Ukimsajilia mtu line jela inakuita

Ukimsajilia mtu line jela inakuita

Chibudee

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
1,775
Reaction score
2,408
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepiga marufuku Watu wenye vitambulisho vya NIDA kuwasajilia wenzao wasiokuwa navyo laini zao kwa alama za vidole kwa madai ya kuwaokoa wasifungiwe.

“Atakayebainika anatumia namba yake ya NIDA kumsajilia laini mwenzake, adhabu ni kulipa faini isiyopungua Million 5 au kwenda jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja”



- TCRA
FB_IMG_1579337831684.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmmmh, kwani lengo hasa la sarakasi zote hizi ni nini, kukomoana au?

Mimi nilidhani wangesema ukimsajilia mtu kisha akatenda kosa la jinai kwa kutumia hiyo simu ndio jela itakuita, ila kumsajilia tu? Kwani kuna nini nyuma ya pazia na huu usajili hivi?
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepiga marufuku Watu wenye vitambulisho vya NIDA kuwasajilia wenzao wasiokuwa navyo laini zao kwa alama za vidole kwa madai ya kuwaokoa wasifungiwe.

“Atakayebainika anatumia namba yake ya NIDA kumsajilia laini mwenzake, adhabu ni kulipa faini isiyopungua Million 5 au kwenda jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja” - TCRAView attachment 1326472

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaelewa mfano Kuna watoto wadogo chini ya miaka 18 ambao wanasoma shule za mbali na hawawezi sajili vitambulisho vya NIDA sababu hawajafikia umri wa kusajili inakuwaje ?

Hawahitaji kusajiliwa Simu na wazazi wao?
 
Nikiwa na simcard 2 kwa kampuni moja mathalani tigo kuna kosa?
Sio kweli mfano una duka lazima uwe na Simu ya dukani na ya kwako.Sababu wafanyakazi huacha kazi kila uchao na Simu ya biashara haitakiwi kabadilika badilika. Sasa Kama umeupenda mtandao mmoja unasajili .

Na Simu ya kwako Kama boss haitakiwi kabadilika badilika

Nyumbani pia Kama una mtoto mdogo au mfanyakazi sio salama asajili Simu yake atumie atumie home phone sio yake.Cha msingi likitokea la kutokea uwe tayari kujieleza Simu hiyo ilifikaje kwa huyo .

Lakini naaamini Kama umesajilia watoto ambao hawana vitambulisho vya NIDA sio big deal .Ila Kama umesajilia hovyo hovyo likatokea la kutokea utakoma.

Mfano Nina jirani aliombwa simu na hawara Yake bar maid amsajilie Simu kwa jina lake anasema na urafiki uliishia hapo hapo akajua kitakachofuata Ni jela laini bar maid aweza wapa majambazi ikatumika kwenye ujambazi
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] Yope
Wamemfunga nani mpaka kufikia Jana SAA 8 mchana,kama serikali imeshindwa hata kuwazia madereva wasio na leseni kuendesha vyombo vya moto wataweza kweli kutuzuia kutumia line za simu za michepuko yetu,hawataweza hata wakipiga yope

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakawatishe wake zao.. nchi ni ya kwetu hii.

Jishindwe kumsajilia mtoto wangu.

Akili matope
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepiga marufuku Watu wenye vitambulisho vya NIDA kuwasajilia wenzao wasiokuwa navyo laini zao kwa alama za vidole kwa madai ya kuwaokoa wasifungiwe.

“Atakayebainika anatumia namba yake ya NIDA kumsajilia laini mwenzake, adhabu ni kulipa faini isiyopungua Million 5 au kwenda jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja”

Ktk huu Mpango Nahisi Kunakitu Kina pikwa hapa kitaiva Soon tu..

- TCRAView attachment 1326472

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaounga mkono ugaidi endeleeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa kupata vitambulisho vya NIDA ni magaidi?

Basi shusheni umri wa kupata vitambulisho vya NIDA hata mtoto mdogo apewe.Kukataa asisajiliwe hata na Mzazi Ni hatari watoto wanarudi mashule usiku Wengine hukatiza mapori hatarishi Simu inamsaidia likitokea la kutokea kumtaarifu Mzazi.Mtoto huwezi acha anaenda shule mbali na kurudi asiwe na Simu huyo ambaye hajafikia umri wa kupata kitambulisho Cha NIDA
 
Back
Top Bottom