Ukimuacha Nyerere, makosa ya Marais wetu ni ya makusudi kwa manufaa ya familia zao

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
Watu hawa tumewadekeza sana na wanazidi kuwa wezi na mafisadi siku hadi siku.

Mwinyi alikuwa na matatizo ya kuuza Loliondo bila aibu na maeneo ya wazi Dar yakachukuliwa. Mkapa akauza viwanda hovyo hovyo na kujiuzia yeye mwenyewe pia, akagawa Tanesco kwa Netgroup solutions ya SA, akagawa ATC kwa SA, migodi ikapewa watu, tukasikia ana hotel SA. Kikwete akaja kutia fola na IPTL, escrow aliyoonesha ushenzi eti siyo pesa za serikali, twiga wakauzwa uarabuni, TRC ikauzwa kwa wahindi, rada na chenji yake ikapotea, ukodishaji wa ndege, Bandari ya bagamoyo, n.k.

Magufuli haijaeleweka sana ni nini alichojineemesha. wengi wanasema Chato Chato lakini ujenzi wa chato kwa upendeleo, iwe airport, iwe hospitali, iwe Burigi N.P, vyote hivi ni vya serikali na wananchi na vimebaki tunaviona. Hawa wengine walijineemesha wao binafsi.

Sasa amekuja Samia ameanza kunadi Bagamoyo kwa nguvu zote, anawaachia mafisadi kama akina Singh kwa bei ya chini kuliko pesa walizo pora. Mwaka haujaisha lakini ni ishara kwamba yajayo yanafurahisha. Sidhani kama muda wa siku 100 ulimtosha kufahamu undani wa mradi na niya njema au mbaya juu ya mradi huu.

Naweza kuhisi kwa 70% kwamba ameambiwa na wanaofahamu mradi ili aendelee, wafaidi. Wananchi anawapoza kwa kuwaambia analeta uhuru na demokrasia. Huu ni mtindo wa Mobutu alivyowaachia wakongo kucheza ndombolo yeye akipora.
 
Dah! Ni hawa hawa wanajengewa nyumba za kustaafu. Hapo ni baada ya kutuibia!

Kama Samia ana akili ya wizi basi ametia fola na yeye maana ndani ya siku 100 anawazia miradi yenye kuleta ugomvi kiasi hiki? Hii imenikumbusha makara ilionesha wezi wa Indonesia na Malaysia wanavyosaidia nchi zao kwa mali walizoiba. Mtoto wa Suharto akajenga kiwanda cha kuunda magari nchini. Mi naomba tumruhusu kuiba lakini ajenge reli yake nchini Zanzibar ili iwasaidie usafiri.
 
Nyerere alitambua hii Katiba iliyopo inaweza kumfanya kiongozi awe dikteta, lakini sio yeye wala wasaidizi wake kina Kawawa na wengine walioona umuhimu wa kuibadilisha, na wakati huo upinzani ungeweza kuwa mdogo kwasababu ungetoka ndani ya chama, na zaidi wasomi wa kuibadilisha kina jaji Warioba walikuwepo.

Lakini baada ya vyama vingi kuanzishwa, na madudu yanayofanywa na viongozi wa CCM na serikali yao, kuipata Katiba Mpya ndio umekuwa mfupa mgumu zaidi, jamaa wanaogopa kubadili katiba kwa kuhofia kuburuzwa mahakamani kwa wizi walioufanya kwa hili taifa.

Vyema tutambue tu haya mapambano sio madogo, ni mtihani wa kweli kuipata Katiba Mpya, tukicheza tutaendelea kupiga kelele tu Katiba Mpya mpaka ugeuke wimbo, kuipata Katiba Mpya kwa kusubiri ruhusa toka kwa mwenyekiti wa CCM ni ndoto, sasa inahitajika mbinu/njia mpya.
 
Laiti ungejua kampuni iliyojenga Chato airport, Uboreshaji wa Dodoma na aliyepewa tenda ya kusupply malori kule Nyerere HEP huyo Meko usingemtoa kwenye list kabisa aisee.

Fanya research zaidi. Ulizia yule dogo bonge aliyekuwa kwenye Landcruiser nyeusi mbele ya msafara wa mazishi ana cheo gani kwenye kampuni ya dingi yake? Anasimamia tenda ngapi? Walizipataje?

Ukipata majibu njoo uedit Uzi wako.
 
Tanzania Marais hawawajibiki wakiwa madarakani kwakua wakimaliza muda wao haijalishi walichokifanya Bado wanabakia na heshima zao ,

Hakuna wa kuwawajibisha.
 
Tanzania Marais hawawajibiki wakiwa madarakani kwakua wakimaliza muda wao haijalishi walichokifanya Bado wanabakia na heshima zao ,

Hakuna wa kuwawajibisha.
But for crimes walizocommitt wakiwa madarakani wanakuwa held liable individually. Yani kama Meko angekuwepo aisee na amemaliza muda na tukaweka mfumo mzuri wa haki angelambwa mvua nyingi sana maana sio kwa hizi siri ambazo mama anazifukua na kuziacha watu wajaji utendaji wenyewe.
 
Nyerere alitambua hii Katiba iliyopo inaweza kumfanya kiongozi awe dikteta, lakini sio yeye wala wasaidizi wake kina Kawawa na wengine walioona umuhimu wa kuibadilisha, na wakati huo upinzani ungeweza kuwa mdogo kwasababu ungetoka ndani ya chama, na zaidi wasomi wa kuibadilisha kina jaji Warioba walikuwepo...
Hio mbinu itaje ili tuijue😅😅😅
 
Laiti ungejua kampuni iliyojenga Chato airport, Uboreshaji wa Dodoma na aliyepewa tenda ya kusupply malori kule Nyerere HEP huyo Meko usingemtoa kwenye list kabisa aisee...
Sasa kujipa tenda kuna ubaya gani kama kampuni ipo na imetimiza vigezo? Kwamba wewe usiajiriwe ofisi aliyepo baba yako kama afisa muajiri ikiwa umeomba nafasi na sifa unazo! Hebu acheni chuki za kishamba jamani
 
Kiini cha matatizo yote ni Nyerere aliweka misingi mibovu sana ya kiongozi na mbaya zaidi aliwatengeneza wananchi wake kuwa mandondocha hatuoni wala hatusikii.

Watu wanao msifia nyerere huwa nawaona na utindio wa ubongo kabisa.kina kazi kubwa sana ya kubadilisha mitazamo ya Watanzania kuhusu.nyerere alaniwe popote alipo.
 
Watu hawa tumewadekeza sana na wanazidi kuwa wezi na mafisadi siku hadi siku.

Mwinyi alikuwa na matatizo ya kuuza Loliondo bila aibu na maeneo ya wazi Dar yakachukuliwa. Mkapa akauza viwanda hovyo hovyo na kujiuzia yeye mwenyewe pia, akagawa Tanesco kwa Netgroup solutions ya SA, akagawa ATC kwa SA, migodi ikapewa watu, tukasikia ana hotel SA...
Mwanangu una akili sana na una bonge la hoja hapa. Uroho, upofu, upogo na kutoona mbali ndiyo chanzo cha walio wengi. Hata Magu alikuwa anajitahidi japo hakufikia mwisho.
 
Sasa kujipa tenda kuna ubaya gani kama kampuni ipo na imetimiza vigezo? Kwamba wewe usiajiriwe ofisi aliyepo baba yako kama afisa muajiri ikiwa umeomba nafasi na sifa unazo! Hebu acheni chuki za kishamba jamani
Well, unajua kanuni za Utumishi wa umma kwanza inakutaka wewe boss mhusika ku-declare interest ili tujue kama haujajipendelea kwenye kujipa kazi.

Ukiangalia tenda alizopata ni hakuna competitive bidding fuatilia Ile ya ujenzi wa airport.

Kujipa tenda ni kosa mzee sio ushamba unless unafurahia tuendeleza kujipa kazi, watoto wetu ndio wapate kazi, wajomba na mashangazi na vimada wetu.

Sijui tutaishia wapi🤷
 
Kiini cha matatizo yote ni Nyerere aliweka misingi mibovu sana ya kiongozi na mbaya zaidi aliwatengeneza wananchi wake kuwa mandondocha hatuoni wala hatusikii.
Watu wanao msifia nyerere huwa nawaona na utindio wa ubongo kabisa.kina kazi kubwa sana ya kubadilisha mitazamo ya Watanzania kuhusu.nyerere alaniwe popote alipo.
Kwa watu ambao hawajatoka nchini na kuona watu wa tabaka lao wanavyosota, hawawezi kumuelewa Nyerere. Huyu baba anaeleweka kwa wenye uzoefu na uoni wa mbali. Mie thesis yangu nilifanya Ujamaa namna ambavyo unaweza kusaidia nchi zenye ukabila barani Afrika na tena nilifanyia Marekani nchi ya kibepari.
 
Well, unajua kanuni za Utumishi wa umma kwanza inakutaka wewe boss mhusika ku-declare interest ili tujue kama haujajipendelea kwenye kujipa kazi.

Ukiangalia tenda alizopata ni hakuna competitive bidding fuatilia Ile ya ujenzi wa airport.

Kujipa tenda ni kosa mzee sio ushamba unless unafurahia tuendeleza kujipa kazi, watoto wetu ndio wapate kazi, wajomba na mashangazi na vimada wetu.

Sijui tutaishia wapi🤷
Ukiniambia hilo nitakuelewa kwamba hawakushindanishwa! Ila pia kimsingi viongozi wote hata Msowger guy alikuwa anawapa tender washakaji na first borne wake riz moko what did you expect the later to do. Hawa jamaa wa chichiem walipoitwa ukoo wa panya sikuelewa but kwa sasa nimeshaelewa, mie siwezi ona we unakwarua na kuunda michakato ya kupiga halafu nikapata nafasi namimi af niache kupiga. Kiwango cha imani tu ndio kitatofautisha aina za upigaji maana kuna ule wa waziwazi kabisa na mwengine ni indirectly kama kujipa tenders and shiit!

The issue ni kuwa jina la kampuni halishabihiani na la ukoo you can never prove dat nepotism shiit ila impliedly inaeleweka kampuni ni yao.
 
Kwa watu ambao hawajatoka nchini na kuona watu wa tabaka lao wanavyosota, hawawezi kumuelewa Nyerere. Huyu baba anaeleweka kwa wenye uzoefu na uoni wa mbali. Mie thesis yangu nilifanya Ujamaa namna ambavyo unaweza kusaidia nchi zenye ukabila barani Afrika na tena nilifanyia Marekani nchi ya kibepari.

Tanzania haikuwa na wala haina ukabila hivyo Ujamaa haukutufaa kabisa??!!
 
Ukiniambia hilo nitakuelewa kwamba hawakushindanishwa! Ila pia kimsingi viongozi wote hata Msowger guy alikuwa anawapa tender washakaji na first borne wake riz moko what did you expect the later to do. Hawa jamaa wa chichiem walipoitwa ukoo wa panya sikuelewa but kwa sasa nimeshaelewa, mie siwezi ona we unakwarua na kuunda michakato ya kupiga halafu nikapata nafasi namimi af niache kupiga. Kiwango cha imani tu ndio kitatofautisha aina za upigaji maana kuna ule wa waziwazi kabisa na mwengine ni indirectly kama kujipa tenders and shiit!

The issue ni kuwa jina la kampuni halishabihiani na la ukoo you can never prove dat nepotism shiit ila impliedly inaeleweka kampuni ni yao.
Ingiza kwenye BRELA hili jina MAYANGA utapata coinage ya hilo jina ni majina ya kwanza ya partners/directors mzee.

Anyway ishu sio hiyo kampuni wacha wale basi tuingie CCM tuibe na watoto zetu naona labda iwe hivyo tu.
 
Now you’re talking,,,lets get to the bread factory! Tusipige kelele kwa tunaowaona through the glass window wakiwa zao ndani wanakula sababu they fought for that in one way or the other awe alibebwa au alipambana its fine!

Maisha ndio yalivyo tu chief!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom