndio umekuwa mfupa mgumu zaidi, jamaa wanaogopa kubadili katiba kwa kuhofia kuburuzwa mahakamani kwa wizi walioufanya kwa hili taifa.

Vyema tutambue tu haya mapambano sio madogo, ni mtihani wa kweli kuipata Katiba Mpya, tukicheza tutaendelea kupiga kelele tu Katiba Mpya mpaka ugeuke wimbo, kuipata Katiba Mpya kwa kusubiri ruhusa toka kwa mwenyekiti wa CCM ni ndoto, sasa inahitajika mbinu/njia mpya.
Unaishia kusema tu inahitajika mbinu , Sasa hizo mbinu unategemea upewe na nani kama wewe mwenyewe umeshindwa kuziweka hapa?
 
JKN na JPM wapo mbaaali kabisa na hao wengine uliowataja.Hawa waliyajua mamlaka yao.Hawakuyumbishwa na kuendeshwa 'external force' kama hao wengine.Walikua wazalendo na waliumwa na umaskini wetu.Walikua na 'vision' na 'mission' ya kututoa nyikani.Hawa wengine walikua ni vibaraka wa genge la wanyang'anyi wa nje na makuwadi wao hapa nchini.Wizi,ubinafsishaji holela,upendeleo,siasa za makundi na batili nyingine nyingi ndio ilikua mtindo wa Serikali zao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom