Ukimsikia Mtanzania anasema wakosoaji wapotezwe au wakaozee jela unajisikiaje mtu wa Mungu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Nchi Ina sheria kwa wanaozivunja wanatakiwa kufikishwa mahakamani lakini tumezoea viongozi wakitaifa wakisema wakosoaji wakaozee jela au wapotezwe, Hawa watu unapowasikia unawachukuliaje?

Mfano sheria ya mtu aliyekosoa au kutukana Ina kifungo cha mwaka mmoja then ukamsikia mwanasiasa anaviambia vyombo vya Dola huyo akaozee jela unapata maana au tafsiri Gani? Kwamba wampe kesi ya Ugaidi, ubakaji, au uhaini si ndivyo?

Nawewe unaposikia kauli hii mtu wa Mungu Huwa unachukua hatua yoyote hata kukemea moyoni au huwa unashangilia Kwa sababu aliyesema ni kiongozi wa chama chako?

Sikiliza nikwambie mtu wa Mungu, endapo utaona mwanasiasa kumuua Mpinzani wake au kumfunga kwa kumbambia kesi ni sawa tambua ipo siku atauawa ndugu Yako na mamlaka zitakuwa zimezoea na hata ndugu zako nao watasema huyu alikuwa anaringa sana, sijui tulikuwa atusalimiani nk

Nataka kusema Nini? Ogopa sana kuruhusu nafsi kusherekea mauaji. Ogopa sana kuwa mwanachama wa kikundi cha watu walioamua Bora watu wafe lakini taasisi Yao iwe hai. Ogopa sana kuhudumu na mtu anayepanga njama za kuua Kwa hisia zake binafsi.

Tunapaswa kushirikiana na taasisi zinazoamini kwamba ukosoaji ni Jambo lisiloepukika na ambalo kulizima Kwa mauaji nikulipalilia makaa na kutengeneza uasi.

Tunashuhudia mauaji yanayotekea Kila siku,zamani tulizoea jamii ikipaza sauti lakini miaka ya hivi karibuni hakuna anayepaza sauti maana yake kuua kunaanza kuwa maziea ya watu, kumwaga damu kunaanza kupata justification kwenye nafsi za watu.

Unapomsikia Msemaji wa familia ya Mo Dewji inasema wakosoaji wapo nje wanakula raha bila kujiuliza kwani ni wapo nje na kauli hii anaitoa mbele ya viongozi wa dini maana yake yeye Mwenyewe anaamini wakosoaji awapaswi kuwepo na may be mamlaka ya Rais inapaswa kuwanyamazisha bila kusema wametenda kosa Gani?

Juma Duni nikiongozi wa ACT, anatamka adharani kwamba watu wanakula kuku nje, anamaanisha kwamba yeye anakubaliana yote yaliyofanywa Kwa Lema na Lisu na kwamba hata yeye angafanya hivyo Kwa wakooaji wake.

Katika kauli hizi hakuna anayekemea na tusipokemea Sasa tunafanya iwe silka na ikiwa silka maana yake kupata madaraka Tanzania kutatokana na ñguvu Yako yakuwadhoofisha wanaokupinga bila kujali mbinu zako zinazingatia sheria au la.

Lakini Hawa watu niliowataja wanaonyesha ubinafsi mkubwa uliopo baini kwamba Mo alipotekwa wakosoaji wakapiga kelele walikuwa sahihi Kwa sababu ni mtoto wao lakini wanaobaki ambao siyo damu Yao kwao siyo hitajio. And this goes far kwamba watu wote waliotekwa na kuteswa nchini familia ya Mo haikuwahi even kutweet. Wanaotakiwa kuishi na wasiotakiwa kuishi.

Ni maombi yangu kwamba Kama una nafasi yakuomba omba roho ya mauaji iondoke Kwa Watanzania. Omba roho yakuona binadamu ulionao damu Moja ni wazuri kuishi kuliko wengine, omba sana tuondokana na wanadamu wanaowaza kumwabudu binadamu badala ya kumwabudu Mungu.

Tupo pabaya sana, mauaji for six years bila ukomo siyo Jambo dog, tumejeruhi nafsi nyingi sana. Tuombe zisiwaze kulipiza kisasi Kwa sababu tutawafahamu baada ya kulipiza kisasi na siyo kabla. Tungeweza kuwafahamu wanaotaka kulipiza tungewadhibuti lakini nivigumu kuwajua maana tunakula nao na kuishi nao.
 
Ukosoaji gani wa kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania inyimwe mikopo, itengwe kisiasa , kiuchumu, na kidiplomasia?
 
Ukichunguza kwa kina, utagundua karibia wote wana mafungamano na nchi jirani, au ni wahamiaji haramu kama yule Mzee aliyefariki mwaka wa jana.

Ila kwa Watanzania wazawa, hizo mambo hatuna.
Watanzania wazawa ni binadamu kama Waafrika wengine wowote katika bara hili.
Tusidanganye sisi ni special sana. Sisi ni Waafrika kama walivyo wahutu, watusi, wabaganda, wajaluo wa kenya, wakikuyu, wasudani n.k
 
Mtu yeyote yule anayetamani kuona wakosoaji wake wakipata matatizo ni mbumbumbu, mgonjwa na maskini wa kujitambua...!
Kuthibitisha hilo mara zote wanawaza kudhuru mwili na hata kuua, wakiamini kufanya hivyo wanadhibiti ukosoaji!
 
Ufisadi,, ubinafsi,,, ukabila..

Hii nchi ngumu sana.... Only God knows...
 
Back
Top Bottom