Ukiitwa kazini Serikalini, kuna pesa ya awali ya kujikimu?

Lung'wecha

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
927
574
Nauliza ndugu zangu

Unapoitwa kazini Serikalini inakuwaje kuhusu pesa ya kuanzia maisha hapo kazini? Je, nauli hurudishiwa? ( Kama umetoka nje ya mkoa) au huwa kuna salary advance?

Mwenye kujua msaada tafadhali!
 
Yah pesa ya kujikimu ipo nauli unarudishiwa na pia waweza pata fringe benefit zingine kutokana na position/ kazi uliyopata.
Ungeweka wazi umeajiriwa kitengo gani na kama nani tunaweza kukupa maelezo zaidi Mkuu....
 
Upo sahihi but mizigo Ni 1.5 tons kwa cheo chake kwa waraka mpya wa marekebisho (machi 2011)
 
ukweli ni kwamba kwa sheria za sasa hv unalipwa hela 45000 mara siku 7 but kwa siku za nyuma ilikuwa mara kumi na nne.

Je,ukiajiriwa kwenye mashirika ya umma kama TFDA,TBS,NDC.kwa mkataba,wanatoka hela za kujikimu kulingana na kanuni ya UTUMISHI au wana viwango vyao.msaada plz
 
Tgs nfo zinaangaliwa km upo A hadi B ni 45000×7 na km kuqnzia C ni 65000×7 hizo ndo calculation za pesa ya kujikimu
 
Nauliza ndugu zangu

Unapoitwa kazini Serikalini inakuwaje kuhusu pesa ya kuanzia maisha hapo kazini? je nauli hurudishiwa? {kama umetoka nje ya mkoa} au huwa kuna salary advance?

Mwenye kujua msaada tafadhali!
Utapewa posho ya kujikimu kwa siku 7, na kama una mke naye atapewa siku 7. Kama una watoto nao wanapewa nusu ya posho yako kwa siku 7. Idadi ya watoto haitakiwi kuzidi wanne. Kiasi cha posho kwa siku inategemea unaenda kuanzia kazi Wilayani au katika miji mikuu ya mikoa na jiji. Kwa kiwango cha sasa kwa Wilayani posho ni elfu 45 kwa siku na kwa miji mikuu ya mikoa na majiji ni elfu 65 kwa siku.
 
14days allowance 4watoto na mke. Watoto half amount. Mizigo 7ton
kwa waraka wa mwaka 2011 ni siku 7 kwa anayeenda kuanza kazi ika kwa uhamisho ndo siku 14. Kwa anayeanza kazi kwa waraka wa sasa hamna fedha ya mizigo, kwa anayehama ndo kuna fedha mizigo kama siyo uhamisho wa kujihamisha.
 
Je,ukiajiriwa kwenye mashirika ya umma kama TFDA,TBS,NDC.kwa mkataba,wanatoka hela za kujikimu kulingana na kanuni ya UTUMISHI au wana viwango vyao.msaada plz
Ni kanuni za utumishi wa umma lakini kanuni hazifanani kwa sekta zote ndo maana hata mishahara intofautiana, mfano anayeanza kazi shirika la umma au katika mamlaka kama TANAPA, TANESCO, TRA n.k anakuwa na mshahara mkubwa kuliko anayeanza kazi Serikali kuu/Wizarani au Serikali za mitaa hata kama watu hao wana elimu inayofanana.
 
sasa wadau hzo TGS mbona zinachanganya maana taasis nyingine wanatumia madaraja mengine mfano..POSS 4! hapo inakuwaje?
 
Back
Top Bottom