figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,662
- 59,100
Tanzania bora ukamatwe na Polisi sio LATRA. Kwanza hawahongeki, hawazoeleki, hawaonei wala hawana huruma.
Hata haya mambo ya Foleni wakiachiwa kazi LATRA, mambo yatanyoka.
Afisa huyo wa LATRA akikukamata, atakusalimia kisha atakuomba kukukagua.
Mfano kwa wanaobeba abiria, atakagua utekelezaji wa masharti ya leseni kama vile;
1. Dereva umethibitishwa?
2. Mhudumu umesajiliwa?
3. Dereva umevaa sare?
4. Gari lina leseni hai ya LATRA au kibali?
5. Gari lipo kwenye ruti yake?
6. Gari limefuata ratiba?
7. Kondakta anatoa tiketi za kielektroniki?
8. King'amuzi kimechezewa?
9. Abiria wamepewa tiketi?
10. Abiria wametozwa nauli halali?
11. Kama ni daladala limewekwa mkanda? Na kuonesha linapotoka na linapokwenda?
12. Na masharti mengine mengi kadiri yanavyotolewa na kanuni mbalimbali.
Ambacho Afisa wa LATRA haruhusiwi kukagua tu ni usalama wa gari yaani (Roadworthiness) mara nyingi huitwa "Uwezo wa gari kutembea barabarani" au "Hali ya gari kufaa barabarani") ni hali ya chombo cha moto (gari, basi, lori, n.k.) kuwa katika hali nzuri ya kiufundi na kiusalama inayokubalika kisheria ili kuendeshewa barabarani bila kuhatarisha maisha ya watumiaji wengine. Roadworthiness ni jukumu la Polisi.
Je, ushawahi kukutana Afisa wa LATRA? Ulijinasuaje?